Naelewa concept yako Ndugu Mtakatifu.Lakini naona kuna mchanganyiko katika maelezo yako.
Tukio la kubariki ndoa, si Toba. Bali ni tukio la kutaka kuishi katika utaratibu sahihi wa Mungu kati ya mke na mume.
Toba ni tukio la kujutia ile dhambi yako,kuikiri na kuiacha, na katika mada hii, dhambi ni uzinzi.
Unaweza kubariki ndoa, lakini ukawa hujatubu dhambi yako ya uzinzi wala hujajutia, na hiyo dhambi ikawa na wewe ndani ya hiyo ndoa.
Ushauri ni kwamba, kabla ya kubariki ndoa,kwanza tubu dhambi yako na kuiacha huku ukiwa unaendelea na mchakato wa kubariki.
Neno KUBARIKI ndoa ni kuita baraka za Mungu ambazo hazikuwepo wakati mmeshaanza kuishi tu bila utaratibu wake Mungu.
Hivyo KUBARIKI ndoa SI TOBA japo unaweza fikia TOBA wakati unaelekea mchakato wa Kubariki ndoa.Ili ile laana ya uzinzi itoke na uanze kuridhiwa kutembea na baraka za Mungu.