Ni ipi sababu ya Rais Samia kuwa karibu sana na kuipa uzito Nchi ya Oman?

Huyo mfalme alikuwa anafanya kazi gani km si kutawala?
Huko Zanzibar alitawala kinanguruwe?
Nilitegemea professional comments from you. Sasa kwa comments kama hizi si kupoteza muda tu kubishana na wewe? Kwahiyo kila penye utawala kuna koloni? SSH ni kiongozi pale juu kwahiyo Tz ni koloni la nani?
 
Omani ndiye aliyekuwa mtawala wa Zanzibar, kuna wazazibari kibao walikimbilia Oman wakati wa mapinduzi.
 
Mkuu, haya ya mtu mweusi kuoa binti wa kiarabu ni ya leo. Historia toka zama na zama inaonyesha mabinti wa kiafrica (weusi) ndio waliokuwa wakizalishwa na wanaume wa kiarabu.
Siwezi kueleza kwa nini ilikuwa hivyo. Pengine ilikuwa ni utamaduni tu, kama ilivyo hadi sasa kumkuta binti wa kihindi ameolewa na mswahili. Na hata kumwona kijana wa kihindi kamwoa binti wa kiswahili, nalo ni jambo lisilozoeleka sana.

Unaposema Oman ina uchumi sawa na nchi hizo za Ulaya, sielewi unataka kueleza kitu gani hasa! Kwamba maendeleo ya Oman ni sawa na ya nchi za Ulaya? Hata hili kwangu sioni maana yake hasa ni nini!
 
wacha tu tupelekwe kama mbuzi sababu watz ni mamburura na tutachezewa sana mpaka tutawafufua waliotangulia mbele za haki.
 
Saud Aramco na Marekeni yumo maana yake ni Saud Arabia and American. Saud arabia wako vizuri
Saudi Aramco ni private Company ni juzi tu ndio imekuwa listed na mpaka sasa asilimia 98.5 inamilikiwa na serikali ya Saudia haina Chochote kinachoifanya iwe kampuni ya Kimarekani.

Na si Saudia tu, Nchi almost zote za Gulf zipo Vizuri, Uae, Qatar, Oman, Bahrain, Kuwait etc wana mpunga wa kutosha.
 

Wanawake wa Ki oman walikuja pwani Ya Africa? Kihistoria wa Oman walikuja Kupambana na Mreno wanajeshi, kushirikiana na Local wakawatoa, ni Jambo la kawaida kwa mwanajeshi kuja kama yeye, na si jambo la kushangaza akapata mwanamke huku.

Hayo mambo ya maendeleo nimeyaleta kuonesha mentality za Wa oman wenyewe, kwa Generation tofauti wameruhusu mtu mwenye damu nyeusi awaongoze, hawajambagua kama Nyie wala kusema ni mweusi basi asiongoze nchi yetu ya kiarabu, wanapendana bila kuangalia rangi ya ngozi zao na mpaka leo nchi yao ipo juu kimaendeleo.

Then angalia mentality hio reflect na wewe, ama Nchi hii kiujumla.
 
80% not true kabisa. Kuna nchi kibao Africa they have also oil reserves but wameshindwa kusimamia vizuri na wananchi wake ni masikini especially Angola n k . View attachment 2153610
Kuna Gabon hapo yule mbuzi Omari Bongo aliunga bomba la mafuta kuwapa France ye akapewa Villa huko Paris na mke huku watu wake wanakufa njaa.
Umemsikia Mfaransa analalamikia mafuta?
Bomba hilo mpk leo jamaa anapiga tu huko

Yule mbuzi alikabidhiwa na bibi wa kifaransa kabisa apigwe vizuri.
Kapigwa na anapigwa tena hata mwanae alipokua rais wa kupewa na babaake jamaa wanapiga tu naye akavuta kwa Stress.
Wananchi hawaelewi mkataba gani huu hauishi.
Ndio hiyo mikataba ya miaka 99 mnayokabidhi.
 
kwani historia inasemaje?? hao waarabu wa Oman si ndio walikuwa wanamiliki watumwa Zanzibar na kuwalimisha mashamba?? Ni ndugu yako gani ambae anakugeuza mtumwa na kukuuza arabuni akiwa kakuhasi? Japo Muingereza nae alikuwa na mabaya yake lakini bora alivyokomesha utumwa vinginevyo mpaka 1964 wengi wangekuwa manamba huko visiwani.

Historia ipo tusijifanye hatuijui, hizo ngozi nyeupe hatuna undugu nao walikuja kimaslahi tu.
 
Kumbukumbu iliyopo ni kuwahasi watumwa na kuwauza utumwani huko arabuni na kuwafanyisha kazi bila malipo hapo visiwani, hakika ni kumbukumbu nzuri sana ya undigu wetu wa damu baina ya waoman na watangayika walioletwa visiwani kutoka bara kuja kulimishwa karafuu
 
Fitna mkubwa wewe ,akheri ya mchawi.
 
EeeeenHeeeee, what a spin. Hiyo aya ya kwanza, wa Oman walikuja kuwakomboa waafrika kutoka kwenye ukoloni wa Mreno?
Huyo "mtawala mweusi" alitokea wapi?
Sasa walipokwishamwondoa mkoloni, na wao kuwa wakoloni wapya, hawakuleta wanawake wao, kama ma'settler' wengine wanvyofanya maeneo mengine, kama Afrika Kusini?

Hilo la mentality ya kutokuwa wabaguzi siwezi kulisemea. Pengine Wa-Oman, siyo waarabu basi? Historia ya hao watu siijui, na kusema kweli Oman ni nchi ambayo siijui kabisa, hata kwenye ramani ukiniwekea mbele niitambue siwezi. Na usidhani kwamba sina elimu ya jiografia ya kutosha, ni tu kwamba 'impact' ya Oman katika maisha yangu haipo kabisa.

Wanazalisha sana hasa kitu gani, mafuta au gesi? Kuna kitu chochote cha kiwandani wanachotengeneza na wanasifika sana duniani kwa kitu hicho?
 
Swali la kijinga, inaonesha elimu yako ni hafifu.
 
Waarabu ndio mabwana zenu. Huna history unayoijua wewe kenge.
Chuki na roho mbaya ndio utamaduni wenu machogo.
 
Kwanini iwe ni kila muomani alihusika na biashara ya utumwa?!!!

Kwani ni kila mmarekani alihusika kuwachukua watumwa Afrika ya magharibi?!!!

Kwani ni kila muingereza alihusika na ukoloni kwa nchi za afrika?!!!

Huko Omani hakukuwa na wananchi wa kawaida wasiohusika na hiyo biashara?!!!

Kama sivyo ,je unawahukumuje waomani wote na biashara hiyo?!!!

Ikiwa utumwa ungalipo huko Oman basi biashara hiyo haijakoma ulimwenguni kote kwani nchi za ulaya ya mashariki na magharibi nao wanaongoza kwa "HUMAN TRAFFICKING...."

N.B Hata waafrika tulichukuana utumwa....isome historia vyema

#Siempre JMT🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…