Ni kama vile Vunjabei anaelekea kufilisika

Kweli mkuu. Kutulia na jambo moja kwanza ni muhimu. Jambo likiwa kubwa automatically litazaa jingine.
 
Hili kosa nililifanya sana wakati ndo nachipukia. Nilikuja kuacha baada ya kujikuta sina kitu na madeni kibao. Kwa sasa nimekuwa mgumu mno kuanzisha kitu kipya. Nikianzisha ni baada ya kufanya utafiti hata zaidi ya mwaka.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Unasema ngoja nianzishe mishe nyingine ili kukuza kipato kumbe unaenda kuzama daah.
 
Nimekusoma hapo chief.. all the best

Aahhhh mkuu acha kabisaa, biashara hiz ni hectic ndugu yangu unafikir watu wanapenda bas kufokea watu?? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.
Inatokea tu πŸ˜†
Nina jamaa mmoja nilikaa nae kiundugu ila hatuna mawazo sawa. Nilikuwa nampa nauli na hela ya kula nje na hela yake nikaona ananipumzikia. Nikakaa kikauzu akili zake zichangamke.

Sasa mtu kaoa na mimi sijaoa, ana watoto mimi sina, anajenga, anasomesha, ana mademu chungu nzima, ana jimama. Hata hela sijui anazitoa wapi ila nazidi kufirisikaπŸ˜‚

Ajiraportla ninachoipendea naweza soma zaidi.
 
Mkuu kwa mfanyabiashara kuishiwa kawaida sana huyo alianza kupotea muda kipindi kile aliposhindwa kuwaletea Simba Jezi zao kwa wakati ni bora hata yeye kanusa Utajiri misingi ya kuipata tena anayo na fursa pia..
Alikuwa anatamba sn mitandaoni kwamba mwanaume lazima uhonge ,,

Kiko wpi sasa?
Hana excuse yeyote ya kujitetea.
 
Alikuwa anatamba sn mitandaoni kwamba mwanaume lazima uhonge ,,

Kiko wpi sasa?
Hana excuse yeyote ya kujitetea.
Tofautisha kufirisika na kuishiwa.
Anaweza akawa amefirisika lakin hajaishiwa. Na hawez kuishiwa afike level yako wewe au mimi
 
Punje chache
 
Mkuu hakuna tofauti yeyote ya kuishiwa na kufliisika.,

Kwa kifupi ni kwamba hana pesa,
,tuache maneno ya kujifariji
Mimi sina ukaribubna yeye natumia tu logic ya kawaida kwamba kwa mfanya biasharabkama yeye si rahis sana kufika hatua ya kuishiwa kiwango hicho unachifikiri wewe.. ila probably wewe unaweza ukawa unamjua in person so nisikubishie pia
 
Umeshaambiwa duka zima lina suruali 6 na soksi 4

Sasa si kama kafunga?πŸ˜‚πŸ˜‚
Hiyo miezi miwili iliyopita wakati nimeenda dukani kwa vunjabei hali haikuwa hivyo. Labda kafirisika ndani ya huo muda siwezi jua
 
Uwezo wa watanzania kwenye fikra ni mdogo sana mimi sijaona kosa la mleta uzi kama naadhi ya watu wanavyomshambulia
 
Na ukianza kujihusisha na waganga tu umeshajichanganya....waganga ni waongo tu wataanza kukupa maagizo ya kipuuzi puuzi tu Hadi ufilisike.
Bora waganga kuliko hawa wachungaji na manabii. Kuna wakati nilipoteza mwelekeo mzima wa maisha nikaona bora niende kuombeawa. Mchungaji wa kwanza alinipokea vizuri siku ya kwanza na kuniombea ila wakati naaga akaniambia nirudi wiki inayofuata na bahasha ya sadaka angalau 20k. Nikaona fresh tu. Mara ya pili alizingua alivyoniambia nitoe mchango wa vifaa vya muziki vya kwaya. Kimoyomoyo nikajiuliza huyu K mbona anaanza ishu za kiwaki? Yaani mimi hata kula ya tabu nitoe mchango wa vyombo vya kwaya? Sikurudi tena. Nikaona niende kwa GeorDavie mwenyewe. Nafika Kisongo kumbe kuna utaratibu wa kishenzi kuliko nilivyodhani. Ilikuwa ni kulipa Tsh 500 kuombewa na wasaidizi wake. Mimi nililipa Tsh 500 nikaombewa na kina mama fulani ambao walionekana kama wamepigika kuliko hata mimi. Geordavie mwenyewe ilikuwa lazima ulipe noti ndefu sana kuweza kuombewa nae. Uamuzi wa mwisho ilikuwa kwenda kwa mganga. Kuna mganga mitaa ya kambi ya fisi akaniambia nisijali nitamlipa baada ya kazi ila nimletee vifaa vya kazi. Vifaa vingi vilikuwa complicated nikaona bora tupige hesabu nimpe mganga hela akanunue. Kwa hesabu ya haraka ilikuwa zaidi ya laki na sikuwa hata na 10k. Nilikaa chini na kuamua sitaki mambo ya wachungaji wala waganga. Baada kama miaka mitatu nilirudi tena kwenye mstari hadi leo. Wachungaji ninawaheshimu ila najua hawana msaada wowote kwa maskini zaidi ya kuwavuna kidogo walicho nacho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…