Ni harufu ya ufisadi tu! Mikataba mikubwa ya trilioni ya pesa haiwekwi wazi na wala Bunge hatusikii likihusishwa. Tunaibiwa tushtuke kabla ya 2025

JPM yupi aliweka mkataba wazi? Nitajie mkataba mmoja tu uliowekwa wazi na serikali yake?? Sheria tu za madini zilitungwa usiku usiku kwa hati ya dharura ndio eti alikua muwazi.

JPM alijitoa OGI, Alipinga sheria ya TEITI iliyotaka mikataba iwe wazi alafu mnakuja kumlaumu Mama Samia?
 
Kwenye madini sakata ya Acacia, Barrick hujua chochote, Tanzania inanufaika vipi?

Naona ni mambo ya ligi za kitoto, Info zote zipo hapa JF.
 
Walishagawana vya kwao tayari, unadhani kwanini pale kawekwa January?
 
Ndiyo maana nishati yupo Makamba na ardhi yupo Kikwete fedha Mwigulu hakuna namna lazima nchi itafunwe haswa
 
Bakuli la Dubai linawapa Jeuri.
A guarantee, 'election' security vis-a-vis investment security. Binafsi 'sishtuki' lakini harufu kali inayotoka, inakufuru harufu.



Nahisi kuna marobota??(sio bakuli) hivyo kuna nguvu ya kunyamazisha ya kuwafanya (wabunge)waangalie kwingine wakati Minada na Ufisadi ukishamiri lakini sijafa moyo wanapigika, watashindwa! Wao ndio "Walioibiwa" Uzalendo.



Usicheze na nguvu ya Mwananchi tena mwenye njaa! nilichobakiwa nacho ni karata hii wala sio "Joker" ni Kura tu! Ni nguvu!

Pamoja na kelele zangu kwa sasa wacha hawa "Wastaa-arabu" wacheze karata zao, watajua "Uungwana" wangu.

Kweli kunanuka, ila kuna ile siku(tarehe kapuni)2025 CCM na Bunge lao watasikia harufu ya machungu ya Wananchi....Watamkumbuka Hayati J.P.M. hatakuwepo kuwasaidia.


CCM must go jamani dah
 
CCM OYEEEE
Hapo siyo CCM tu, chadema wanahusika. Waliopokea bahasha kwa msoga ili kuzima ajenda walikuwa CCM?

Yanayoendelea Ngorongoro yalianza kitambo, lakini watu wako bize na chai ya mama na hawamwonyi kuhusu hili.

Kifupi chadema wameolewa rasmi na CCM na wanakula sahani moja.
 
Mikataba iwekwe wazi , wawakilishi wa wananchi wajue kwakuwa kazi yao ni kusimamia nakuishauri serikali kama kweli mikataba hiyo imezingatia maslahi mapana ya Taifa ,,,
Bunge gani sasa akina babu tale na mwana FA? Lissu aliwaambia ingia mtaani kura zimeibiwa kila mtu akawa bisy na shughulizake mkitegemea watu waibe kura kisha wakuletee mikataba ya gesi nyumbani kwako?siku nyingine mkiambiwa na Lissu msikilize au mkubali yaishe mtu kama anaweza kupanga matokeo ya uchaguzi anashindwa nini?
 
HAKUNA BUNGE ndio maana KIKUNDI cha Watu SERIKALINI wanamaliza kila kitu



Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Sasa mbona na wewe unamchomeka ati "Mama Samia"

Halafu akitunguliwa na maneno yake uje useme "Hapendwi kwa sababu mwanamke" Hawampendi kwa sababu ni "Udini"
Sasa usishangae nimefika vipi na hayo juu


Huyo amesema JPM..."alituambia" na hakusema kuweka wazi.

Tiendelee
 
Wanaodai katiba mpya mnawaonaga wajinga, katiba ya zamani inampa mamlaka rais kusain mkataba bila kuwashirikisha wananchi
 
Kwenye madini sakata ya Acacia, Barrick hujua chochote, Tanzania inanufaika vipi?

Naona ni mambo ya ligi za kitoto, Info zote zipo hapa JF.
Kisiasa mbona hata mkataba huu ungeweza kuambiwa utakavyonufaika na Raisi angeweza kutengeneza mazingira ya kusaini mbele ya camera na kisha kutoa hotuba.

Swali ni, Ili tuseme mkataba umewekwa wazi ni jambo gani linafanyika?
 
Mikataba iwekwe wazi , wawakilishi wa wananchi wajue kwakuwa kazi yao ni kusimamia nakuishauri serikali kama kweli mikataba hiyo imezingatia maslahi mapana ya Taifa ,,,

JPM alisemwa sana kwa hili mara baada ya kuumaliza mwendo, tena alisemwa na kusemwa na hawa hawa walioko madarakani sasa na wenyewe wangoje wasubiri wafanye retirement.
 
Watanzania ni wanafki sana waache waonje joto la jiwe
 
USA+Rostam+kikwete+SSH.

Tafuta tu ugali wa watoto, maana hamna kitu unaweza fanya ukiforce utanyang'anywa
uhai.

Bado dili moja kaa kwakutulie ut
tt
 
Mikataba ya ndege,sgr,Bwawa la Nyerere nk viliwekwa wazi? Jumla ni Til.ngapi?

Kwa hiyo ni piga nikupige? Kuharalisha ujinga kwa upumbavu? Si ni nyinyi mliokuwa mnapiga kelele za utawala wa JPM ulificha uwazi wa mikataba na SSH yuko wazi? Nyie vijana wa keyboards na buttons hamna chochote mnachojua katika serikali inavyoendeshwa, ukichagua kuwa chawa wewe kuwa chawa tu tabia za kunguni muwache.
 
Kwenye madini sakata ya Acacia, Barrick hujua chochote, Tanzania inanufaika vipi?

Naona ni mambo ya ligi za kitoto, Info zote zipo hapa JF.

Ukibishana na chawa tena hawa buggs jr hawa utapoteza muda. They are brainwashed brainless kwa medulla oblangata zao. They have no sense of empathy wala rational thinking [emoji189]
 
Wewe unajua serikali inavyoendeshwa?
 
USA+Rostam+kikwete+SSH.

Tafuta tu ugali wa watoto, maana hamna kitu unaweza fanya ukiforce utanyang'anywa
uhai.

Bado dili moja kaa kwakutulie ut
tt
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…