Ni heri kubariki ndoa kuliko kufunga harusi

Ni heri kubariki ndoa kuliko kufunga harusi

...una maana gani...
Ukibariki ndoa cheti mnachopewa ni tofauti na cheti wanchopewa maharusi..?

Ndoa ni ndoa tu haijalishi mlifanya tafrija kubwa au ndogo kiasi gani
Mkuu hatuongelei vyeti vya ndoa ..tunaongelea jinsi ya utaratibu ndoa hufungwa kwa wapenzi ambao bado hawajakutana kimwili na kubariki ni kwaajili ya wazinzi kutubu na kuapa kutorudia Tena utovu wa nidhamu kwa Mungu
 
Ukitaka uishi na mwanamke wako mda mref

1.mzalishe
2.ishi nae kama mke na mume
3.ila usimuoe

Aisee mtaish kwa amani sanaaaa... My observation

Sent using Jamii Forums mobile app
3. Weka mbariki ndoa ....Mungu huwa anathamini Sana mwana mpotevu anarudi kwake baada ya kugundua kakosea na kuona yeye anaumuhimu
 
Haya mambo yako kiimani zaidi, na si kila mtu ana hizo imani.

Wengine hufunga za kimila/kiserikali na huwa na amani zaidi kuliko hao wanafunga "NDOA TAKATIFU"
 
Haya mambo yako kiimani zaidi, na si kila mtu ana hizo imani.

Wengine hufunga za kimila/kiserikali na huwa na amani zaidi kuliko hao wanafunga "NDOA TAKATIFU
Ila kiimani huo ndio ukweli mchungu , Ndoa nyingi Mungu hazitambui kabisa na Hana mpango nazo ndio maana shida na majanga hayawaishi
 
Ni sawa lakini wanasahau kwamba kujamiana kumebeba utu wa mtu ...ndio maana waswahili wakasema kuingiliana kimwili Yani mnakua mwili mmoja na tunda linalopatikana hapo ni watoto ambao wamechanganyika kwa vinasaba vyenu
Narudia kujamiana ni tendo la heshima Sana maana ni Mungu mwenyewe alisema tuzaliane tuijaze dunia

Kuoa na kufunga ndoa ni kitu kimoja ambapo wapenzi ambao bado hawajakutana kimwili wanatakasa miili yao kwajili ya maisha ya mume na mke
Kubariki ndoa ni kwajili ya kuwapa nafasi wazinzi kutubu na kujutia makosa yao na kutakasa miili yao kwa maisha ya ndoa
Namkumbuka aliyewahi kuwa Askofu wa Mwanza, Mayala (R.I.P) alikuwa anapenda kusema mara kwa mara kuwa, hakuna kitu kinachoitwa "KUBARIKI NDOA", kwa wapenzi waliokuwa wanaishi pamoja, bila kujali wameishi miaka mingapi, kama hao wenza walikuwa hawakufunga ndoa!
Ndoa, ni kile kitendo cha UHALALISHAJI, kupitia kanisani, Bomani huko, Msikitini au, pale ma-sheikh wanapotufuata nyumbani kufungisha ndoa.
Na huwa tunasika,…… .wale watu wameishi muda mrefu, bila ndoa….!
 
KUFUNGA NDOA ni kwa wachumba ambao bado hawaja shiriki tendo la ndoa ( hata Kama kila mmoja alikua na watoto sehemu nyingine ila walipatikana Bila ndoa takatifu)
Kubariki ndoa ni kwa wachumba walioshiriki teali tendo la ndoa hata Kama hawana watoto au wanao watoto.
Oooooh ahsante kwa somo.
 
Ila kiimani huo ndio ukweli mchungu , Ndoa nyingi Mungu hazitambui kabisa na Hana mpango nazo ndio maana shida na majanga hayawaishi
Swali ni je walioishi kama mke na mme kabla.hiz dini kuja wao Mungu anawachukuliaje?

Kwenda kanisan kufunga ndoa ni kitendo cha kuhararisha tu mahusiano yenu kikanisa na mbele za watu na sio kwa Mungu, Mungu yeye anahesabu ndoa yenu toka ile siku ya kwanza mlipokubari kuweka agano la kuishi kama kitu kimoja mioyoni mwenu iwe ni kwa maneno au kwa damu.
 
@saintmwakyoma kubariki ndoa n ktabu gan ktka biblia
Kubariki ndoa ni kitendo Cha kutubu na kujutia dhambi ya uzinzi na kumsihi Mungu wape neema na rehema ......biblia inasema aungamaye dhambi zake na kuziacha huyo atamuona Mungu
 
Back
Top Bottom