Ni kama vile Vunjabei anaelekea kufilisika

Ni kama vile Vunjabei anaelekea kufilisika

Nilikuwa Mbeya huko nikapita mitaa ile ya SIDO ni kama vile duka la Vunjabei linapumulia mashine, halina mzunguko wa biashara kivile.

Jana nimepita Iringa napo naona lile duka alilolifungua kwa mbwembwe nalo lishajifia na kufungwa muda tu.
Hapo Dar duka lake la Sinza nalo linapumulia mashine.

Ni kama vile jamaa kaanza kufilisika mdogo mdogo.

Nimeambatanisha picha za duka lake la Iringa lililofungwa.

View attachment 3088613
Kwahiyo wewe kazi Yako ni kuzunguka mikoa tofauti kuangalia maduka ya Vunjabei tu?

Kama wewe ni kijana basi nakuhakikishia ukifikisha miaka 50 utakuwa umehitmu kuwa mwanga na mbaya zaidi utakuwa unawachawia mpaka ndugu zako.
 
Yani hakuna kitu rahis..nami nilipitia business downfall ila kwa kukosa maarifa na uchanga na uoga nikafeli nikajikutabzero nikajikuta disputes na wateja ambao pesa zao zilipotea kwenye michakato ya biashara..weee nitakuja kusimalia hapa
Pole kwa mapito hayo. Inabidi tuanzishe Uzi maalum wa wafanyabiashara ili tushare Mambo mbalimbali Kama changamoto, mafanikio na mapito tunayopitia.
Biashara Kama unaroho nyepesi hutoboi aisee
 
Vijana wa mbeya waliuziwa jordan retro kwa 15k baada ya kuivaa kwenda nazo club 3times zinang'oka soli marekani akiskia kuna mtu jordani anauziwa dollar 10 atakua anacheka tu
e12fa9b8072a4b1cad5f24dae96f0b4a~2.jpg
 
Biashara ya pharmacy inaonekana Ina faida sana alafu Haina stress sana..maana madawa hayana fashion
 
Hata la sinza pale wateja wamepungua vibaya mno. Wataalam wanasema jamaa kapigwa "Juju" hasa na mmoja ya mademu alietoka nae akamuacha
Kwamba hilo juju ndo limefanya sisi wateja tuache kwenda, mbona hai make sense

Na kama hilo juju linafanya kazi hapo anayekua amerogwa ni vunjabei au sisi wateja
 
Mwenzake Frank knows mwanzoni alikua na maduka

K.koo mtaa wa kongo
Sinza
Arusha
Dodoma
Mwanza

Ila sahv amemua kufunga maduka ya Mwanza na k.koo mtaa wa kongo, amebaki na maduka matatu tuu,

Nafkir jamaa yeye hataki show off anaangalia na biashara inaendaje, akiona hailipi au gharama za uendeshaji ni kubwa anapiga chini
 
Mwenzake Frank knows mwanzoni alikua na maduka

K.koo mtaa wa kongo
Sinza
Arusha
Dodoma
Mwanza

Ila sahv amemua kufunga maduka ya Mwanza na k.koo mtaa wa kongo, amebaki na maduka matatu tuu,

Nafkir jamaa yeye hataki show off anaangalia na biashara inaendaje, akiona hailipi au gharama za uendeshaji ni kubwa anapiga chini
Mwanza, mbeya , arusha hakuna wateja may be uwe mzawa ila mgeni unabid uweke mipambano mikali
 
Ukiona biashara imeshamiri na kuwa katika peak aka kilele basi fahamu kifuatacho ni anguko so kwa wajasiri wa mali wa kweli huwa wanafanya kitu kinaitwa daivesifikesheni...
Yaani wafungua biashara nyingine isiyoahabiliana na hiyo iliyo kwa peak..

Wajifunze kwa huyu mzee, mzee wa Azam Marine... Huyu mjamaa kufilisha labda serikali ihusike ila huku ana ferry huku unga huku maji pipi king'amuzi sijui azam pesa yaani mambo lukuki.

Yaani kufilisika huyu shuruti serikali ihusike oops nimesahau na azamu sukari hahahaha!!
 
Back
Top Bottom