Ni heri kubariki ndoa kuliko kufunga harusi

Ni heri kubariki ndoa kuliko kufunga harusi

Saint_Mwakyoma

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
865
Reaction score
1,208
Nimechukua miaka miwili kuchunguza hili Jambo, kwanini ndoa za siku hizi hazidumu na zimesongwa na milima mingi na mabonde kuliko tambarare. Kila mara watu wanatumia nguvu nyingi kuendesha mahusiano yaliyokufa ndani ya nafsi japo Yana heshima kubwa mbele ya macho ya watu.

Baada ya uchunguzi nimegundua ndoa nyingi zinazofungwa makanisani na misikitini zilitakiwa zibarikiwe tu na sio kufungwa Kama ndoa takatifu maana ndoa hizo zilishafungwa tayari na wapendanao.

Athari za kufunga ndoa iliyotakiwa kubarikiwa

1) Ulinzi, baraka na ahadi za Mungu juu ya ndoa hupotea na kamwe hautakuepo mpaka mtubu dhambi ya uzinzi juu yenu.

2) Kufa kwa ndoa husika maana mshahara wa dhambi ni mauti na Mungu kamwe hadhihakiwi.

HITIMISHO
Usiende mbele za Mungu kuoa au kuolewa na mpenzi ulieshiriki nae tendo la ndoa kabla ya ndoa Bali mbariki hiyo ndoa kwa kuomba toba ya msamaha ili Mungu afanye Jambo jipya ya kale yatapita na tazama yatakuwa mapya.
 
Umesema bora kufanya nini kuliko kufanya nini eti..???👊🏿👊🏿👊🏿
Kubaliki ndoa kuliko kwenda kumkana Na mumdanganya Mungu mbele ya madhabau takatifu ......kuapa uongo mbele za Mungu ni kitu hatari Cha kuogopwa na kutisha magumu wanayopitia waliofanya hivyo kamwe usikae kuwashauri laana zinavyo watafuna
 
Kuna mzee mmoja aliwahi kuniambia kamwe usioe mwanamke ambae tayari umeshazini nae, akadai ukioa mwanamke uliyezini nae basi ndoa yenu haitakua na amani ya kudumu, kila mara mtakua ni watu wa kukwaruzana tu.

Inawezekana maneno ya mzee yule yakawa na kaukweli fulani.
 
Mungu hadhihakiwi mkuu na hataniwi mnafunguana vishikizo na Kuweka agano la damu Bila kumshirikisha Mungu alafu mkiulizwa na watumishi wa Mungu mnamkana Mungu kwamba hamjawahi Sasa iyo ndoa Mungu aje kuiokoa akati mshakana 😂😂😂
Kwaiyo ninyi kanisan kwenu mkitaka kufunga ndoa mnaulizwa kama mlishawai kubanduana?
 
Kwani kubariki na kufunga ndoa kuna tofauti gani vile? Na ni kwa mujibu upi tunatengeneza hizi definition?
KUFUNGA NDOA ni kwa wachumba ambao bado hawaja shiriki tendo la ndoa ( hata Kama kila mmoja alikua na watoto sehemu nyingine ila walipatikana Bila ndoa takatifu)
Kubariki ndoa ni kwa wachumba walioshiriki teali tendo la ndoa hata Kama hawana watoto au wanao watoto.
 
Back
Top Bottom