Ni kigezo kipi kimetumika kurudisha kodi ya kichwa wakati tayari ilihamishiwa kwenye bidhaa?

Ni kigezo kipi kimetumika kurudisha kodi ya kichwa wakati tayari ilihamishiwa kwenye bidhaa?

Kwanini asizalishe chochote, anaishije….. nafikiri ni vema kuhamasisha watu wazalishe na si kuendekeza uzembe.
Hayo ya kuhamasisha na sijui kwa nini hafanyi kazi ni mada nyingine kabisa!!

Nambari ya mlipa kodi ni kwa ajili ya mlipa kodi baasi!
Kama inarudishwa kodi ya kichwa waseme wasione aibu!
 
Unapotosha au hujui unachokiandika! TIN Ni registration nyingine Kama Ile ya NIDA, Kodi hulipwa na Kila mtu mwenye kipato halali, hivyo unaweza ukawa na tax identification number(TIN)Lakini huna kipato aujira hufungwi kulipa Kodi, huna kazi,biashara au shughuri yoyote Kodi itakukuta wapi? Unafahamu principles and cannon of taxation?
 
Hii kodi Mwl Nyerere aliifuta, akaja Mwinyi akairidisha baadae tena akaifuta. Naona Samia kairudisha.

Ni kodi ya kishenzi, mtu asiezalisha chochote hatozwi kodi, anasaidiwa jamani!
Kodi ya kichwa/maendeleo ilikuwepo mpaka 2000 hapo,lipumba akapiga kelele zikatolewa..Kodi ya tin siyo kichwa,na imesemwa wazi kwa wenye kipato,huwezi kuwa na kipato bila kuwa na shughuli
 
Kwa hiyo huko kwa wauza bidhaa hakuna TIN sio?

Una kichwa kikubwa ila kimejaa uji wa mhogo 😆😆😆😆
Nani kasema wauza bidhaa hawana TIN? Hai ni wafanyabisahara na ni mawakala wa kukusanya kodi ya serikali hivyo lazima wana TIN. Hoja ni kwamba hata asiye na TIN bado analipa kodi kupitia hao mawakala (wafanyabiashara) na hivyo si sahihi kusema kwamba wasio na TIN hawalipi kodi hivyo wapewe TIN ili walipe kodi as if sasa hawalipi kodi, wakati ukweli ni kwamba kodi hii ya kichwa ilikwisha ondolewa na kuwekwa kwenye bidhaa, ukinunua bidhaa, hata kama huna TIN basi moja kwa moja unakuwa umelipa kodi.
 
Nani kasema wauza bidhaa hawana TIN? Hai ni wafanyabisahara na ni mawakala wa kukusanya kodi ya serikali hivyo lazima wana TIN. Hoja ni kwamba hata asiye na TIN bado analipa kodi kupitia hao mawakala (wafanyabiashara) na hivyo si sahihi kusema kwamba wasio na TIN hawalipi kodi hivyo wapewe TIN ili walipe kodi as if sasa hawalipi kodi, wakati ukweli ni kwamba kodi hii ya kichwa ilikwisha ondolewa na kuwekwa kwenye bidhaa, ukinunua bidhaa, hata kama huna TIN basi moja kwa moja unakuwa umelipa kodi.
TIN ni lazima kwa kila mwananchi aliyetimiza miaka 18 and above,porojo zingine utazijua wewe..

Sisi watumishi tulikata TIN toka 2019 na ni bure
 
Nimesoma heading pekee nikaja kucomment, kama mtoa mada kaeleza mbadala mseme ili nirudi kusoma uzi wote, kama kaishia kulalama, fanya kupotezea tu.
Mbadala ulishapatikana, walifuta kodi ya kichwa wakaihamishia kwenye bidhaa, unataka mbadala gani, tukakuuze kwenye danguro? Huo ndio mbadala unaotaka wewe?
 
TIN ni lazima kwa kila mwananchi aliyetimiza miaka 18 and above,porojo zingine utazijua wewe..

Sisi watumishi tulikata TIN toka 2019 na ni bure
Kuwa na TIN ni kitu kimoja, ila kuitumia hiyo TIN ili kulipisha raia kodi ya kichwa ambayo tayari ilishahamishiwa kwenye bidhaa ni kitu kingine na ndio inatufanya tuombe serikali ifunge CCTV camera kule Mirembe ili kudhibiti utoro
 
Binafsi ninaamini mpaka kufa kwangu , CCM ndiyo chanzo cha umaskini wa Watanzania . Miaka 50 madarakani halafu tunaburuzwa hivi halafu familia zao ziko safe hatari . Siku moja nitamfunga paka kengele
 
Hao wabeinge walishindwa kuhoji haya mambo au ndo ile ya kupigia makofi na kusema ndiyooo ipiteeee?
Wabunge hutajirika kwa kupitishiwa migao kwenye bahasha za khaki ili kupitisha uozo..
 
CCM inatakiwa itoke madarakani hiyo ndiyo suluhu. Hata marekani kuna vyama viwili vinapokezana kuna Republic na Democratic. Kwa mbongo yeye anaona hakuna chama kingine zaidi ya CCM.
Tena wawekee na kodi ya laini yaani kila mtanzania awe analipa buku kila mwezi mwenye laini.
Kidumu chama cha mapinduzi
Mbona imewekwa hiyo ya kulipia line za ving’amuzi 3,000/= kila mwezi
 
Kuwa na TIN ni kitu kimoja, ila kuitumia hiyo TIN ili kulipisha raia kodi ya kichwa ambayo tayari ilishahamishiwa kwenye bidhaa ni kitu kingine na ndio inatufanya tuombe serikali ifunge CCTV camera kule Mirembe ili kudhibiti utoro
Kila mtu anaestahili akiwa nayo workforce itajulikana na tija yao.
 
Kwanini asizalishe chochote, anaishije….. nafikiri ni vema kuhamasisha watu wazalishe na si kuendekeza uzembe.
Hazalishi ananunuaje bidhaa na kulipia kodi kupitia bidhaa?, kama ana akiba yake kaachiwa urithi basi muache ainjoy maisha yake.
 
Waweke na tozo kwenye kila bao linalopigwa, wataalamu mkuje na njia ya kukusanya tozo za mabao,
wale mnao wahi kumwaga Kama majogoo mtajua wenyewe.
Hahahah, hii tozo ya mshindo itakuwa balaa sana, ukipiga bao tatu unatozwa kodi mara tatu 😂😂😂😂
 
Watanzania hatuna kauli haya kipi kifanyike au ni kulalama tu
 
Umeandika vizuri kuhusu kodi ya kichwa. Je unadhani kodi inayolipwa ukinunua soda, ni kodi pekee unayopaswa kulipwa?

Je, una namna gani ya ku-tap informal economy?

Tulinganishe na kodi ya kichwa, kwa hiyo unadhani mwenye miaka 18 wataanza kukimbia kama ilivyokuwa kwa wazee kipindi cha mkoloni kabla kodi haijaendelea?

One fact, Kodi ya kichwa ilikuwa inafahamika kuwa ni kiasi kadhaa, hii imesema tu usajili, Je unadhani itakuja kustate kuwa kila mwenye TIN alipe kiasi kadhaa?
Umesoma huo muswada? Hebu soma halafu uone kilichoandikwa, ni kwamba kila TIN inayosajiliwa itakadiriwa na utalipa kwa kupotia simu, hutaki unaweza hata kukatwa pesa unayotumiwa kwenye simu yako.., na kiwango kitaendana na miamala unayofanya, hii ni kodi ya kichwa kabisa, ambayo ilikwisha hamishiwa kwenye bidhaa. Suala la kuwa kodi pekee inayopaswa kulipwa inategemeana na shughuli zako, kama unalima korosho utakatwa kodi kwenye korosho zako, kama ni mfanyabiashara utalipa income tax nk, nk ,nk, kama unatuma pesa utakatwa tozo, kodi ziko nyingi tunalipa, ila tusirudishe kodi tukizohamishia kwingine, hivi leo wakirudisha Road license na kodi za majengo ambapo tayari unazilipa kupitia mafuta na LUKU utaona ni sawa?

Hivi huko Mirembe huwa mnatorokea geti lipi?!
 
Wazazi walinihadithia kwamba hapo zamani, wazazi wao wa kiume(babu zangu) walikuwa wanatabia ya kukimbia na kujificha maporini pale ambapo walikuwa hawajalipa kodi ya kichwa, maana familia ilikuwa ni kubwa, na hapakuwa na pesa ya ziada ya kwenda kulipa kodi ya kichwa, hivyo kuna kipindi iliwabidi kuwaacha na mama zao ili wao waende kufanya vibarua sehemu mbalimbali na as soon as wanapopata pesa ya kulipa kodi ya kichwa ndio walirudi majambani mwao.

Kwa wale ambao hawakulipa na hawakutoroka mafichoni, walikamtwa na maaskari wa mkoloni na kwenda kulimishwa kwenye mashamba ya chai, pamba na kadhalika hadi pale deni litakapoisha. Mkoloni alitumia reli kusafirisha pamba , chai , katani nk. hadi kwenye bandari na kuzisafirisha kwa meli hadi Uingereza na kuwapa utajiri wa kufuru.

Hiyo ni miaka ya ya kabla na baada ya ukoloni , 1950’s kuendelea. Sasa fastfoward hadi kipindi cha Mkapa, uamuzi ukafanyika kwamba kodi ya kichwa ihamishiwe kwenye bidhaa (Vat na kadhalika), ambapo kwa hivi sasa, hata mtoto mdogo akinunua soda tu (japo hana TIN number) tayari analipa kodi na inakwenda serikalini. Hivyo kwa mantiki hiyo, hakuna MTanzania ambae halipi kodi, hata kama hana TIN number, bado analipa kodi kupitia bidhaa anazonunua.

Sasa jamani, leo hii mtu anatoroka milembe kimagendo magendo tu, kwa njia anazojua yeye, bila ruhusa ya daktari ili kudhibitisha kama akili zake zipo sawa, anakuja huku uraiani leo hii 2022 anasema waTanzania wasio na TIN hawalipi kodi, tena hao hao ambao kila siku wanakatwa pesa za miamala, yeye anasema halipi kodi, hivyo wote wapewe TIN number ili waanze kulipa kodi.

Kwahiyo tumerudi miaka ile ya 1950’s ambapo kwa sasa njia inayotumika ni kutupa mikopo ‘HEWA’ , mfano mkopo wa chanjo wa Trillion 2 na vifaa tiba vya kupima chanjo, mkopo ni hewa maana hata ugonjwa ni hewa, hata Barakoa Rais havai tena, malengo yametimia, na ili kulipa mkopo huo ndio wanarudisha kodi ya kichwa kwa style hii, na mwisho wa siku trillion 10 kila mwaka inayokusanywa, ni ya kulipa madeni na riba juu, yaani badala ya kupeleka pamba, chai na katani, tunapeleka pesa kama watumwa, mariba matupu!!!

Hii nchi amani itakuja kutoweka, THERE IS A LIMIT, hata kondoo ana uvumilivu wake!!!

USHAURI: Ulinzi uongezwe Mirembe, pafungwe CCTV, wagonjwa wanatoroka hovyohovyo!


Naawaza mtu akikosa kulipa hiyo kodi ni watamfunga ama.
Kwanza wananchi tunatakiwa tushirikishwe kuhusu maamzi ya kitaifa.

2. Kodi zinaongezeka at the same time ndugu zetu wamasai wanatimuliwa ili kumuacha mwekezaji.

3. Tunatangaza kukopa kila kukicha utasikia mama amekopa trion amani billion kadhaa kutoka nchi fulani, is seriously tunafurahia kukopa kiasi hiki?. Ni seriously tunajenga miradi yote na kujenga uchumi wa nchi yetu kwa kukopa?. Ni lini tutaheshimika duniani?.


I wish I could be PRESIDENT
Machepele wa Tanzania
 
Watz tulio over 18 hatufiki hata milion 30..hata tukitoa buku buku kila mtu bado ni hela ndogo sana watakayokusanya kuliko athari zake kisiasa..wabane matumizi tu. trilion 40 ni mzigo mrefu sana.
Wewe kwa akili yako watachukua buku? Kwa mwaka unaweza ukalipa kodi ya kichwa hata milioni, inategemea na ukubwa wa kichwa chacko
 
Unapotosha au hujui unachokiandika! TIN Ni registration nyingine Kama Ile ya NIDA, Kodi hulipwa na Kila mtu mwenye kipato halali, hivyo unaweza ukawa na tax identification number(TIN)Lakini huna kipato aujira hufungwi kulipa Kodi, huna kazi,biashara au shughuri yoyote Kodi itakukuta wapi? Unafahamu principles and cannon of taxation?
Wewe umesoma hicho kilichoandikwa au unakuja kubwabwajantu kama ngedere? Kila aliye na miaka 18 na kuendelea atapewa TIN number kama hana, na atakadiriwa kiasi cha kodi atakocholipa kupitia simu yake kulingana na kiwango chake cha miamala..., hivyo kila mtu atalipa kodi ya kichwa! Kama ingekuwa suala ni Identification, basi NIDA ID is quite Sufficient for that purpose, isn’t it?!
 
Back
Top Bottom