Ni hatari sana kwa nchi kutegemea ushauri wa Legal Officer (Hamza Johari), na kuiingiza nchi kwenye mkataba

Tunakwenda wapi?
 
Shida ni moja tu, taaluma zina matter only zinapo support agenda ya chama kikuu. Zikianza kupinga zinakuwa ignored, black painted, hata kudharaulika.
Bad news ni kwamba chama husika kinatumia class 7 to do that dirty job
Musukuma.
Lusinde.
Zungu
 
.Wale mnaolaumu wanasheria, tujiulize kwanza, Je aliyetoa ushauri wa kisheria ni mwanasheria kwa mujibu wa taaluma yetu ya kisheria?

Na kama si hivyo, aliwezaje kufanya kazi asiyokuwa na taaluma nayo?
Very valid arguments, ila kwagu mimi mbona hili ni dogo tuu!.

Katiba ndio sheria Mama, sheria nyingine yoyote inayokwenda kinyume cha katiba ni sheria batili.

Tanzania tuna wanasheria lukuki, manguli wabobezi na wabobevu wa sheria lakini serikali yetu imetunga muswada wa sheria batili, ukaupeleka Bungeni, kutungwa kuwa sheria.

Bunge letu lililosheheni wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu, wakaijenga sheria batili hiyo!.

Mahakama Kuu ikaitamka sheria hiyo ni batili, serikali ikakata rufaa kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu na kupeleka Bungeni muswada wa marekebisho ya katiba kwa hati ya dharura, na kuuchomekea ubatili huo ndani ya katiba yetu!.

Hapa unashangaa nini?. Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?

Nimeuliza Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?

Hata TLS walipotoa kauli yao, nikauliza Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?
P
 
Tusimlaumu Johari.
Tumlaumu mlinzi mkuu wa rasilomali zetu.
Ikulu imejaa wataalam wa sheria hii imekusudiwa watu wajimilikishe, wamepewa majumba huko nje na wamepewa share kwa DPW ndio maana wameweka gundi masikioni
 
Mpwayungu Village taaluma yako ya ualimu inahitajika kwenye suala hili la Bandari. Tuliza Fujo, weka mazingira ya kama vile unasimamia kituo cha kupiga kura
 
Hata mwenye akili ya kutosha kuvuka barabara tu hawezi kukosa kuelewa mhitasari huu uliouweka hapa vizuri kabisa.
 
Nimekwama hapo-si lawyer by professional.....kosa la usemi wa lugha...paswa iwe si lawyer by profession....lakini pia hoja ingeeleweka kwenye representation mahakamani ndipo ushauri huu uzingatiwe...mambo ya ushauri na tafsiri za Sheria yeyote mwenye llb ambaye hajawahi kupitia TLS anafanya...Sasa johari alihusikaje na Bandari
 
Weka hapa huo ushahidi wako, umewekewa link hapo juu huyo unayemtetea yumo?
 
TAAA inachohitajika Mkurugenzi sio lazima awe mwanasheria mnatuchanganya. Hamza wa TAAA alihusika vipi mkataba wa ikulu na DP World
 
Mnaotumia maneno professional, profession njooni comment hii ipo sahihi Kwa matumizi sahihi
 
Huyu jamaa watu "walimpamba" kama WAKILI MSOMI, kumbe siyo. Hatari sana.
 
Usichanganye au kupotosha maksudi mazima.

'Ratfication' ya IGA kati ya mataifa mawili bado haijakamilishwa.

Bunge liondoe uchafu lililofanya na IGA itakuwa hakuna.
 
Hayati JPM alimkubali sana namna anavyofanya kazi, alikuwa ni mtu wake wa karibu kwa sababu JPM alikuwa mpenda haki na mzalendo wa kweli wa Tanzania.
Ungeyasema haya kuhusu Samia, ambaye alikuwa ni Makamu wa Rais, ningekushangaa; lakini naona umeepana kuangukia kwingine.

Sasa ninakuunganisha na huyo Hamza, pengine itakuwa ni wewe mwenyewe, au uko karibu sana na huyo mtu.
 
Nchi zinazotuzunguka kama Kenya, Uganda, Malawi na Msumbiji hazina haki ya kusimama na Tanzania kwa aina ya utajiri tuliojaliwa na Mungu. Lakini bado tunalo tatizo la weak manpower. Tuna uongozi mwingi dhaifu.
Kati ya yote uliyoandika; hili hapa ninakubaliana nawe kabisa. "Tuna uongozi mwingi dhaifu", tukianzia juu kabisa kwa Samia mwenyewe.

Hayo ya "majungu" na kutulinganisha na nchi jirani ni kelele tu zisizokuwa na maana yoyote.
 
Huwezi kuwa mkurugenzi mkuu wa TCAA yaani anga zima la Tanzania liwe chini yako halafu usiwe professional kwenye kazi yako!. Mikataba mingi ameingia kwa niaba ya serikali huu wa bandari ni maarufu kwa sababu ya unyeti wake.
Duh!
Sikujua kuwa ulikuwa thismuch shallow!
God have mercy upon us.

This is it! Kumbe huna kitu kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…