Ni ipi ni njia nzuri ya kumdhibiti mtoto mtundu?

Ni ipi ni njia nzuri ya kumdhibiti mtoto mtundu?

Jinsia yako kwanza...!!nsije kutoa ushauri kumbe wew ni jiran tu
 
mtoto mlee kwa fimbo kiasi mpe makuzi sahihi mwanao usione ugumu kumuazibu pamoja na kumkemea pindi uonapo anakosea
,Mtoto muhalibufu wa vitu anatakiwa azibitiwe na akemewe asichekewe hata kidogo lazima aishi ajue hivi vitu vinasamani si vya mchezo mchezo hata kama nikidogo lazima ajue vinatafutwa kwa jasho hata kama kuna uwezo mkubwa wa kifedha ila mpe mtoto nidhamu ya vitu mkuu kuwa mkali kwenye vitu mkuu..
ahsante ndugu, nitafanyia kazi ushauri wako
 
Habari wana JF,,

Mwanangu ana miaka 5 lakini ni mtundu kupita kiasi, daily anaharibu vitu ndani, anapiga wenzake, ashameza msumari akanusurika, alimtia harage puani mdogo wake mpaka akatolewa hospitali, hua nina mchapa kiasi lakini sioni akipunguza utundu.

Laiti kungekua na selo za watoto nadhani ningempeleka kwanza akatulie huko, please mwenye kujua njia nzuri ya kumkabili mtoto wa aina hii anijuze maana nahisi kuchanganyikiwa.

Watoto rafiki zao wa kwanza ni baba na mama.

Hivyo iwe wewe au mama ni lazima mjenge urafiki na watoto hadi wakuzoee na wasiwaze ujinga mwingine.

Wasaidieni kusoma, kufanya shughuli za ndani na kucheza nao pamoja pale wanapohitaji kucheza.

Wapeni motisha kila mwisho wa wiki ni outing ya wote au mmoja wenu anatoka nao.

Wasikilizeni watoto na huyo mkubwa mfundishe baadhi ya vitu asiviharibu yaani kama ni kuiwasha TV, kuchezea radio na vifaa vingine ambavyo si vya jikoni umfundishe ili asije kuharibu.

Watoto ukiwa rafiki yao watakueleza kila kitu bila uoga na watakuonyesha upendo wa ajabu.

Ila ukijenga uadui na watoto kwa kuwachapa tu kwa hata kosa dogo na la kawaida basi, wanakuondoa akilini kidogokidogo.

Mwisho watajiunga na makundi ya kihuni, kufeli shule na mwisho kuja kuwa malofa.

Ni kama vile nyoka waweza kumfuga hadi akue na kurefuka na kuja kukupita urefu.

Vile unapomchezea nyoka huyo kwa kujaribu kukuviringa mwilini ndio nyoka yule anakutazama tu akikulia "timing".

Siku ya siku ikifika umesahau kumlisha na ana njaa kali basi ataamua kukumeza mzimamzima.
 
laiti kama viboko vingesaidia sidhani kama ningekuja hapa kutaka ushauri, kama unaushauri wa ziada please nisaidie ndugu
Mkuu hujasema mtoto ana miaka mingapi
Tungejua kwamba umechelewa kumnyoosha ama lah.
Lakini basi inaelekea ulimdekeza sana
Kiasi kwamba haogopi labda yaani awaze nikifanya hivi baba atakuja kunchapa
Hawazi! Anajua sracks him few stick then mumalizane basi wahi kabla hujachelewa
Zaman mtoto alikuwa ni wajamii

Kwamba Mimi nikimkuta mtoto wa mama juma anacheza barabaran namkemea ikiwezekana na bakora anapata

Ila nowadays hali imekuwa tofaut yaani gusa mtoto wa MTU uone
Hii imechangia kuwafanya watoto waone wazazi wao pekee ndo wanatakiwa kuwanyoosha.
Mlete hata mjomba au bamkubwa akae hapo hata mwezi
 
Okay ni hivi
Kil mzazi ana majukum yake kwenye malezi

Mama humfunza mtoto majukum ya ndan...usafi...!!na kazi mbali mbali

Dingi kazi yako ni kusimamia displini ndan ya nyumba...!!haitakiw akuogope....ila akikuangalia tu ajue kosa lake automatically(yan bila hata kumpiga kama ukiwa serious na malezi ya mwanao)

Pale mtoto anapoanza kutembea tu ulezi wako unaanziaga hapo...!!ndo kipindi cha kumkunja samaki...!!kumfunga paka kengele...!!

Ila kama umfikia hatua hakusikii jua umekosea mahali...!!makosa ni hapo kufanya ujinga wew ukiwepo....haaaapo
me, haya karibu kwa ushauri
 
Cha pili pia kama una mpango wa kuongeza mtoto mwingine epuka majina ya kurithi....majina mema au majina ya kwenye bible /quraan

Nitaftie kokote pale ulipoona watu wenye majina ya neema...furaha...bahati...amani...upendo wenye kujielewa...(ukipata ni 1 katika 30)

Mfano hai:
Kuna mzee alifariki...na akazaliwa mtoto kwa kaka yake..(wakampa jina la marehem)

Yaan tabia zote za marehem kazichukua...mtundu...mbiiishi...mkorofi...hasikiii

Uzazi sio kuzaa tu
me, haya karibu kwa ushauri
 
Cha pili pia kama una mpango wa kuongeza mtoto mwingine epuka majina ya kurithi....majina mema au majina ya kwenye bible /quraan

Nitaftie kokote pale ulipoona watu wenye majina ya neema...furaha...bahati...amani...upendo wenye kujielewa...(ukipata ni 1 katika 30)

Mfano hai:
Kuna mzee alifariki...na akazaliwa mtoto kwa kaka yake..(wakampa jina la marehem)

Yaan tabia zote za marehem kazichukua...mtundu...mbiiishi...mkorofi...hasikiii

Uzazi sio kuzaa tu
ahsante sana ndugu
 
wangu sio wa dawa, ye karithi kwa babu yake japo yeye anaonekana kazidi
Vyakurithi always huwa vinapitiliza mkuu, wala usihofu baada ya miaka kadhaa atakuwa mpole sana na utashangaa, huwa wanatumika kama demo(wa kutolea mfano) badae.
 
Parenting 101

Huyo ni mwanao chief. Kwanza mfahamiane.. inaonekana unastruggle hata kumuelewa kijana wetu.. take time mjifunze na umuelewe. Utundu wa mtoto unachimbuko jema tu.. yupo curious na wakati mwingine si kitu anaweza kukicontrol ni kazi yako kama mzazi kusaidia.

Ili muanze safari ya kusaidiana, inabidi umuelewe na umsaidie kukuelewa wewe pia. Hawa sio watoto ni watu wadogo na inexperienced... Bottom line ni watu.. tujitahidi kuwatreat kama watu. Since he is curious ..jitahidi kumsaidia kuchannel huo uwezo kwenye vitu productive.

Chonde chonde usimyime mapigo.. ila lazima kuwe na uelewa kwann anaadhibiwa.. wengine tunachapana kwa makubaliano na ikitokea amekosa kama baba lazima nimchape kama tulivyokubaliana na yeye lazima aelewe kwann amechapwa. Usimchape tu hivyo haisaidii..



Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom