Kuna rafiki yangu Fulani tulisoma pamoja O level kitambo alifiwa na mke wake, taarifa nilizipata kwa wakati nikaenda msibani kuzika, yule mwamba alikuwa analia kama mtoto kiasi kwamba nilimsalimia tu na kumuacha hakuwa normal.
Tulivyotoka makaburini kwa sababu kuna watu nawajuwa wa mitaa ile ndio nikafanya udadisi ndio nikapewa mkanda mzima kwamba mwanamke ndio alikuwa kila kitu, amembeba sana mshkaji na mtaani watu wakiwa na shida ya pesa huwa wanakopa kwa huyo Shemeji yangu marehemu, na nikaambiwa Jana jamaa alipelekwa hospitali akawekwa mapumziko na dripu juu, sukari na pleasure vilipanda.
Kwahiyo nakubaliana na hoja yako ukiwa marioo msiba lazima utakusumbuwa kupitia kiasi.
Kuna mwamba mwingine huyo ni wa mtaani kwangu kabisa mke wake alipofariki wote tulijuwa ni lazima amefurahia kifo hicho, maana gwaride alilokuwa anapelekeshwa na mwanamke siyo la dunia hii, halafu mke anajuwa kabisa jamaa ana financial harassment lakini mwanamke haelewi ni gubu hatari.