Ni jambo gani, sasa unaliamini tofauti kabisa na vile ulivyokuwa ukiliamini kabla hujawa mtu mzima?

Ni jambo gani, sasa unaliamini tofauti kabisa na vile ulivyokuwa ukiliamini kabla hujawa mtu mzima?

NACKO

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2022
Posts
1,298
Reaction score
2,514
Wakuu natumaini mu wazima wa afya,....

Katika maisha, binadamu tumekuwa watu wa kujifunza mambo mbali mbali kila siku, hali inayopelekea WATU kubadili mitazamo na baadhi ya imani pale inapobidi,...

Kwangu mimi , nilipokuwa mtoto, nilikuwa nikiwaona WATU WAZIMA wakiongea PEKE YAO njiani, basi niliwashangaa sana na pengine kuwaona kama watu waliochanganyikiwa, lakini kwasasa MTAZAMO wangu huo umebadilika kabisa, badala yake NAJIULIZA, ni nini SIRI YA WATU WAZIMA AMBAO HAWAONGEI NJIANI PEKE YAO PAMOJA NA MAGUMU YOTE HAYA TUNAYOPITIA?

Leo katika pita pita zangu mtaani nikielekea kazini, kama unavyojua tena wengine hatuna weekend wala likizo,...nikamuona mtu mmoja kwa mbali akija uelekeo wangu, alikuwa mwanaume wa kama miaka 40's alikuwa smart kiasi, LAKINI ,alikuwa akiongea peke yake, basi ikabidi nimpishe tu kwa TAHADHARI, maana wakina sisi wengine hadi NGUMI na hata MATEKE huwa tunarusha..😂😂

#maisha🙌🙌
 
Ata ya kula inakosa kabisa
niliwahi ambiwa na bro wangu wa kitaa kuwa hakuwahi kushiba kwa mda wa wiki tatu za mwanzo alipoenda kutafuta maisha ARUSHA,kipindi hicho mi niko school , nilicheka sana na sikuamini,..alooooh!..nilipoingia kitaa kuanza kutafuta maisha, yalinikuta, na Yaliyonikuta ni zaidi ya WIKI TATU ,...sitaki nikumbuke😥😥😥
 
Ila kama ungekuwa wa kike ungepata fursa..
Yapi yalikukuta..

Pole mkuu
 
Back
Top Bottom