Uko sawa kabisa mie nakumbuka nilipohitimu kidato cha sita nilibahatika kupata ajira Mgodini kampuni kubwa tu hapa Tanzania, niliingia kama mine trainees ( Mchimbaji mwanafunzi) nilikaa kwenye hiyo kazi mda tu huku najipanga kurudi shule siku moja nikaona tangazo la kazi humo ndani ya kampuni vigezo wanahitaji mtu aliyesomea Mine engineer, duh mie nikaona isiwe shida acha niombe tu wakiniita nitajaribu maana kigezo kingine uwe mzuri kwa hisabati na miraba kwawakati huo nilikua sijambo kweli kwenye hisabati na ukizingatia bado shule haijaisha kichwani kipindi hiko Mungu si abdallah kikaitwa kufanya usahili tukiwa watu Hamsini na nafasi taraji ni sita tu ajabu nilipambana nikawashinda mpaka waliokuwa na vigezo zaidi yangu kumbe mie ndio nilijibu maswali yote kwaufasaha zaidi, Unajua ukikuta usahili anafanyisha mtu kutoka nje ya nchi unaweza kufurahia sana hakuna longolongo kama Watanzania wenzetu, Hivyo kijana jiamini tu unapoona nafasi ya kazi na sifa angalau unaendana nazo jaribu mengine makaratasi tu wala yasije kukutisha.