Ni kheri ufiwe na mzazi kuliko kufiwa na mume/mke

Umeandika vema mno, mtoa mada asome andiko lako mara mbili then ajitafakari.

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Halafu hii kauli ya mke kumkimbia Mme huwa siipendi kuisikia masikioni mwangu, mbona wanawake wengi tu wanatunza waume zao? Na wapo wanaume wengi wanakimbia wake zao? Tena wengine wanakimbia hadi watoto ? Ndugu wa Mme sijui huwa na roho gani nikama huchukua roho ya shetani
 
Pole sana
 
Inategemea mahusiano yenu mlivyokuwa mnaishi, kwako inaonekana mlikuwa vizuri, kuna wengine mke/mme akiondoka ni furaha tele, unaweza usiamini lakini imetokea sana tuu
Wanamsakama tu mtu unayelala naye una amka naye akikutoka ni ngumu sana kukabili kuna ndugu yangu mwaka 7 huu hajaoa na nyumba haikuwa nyumba haeleweki kabisa, lakini alifiwa na Baba yake akaomboleza maisha yakaendela baada ya miaka 6 mkewe mmm mpaka leo anashauriwa aoe lakini bado anwewesekaga tu, huyo nikumtia moyo sio kumtonesha.
 
Hawatakuelewa
 
Wake zetu hawana uchungu na wanaume zao hilo linajulikana , tena wengine hadi wanafanikisha vifo vya waume zao kwa namna moja au nyingine.
Wanaume wanapenda kwa dhati ,wanawake wanapenda kwa nafasi . Ndo maana majumba yetu yanajaa ndugu wa mke tu.
Sio mzima wewe, utakuwa na matatizo na mwanamke wako
 
Huwa namshangaa sana mtu asiyekubali toka moyoni kwake kwamba kuna kifo na ni hatma ya kila mmoja wetu, na endapo kifo kitamchukua mtu wako wa karibu haina maana ndio mwisho wa maisha...
Wewe umefiwa na nani wa karibu ukakubali mapema ?
 
Pole sana kwa kufiwa na mke ila umekosea sana kuwalinganisha wazazi na mke. Kumbuka mke waweza kumreplace lakini mzazi ni mmoja tu (Baba/Mama) ukimpoteza hutakuwa na mbadala.

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
Mke unaweza kumreplace kama ulivyosema lakini si kwa wepesi, huyu mkuu nimemwelewa, mnaweza kuwa mmezaliwa wengi mkaliwazana, ila kwa mwenza unabaki mwenyewe, pole yake tu huyo ndugu, Mungu ampe faraja yake maana ya binadamu nikama mawe haya wanayo mdondoshea.
 
Shida si kukubali, inategemea bna personal attachment na huyo aliyeondoka., Mchango wake kwako watoto na kadhalika, kuna wenza uwepo wao nibzaidi ya nyota kwako, mnafanya mambo mengi ya maendeleo naye mnalala naye na pengine ni msiri wako wa ndani, huyu akiondoka duniani si rahisi kukubali .
Mzazi kama mzazi , ni rahisi sana ku move on maana kifo kinajulikana .mzazi hulali naye na wala hawezi kukufanyia ya mkeo .

Nb kama hamkufanya chochote cha maendeleo na mkeo , halafu akafariki , ni tofauti . Mtoa mada anaposema hata akiingia chumbani kuwa anasikia harufu ya mkewe maana yake kuwa walifanikiwa kujenga , angekuwa amepanga hilo lisingetokea , maana angehama tu nyumba.
 
Kwa ambao hawajaoa hawataweza kukuelewa watakudhihaki tu hapa ila mimi nimekuelewa ni jangwani unapita kaka soon utafika caanan.. mke/mume akifariki ni mzigo mzito maumivu yake si mchezo kabisa.
Hata mi nimemuelewa sana na ni katika vitu vinasononesha sana .
Wazazi tunawapenda na kuwathamini, lakini for the sake of life huwa tunawaacha na kwenda kuanzisha maisha yetu mapya na wenza wetu , . Hiyo ni hatua ya kwanza ya kujiondoa kwao. , Ukiingia kwenye ndoa tayari kunakuwa na maamuzi ya kindoa na wazazi by default wanakuwa wako mbali na kinachoamuliwa au kufanyika kwenye ndoa.
Typical men huwa wanaondoka nyumbani kwa namna moja au nyingine wakiwa na miaka 13 hadi 18, na ndo muda mahusiano ya kindoa yanapoanza .
 
You are right......Mke ni mali sana ila usiombee kufiwa na wazazi pia.
 
Pole sana mkuu ila kufiwa na Mke ni sawa tu kufiwa na wazazi....inauma mno😑
 
Pole sana ndugu, Mungu aendelee kukufariji ambaye hajawahi kupitia hali hii anaweza asikuelewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…