Kodi hii tayari ilishahamishiwa kwenye bidhaa na tunailipa, hata Umeme ukininua kuna Vat ndani yake, hata ukinunua bia unalipa kodi, hii kodi ya kichwa ilishahamishiwa kwenye bidhaa, huyu mtu kachanganyikiwa, ni mtoro wa mirembe, hakuna kuoneana aibu katika hili
Wazazi walinihadithia kwamba hapo zamani, wazazi wao wa kiume(babu zangu) walikuwa wanatabia ya kukimbia na kujificha maporini pale ambapo walikuwa hawajalipa kodi ya kichwa, maana familia ilikuwa ni kubwa, na hapakuwa na pesa ya ziada ya kwenda kulipa kodi ya kichwa, hivyo kuna kipindi iliwabidi kuwaacha na mama zao ili wao waende kufanya vibarua sehemu mbalimbali na as soon as wanapopata pesa ya kulipa kodi ya kichwa ndio walirudi majambani mwao.
Kwa wale ambao hawakulipa na hawakutoroka mafichoni, walikamtwa na maaskari wa mkoloni na kwenda kulimishwa kwenye mashamba ya chai, pamba na kadhalika hadi pale deni litakapoisha. Mkoloni alitumia reli kusafirisha pamba , chai , katani nk. hadi kwenye bandari na kuzisafirisha kwa meli hadi Uingereza na kuwapa utajiri wa kufuru.
Hiyo ni miaka ya ya kabla na baada ya ukoloni , 1950’s kuendelea. Sasa fastfoward hadi kipindi cha Mkapa, uamuzi ukafanyika kwamba kodi ya kichwa ihamishiwe kwenye bidhaa (Vat na kadhalika), ambapo kwa hivi sasa, hata mtoto mdogo akinunua soda tu (japo hana TIN number) tayari analipa kodi na inakwenda serikalini. Hivyo kwa mantiki hiyo, hakuna MTanzania ambae halipi kodi, hata kama hana TIN number, bado analipa kodi kupitia bidhaa anazonunua.
Sasa jamani, leo hii mtu anatoroka milembe kimagendo magendo tu, kwa njia anazojua yeye, bila ruhusa ya daktari ili kudhibitisha kama akili zake zipo sawa, anakuja huku uraiani leo hii 2022 anasema waTanzania wasio na TIN hawalipi kodi, tena hao hao ambao kila siku wanakatwa pesa za miamala, yeye anasema halipi kodi, hivyo wote wapewe TIN number ili waanze kulipa kodi.
Kwahiyo tumerudi miaka ile ya 1950’s ambapo kwa sasa njia inayotumika ni kutupa mikopo ‘HEWA’ , mfano mkopo wa chanjo wa Trillion 2 na vifaa tiba vya kupima chanjo, mkopo ni hewa maana hata ugonjwa ni hewa, hata Barakoa Rais havai tena, malengo yametimia, na ili kulipa mkopo huo ndio wanarudisha kodi ya kichwa kwa style hii, na mwisho wa siku trillion 10 kila mwaka inayokusanywa, ni ya kulipa madeni na riba juu, yaani badala ya kupeleka pamba, chai na katani, tunapeleka pesa kama watumwa, mariba matupu!!!
Hii nchi amani itakuja kutoweka, THERE IS A LIMIT, hata kondoo ana uvumilivu wake!!!
"Kila mtanzania mwenye umri wa zaidi ya miaka 18 na mwenye kipato anatakiwa kulipa kodi. Ili kutimiza amza hiyo, Serikali inakusudia kutoa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 au zaidi" "Kwa kuwa utaratibu wa usajili wa namba ya utambulisho...
Hii mikopo tunayobugia kwa pupa hivi tutakuja kuilipa kupitia puani. Tanzania yakopa Tsh trilioni 2.4 kutoka IMF Muda wa kulipa ukifika, tunaweza hata kuambiwa tulipie hii hewa tunayovuta, maana ni rasilimali ya serikali na tulipe kama tunavyolipa kodi ya ardhi. Unapimwa uzito wako kisha...
Na mkoloni alitoza kodi ya kichwa kama tools ya kumfanya mwafrika afanye Kazi yaani kumjengea utamuduni wa kupenda Kazi, mkoloni hakutegemea kodi kuendesha nchi, bali raslimali zilizopo.
CCM wamekosa ubunifu, soon tutasherekea jubilei ya miaka 100 ya UHURU tungali na matatizo yaleyale tangu UHURU
CCM inatakiwa itoke madarakani hiyo ndiyo suluhu. Hata marekani kuna vyama viwili vinapokezana kuna Republic na Democratic. Kwa mbongo yeye anaona hakuna chama kingine zaidi ya CCM.
Tena wawekee na kodi ya laini yaani kila mtanzania awe analipa buku kila mwezi mwenye laini.
Kidumu chama cha mapinduzi
Ndiyo matokeo ya kuwa na wabunge wengi wa chama kimoja. Wabunge wenyewe wameingia kwa magumashi wanaweza kupinga kweli?
Waweke na kodi ya laini yaani kila mtanzania alipe buku kwa mwezi
Unalipishwa kodi na mitozo ya kila aina, halafu hela wanaenda kununulia magari ya kifahari ma V8 VXR, kulipana posho nene, na kuishi kwenye majumba yao ya kifahari!
Ifikie wakati wananchi tuukate huu ukoloni wa ccm.
Wazazi walinihadithia kwamba hapo zamani, wazazi wao wa kiume(babu zangu) walikuwa wanatabia ya kukimbia na kujificha maporini pale ambapo walikuwa hawajalipa kodi ya kichwa, maana familia ilikuwa ni kubwa, na hapakuwa na pesa ya ziada ya kwenda kulipa kodi ya kichwa, hivyo kuna kipindi iliwabidi kuwaacha na mama zao ili wao waende kufanya vibarua sehemu mbalimbali na as soon as wanapopata pesa ya kulipa kodi ya kichwa ndio walirudi majambani mwao.
Kwa wale ambao hawakulipa na hawakutoroka mafichoni, walikamtwa na maaskari wa mkoloni na kwenda kulimishwa kwenye mashamba ya chai, pamba na kadhalika hadi pale deni litakapoisha. Mkoloni alitumia reli kusafirisha pamba , chai , katani nk. hadi kwenye bandari na kuzisafirisha kwa meli hadi Uingereza na kuwapa utajiri wa kufuru.
Hiyo ni miaka ya ya kabla na baada ya ukoloni , 1950’s kuendelea. Sasa fastfoward hadi kipindi cha Mkapa, uamuzi ukafanyika kwamba kodi ya kichwa ihamishiwe kwenye bidhaa (Vat na kadhalika), ambapo kwa hivi sasa, hata mtoto mdogo akinunua soda tu (japo hana TIN number) tayari analipa kodi na inakwenda serikalini. Hivyo kwa mantiki hiyo, hakuna MTanzania ambae halipi kodi, hata kama hana TIN number, bado analipa kodi kupitia bidhaa anazonunua.
Sasa jamani, leo hii mtu anatoroka milembe kimagendo magendo tu, kwa njia anazojua yeye, bila ruhusa ya daktari ili kudhibitisha kama akili zake zipo sawa, anakuja huku uraiani leo hii 2022 anasema waTanzania wasio na TIN hawalipi kodi, tena hao hao ambao kila siku wanakatwa pesa za miamala, yeye anasema halipi kodi, hivyo wote wapewe TIN number ili waanze kulipa kodi.
Kwahiyo tumerudi miaka ile ya 1950’s ambapo kwa sasa njia inayotumika ni kutupa mikopo ‘HEWA’ , mfano mkopo wa chanjo wa Trillion 2 na vifaa tiba vya kupima chanjo, mkopo ni hewa maana hata ugonjwa ni hewa, hata Barakoa Rais havai tena, malengo yametimia, na ili kulipa mkopo huo ndio wanarudisha kodi ya kichwa kwa style hii, na mwisho wa siku trillion 10 kila mwaka inayokusanywa, ni ya kulipa madeni na riba juu, yaani badala ya kupeleka pamba, chai na katani, tunapeleka pesa kama watumwa, mariba matupu!!!
Hii nchi amani itakuja kutoweka, THERE IS A LIMIT, hata kondoo ana uvumilivu wake!!!
"Kila mtanzania mwenye umri wa zaidi ya miaka 18 na mwenye kipato anatakiwa kulipa kodi. Ili kutimiza amza hiyo, Serikali inakusudia kutoa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 au zaidi" "Kwa kuwa utaratibu wa usajili wa namba ya utambulisho...
Hii mikopo tunayobugia kwa pupa hivi tutakuja kuilipa kupitia puani. Tanzania yakopa Tsh trilioni 2.4 kutoka IMF Muda wa kulipa ukifika, tunaweza hata kuambiwa tulipie hii hewa tunayovuta, maana ni rasilimali ya serikali na tulipe kama tunavyolipa kodi ya ardhi. Unapimwa uzito wako kisha...
Umeandika vizuri kuhusu kodi ya kichwa. Je unadhani kodi inayolipwa ukinunua soda, ni kodi pekee unayopaswa kulipwa?
Je, una namna gani ya ku-tap informal economy?
Tulinganishe na kodi ya kichwa, kwa hiyo unadhani mwenye miaka 18 wataanza kukimbia kama ilivyokuwa kwa wazee kipindi cha mkoloni kabla kodi haijaendelea?
One fact, Kodi ya kichwa ilikuwa inafahamika kuwa ni kiasi kadhaa, hii imesema tu usajili, Je unadhani itakuja kustate kuwa kila mwenye TIN alipe kiasi kadhaa?
Watz tulio over 18 hatufiki hata milion 30..hata tukitoa buku buku kila mtu bado ni hela ndogo sana watakayokusanya kuliko athari zake kisiasa..wabane matumizi tu. trilion 40 ni mzigo mrefu sana.
Mwisho wa siku trillion 10 kila mwaka itakayokusanywa itakwenda kulipa madeni na riba juu, yaani badala ya kupeleka pamba, chai na katani ulaya tunapeleka pesa kama watumwa!.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.