Ni kheri ufiwe na mzazi kuliko kufiwa na mume/mke

Utakuwa na matatizo sana
Huwezi hata siku moja ukalinganisha wazazi na mke au mume

Inawezekana imekuuma sana lakini kauli ya wazazi FUTA

Kuna jamaa yangu alifiwa na mke wake na kumuachia watoto 4.
Alioa baada ya miezi 3 tu ili kuwasaidia watoto wasiumie zaidi kwa kumkosa mama yao

Kuishi na baba tu ni ngumu sana Kama baba mwenyewe anaenda kutafuta riziki
Bahati nzuri alipata mke ambae alikuwa anawaangalia watoto kwa huruma ya hali ya juu

Acha kuwatesa wanao kisa umeshindwa kuendelea na maisha mengine

Kifo ni wajib ila hatujaambiwa tuomboleze milele
Unajiumiza mpaka utashindwa hata kufanya kazi sasa wanao nani anawahudumia au uko nchi ambayo mnasaidiwa kila kitu?
 
Najua unachopitia lakini msemo na mtazamo wako sio sahihi..umeonyesha ubinfsi zaidi.

Mama yako ni mke wa babako
Baba yako ni mume wa mama yako

Hicho unachopitia nao wangepitia vivyo hivyo.
Mwisho nikutakie uponyaji ndani yako
 
Sawa atapata mke mwingine, je hao watoto watatu wtapata mbadala wa mama yao mzazi? Tujaribu kufikiria pande zote, imagine watoto wadogo ambao bado wanahitaji malezi ya mama yao halafu wamempoteza

Niseme tu kila mmoja kwenye maisha yetu ana nafasi yake, wazazi wana nafasi, wenza wana nafasi na hata ndugu wana nafasi lakini hakuna jambo gumu kama mzazi kufariki ingali watoto bado wadogo na hawajaweza kujitegemea
 

Ngumu sana sana sana na Pole, ila Nguvu ya kuyashinda haya yapo mikononi mwako na siyo saikologist, move on, she is in a better life, dont talk about it.
 
Mzee anakuwa kama benki yako ya siri zako anakufichia siri zako. Pia mzee ni mshauri wako mkuu akiondoka mzee nusu ya moyo nao umeondoka.

Maneno ya mumeo alie filiwa na mkewe:- mke wangu kwaheri lakini msiba wako umeleta kheri nimepata demu mpya nikiwa nakulilia sasa nimepata mfariji mpya.🤣
 
Pole sana Mungu akusaidie uweze kumove on umesema una watoto hamisha nguvu zako kwa watoto ni ngumu lakini itakusaidia
 
Una umri gani Mkuu?
 
Hapo mama yao amefariki hakuna la kufanya
Ila mume inabidi awasaidie watoto kwa kuoa ili mke awalee hao watoto
Yamemkuta ila nae lazima awahurumie watoto zaidi waliofiwa na mama yao
 
You have nailed ,yaani Leo hii nilinganishe kifo cha kufiwa Mke au mume kiwe bora kuliko wazazi wangu,mtoto wangu au kaka ma Dada zangu !?

Mke ndio ana nafasi yake lakini sio kwa kukinganisha ni ndugu zangu wa damu,watoto au wazazi wangu.

Huyo mwamba kazingua ile mbaya
 
Wewe ni mwanamke ila umeongea ukweli. Umewasagia kunguni wanawake wenzio... hakika kwa hali hii Team Kataa Ndoa wanakwenda kushika. Mpaka dk hii ubao unasoma Team Kataa Ndoa 4 na Team Kubali Ndoa hawajafanikiwa kupata chochote.[emoji38]
 
Mchumba wangu alipata miscarriage, aliumia sana. Ajabu akaniambia ni bora angenipoteza mimi! I was perplexed! Since then I learned mke siyo ndugu yako. They're too selfish.
Ulichelewa sana kujua. Na huyo hakupendi anataka hela zako, siyo ajabu hiyo mimba haikuwa yako. Vitu vizuri vyote wanataka kuvibinafsisha kuwa vyao. Dawa ni kuishi nao kikatili tu hakuna namna.
 
Wewe ni mwanaume legelege,umelelewa na soap opera za kifilipino na telenovelas
 
Pole sana mkuu.

Baba yangu alifariki nikiwa Nina miezi kadhaa ..mama yangu hajawahi kuolewa Tena nikawa mtoto wa mwisho kwake.

Huwa tu ananiambia, "Mwanangu heri nife Mimi ila sio mumeo".

Aiseee basi Huwa naogopa sana.

Ukiacha hilo niliwahi kushuhudia mama yangu mdogo akiwekwa ICU siku nne baada ya mumewe kufariki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…