Ni hatua gani za kuchukua iwapo hakuna maelewano kwenye ndoa?

Bado kitambo kidogo, yote haya yatakwisha.
Kuachana sio suluhisho, bali kujishusha kwako na kuomba msamaha ili hali hujakosea .
Yaweza kuwa jambo jema zaidi na lenye manufaa zaidi kwa pande zote.

Dunia hii kila mtu analo Jaribu lake.
 
Una uhakika hiyo ni ndoa!? Maana kuna watu mmnasogezana tu!!
 
Kuna kipindi cha mpito ambacho ndoa zote hupitia na vijana wengi wa sasa hawawezi kukivuka salama kipindi hicho. Ndoa huwa zinakufa.

Ndoa tamu ni mwaka mmoja mpaka mitatu baada ya hapo huwa ni vurugu. Na inaweza kuwachukua hata miaka 5 mingine au zaidi kukaa sawa na kuchukuliana madhaifu yenu.

Humu utashauriwa mengi akili za kuambiwa changanya na zako ila hakuna ndoa ambayo haijapitia hicho kipindi cha mpito na hakiishi mwezi mmoja ni miaka inapita kunakuwa na tumvutano twa hapa na pale
 
Jipeni break kaeni mbali mbali kwa muda hata miezi mitatu. Au kama vipi achaneni tu maana hakuna kitu hapo
 
Jipeni break kaeni mbali mbali kwa muda hata miezi mitatu. Au kama vipi achaneni tu maana hakuna kitu hapo
Kujipa muda na kujaribu kukaa mbali ndio point ya msingi. Kuna wanandoa wengi wa kizazi hiki walipeana talaka na kugawana mali lakini baadae waligundua kuwa bado wanahitajiana.
 
Kujipa muda na kujaribu kukaa mbali ndio point ya msingi. Kuna wanandoa wengi wa kizazi hiki walipeana talaka na kugawana mali lakini baadae waligundua kuwa bado wanahitajiana.
Na mkiwa mbali ni rahisi kuongea, na kama mnapendana mtasolve tu
 
Usijipe mwoyo kwamba eti vumilia ni kipindi cha mapito, wala sio Mtu mzima habadiliki kirahisi hiyo ndo itakua hali yenu ya ndoa mda wote, isipo kua kipindi cha high na low season kulingana na mazingira yenu, "kama unataka kudumu kwenye ndoa yako ni lazima uwe tayari kuivuja hiyo ndoa yako mda wowote"...........maisha ndo haya haya kwanini upoteze mda wako ambalo alikufundishwa utaratibu kwao
 
Na mkiwa mbali ni rahisi kuongea, na kama mnapendana mtasolve tu
Ni kweli kabisa. Na watu wanaachana wakiwa wanapendana. Ikitokea wakaanzisha mahusiano mengine wanarudi kuwa wapasha viporo wakuu
 
Kuna wakati ndoa inakosaga mwelekeo, tulia tu.

Katika nyakati za furaha, timiza yote kwa usahihi.

Usiogope, ni kipindi tu. Kitapita.
 
Ugomvi wenu wa ndani msiusambaze nje na kuwaambia watu wengine,watu wa nje sana sana atakwambia "Usikubali mume akufanyie hivyo,nawe mfanyie hivi" hapo mnajikuta mnashindana kufanyiana viburi na kila mmoja akilenga kupata ushindi dhidi ya mwenzake kumbe ndio mnazidi kujiingiza kwenye matatizo,

Matatizo yenu yamalizeni wenyewe mpaka pale mtakaposhindwa ndio myapeleke kwa wazazi na sio kwa marafiki au watu wengine,

Maisha ya ndoa haimaanishi ni maisha ya kustarehe kila siku na kua na amani kila siku,matatizo ni sehemu ya maisha ila issue ni kua mnasolve vp matatizo yenu? pia msiingize matatizo yenu kwa watoto yatawaathiri sana kwenye maisha yao hata kwenye masomo yao.

Pole sana and Good luck.
 
Daaah hizi mambo zinakataga stimu aseee [emoji1][emoji1][emoji1] hata kama kila mtu ana mapito yake !!! Mimi naona mkifikia hatua ya kutojali na roho ya msamaha bora mtengane

Ndoa yangu ina miezi sita tuko vizuri sana !! Najifariji kidogo maana nimemuoa rafiki yangu[emoji1][emoji1][emoji1] siku gari likiwaka moto sijui itakuaje ?
 
Uzinzi,uchepukaji,kutojiheshimu,usaliti,kujiona,ujivuni ndio chanzo kikubwa cha migogoro.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…