Ni kisa au mkasa gani uliwahi kufanyiwa na ndugu au mtu wako wa karibu?

Ni kisa au mkasa gani uliwahi kufanyiwa na ndugu au mtu wako wa karibu?

Ndugu yangu wa mbali kaja mjini kakaa kwangu miezi 2. Cha ajabu alivyoondoka kaenda kunianika kijijini kuwa tunakula wali maharage Kila siku jioni....na Dagaa kabichi mchana na kwamba wife atakua mchoyo!
Wamekupa likes za bure lakini huyo ndugu yako ni mtu mzuri sana. Ni mkweli. Ulitaka aseme unakula kuku na ngombe kila siku wakati siyo kweli? Huoni angekuchongea kwa ndugu zako na wangetaka ''uwapunguzie'' raha zako? Au siku akija ndugu mwingine na akute unakula maharage na kabeji kila siku na huku huyu alisema vingine, angedhani umeamua kumkomoa?
 
kuna kazi ilitokea jeshini yaani mafunzo ya jeshi (jw) kipindi hicho mkuu wa kambi ana pewa nafasi za watu watatu kuwaingiza jeshini bure basi nafasi ikawa imedondokea kwangu,rafikiake na mkuu wa kambi ni ndugu yetu sa akawa amepeleka jina langu kule kwa mkuu kule lugaro, mzee sikuya mwisho ana ambiwa mwanao anatakiwa alipoti ila andaa jiwe3 za soda akagoma.usiku na kuja kusikia ana mueleza bi mdogo ,yaani aende jeshi siatatusumbua huyu iliniuma kinoma,nikapata rafiki baharia wa meli kikabila ni muhaya,ye anaishi uk anagereji akamwambia dingi nienda ymca pale posta nisome mechanico injiniaring chakusikitisha niliishia kupigwa nondo nashule sikumaliza, jamaa anataka atumeviza dingi akamwambia nimehuni shule basi ikaishia hivyo.nachoshukuru mungu hajaniacha bahati bado ipo kwangu. Na dingi baadae alifirisika amebaki hana jeuri.n.b wazazi wengine ni wabinafsi hata kwa watoto wao wakuwazaa,nawaza sasaiv ningekuwa zangu jw au uk. ila hapa hapa maisha yanajipa dingi jeuri hana loho mbaya ilimponza.
Looooh[emoji23]
 
Iv hizi issue za kutesana kwa kukaa aakwa ndg ziko kweli?
Nimekua ndg wanasomea kwetu(ndg wa upande wa mama) sikuwan ona shida yoyote wamepata
Sisi wenyewe tumesomea kwa ndg baba wadogo hapa dar hatujawah pappta shida yoyote
Now kwangu ndg wamepita kibao wengine kusoma na wengine wanakuja mjini kutafuta mishe ya kufanya sijawah ona shida sometime nakaaga na watu siwajui but amna shida
Najiuliza iv unamtesaje mtu? Kama hutak kukaa nae si umwondoe tu ? Na unapomtesa mtu iv kesho yako unaijua kweli?
Baba mdogo aliwah tuambiwa wakat huo tunakaa kwake vijana kama 7 iv wite tunasoma " ukipokea wagen ndani kwako hutakaa upungukiwe chakula kamwe" huu msemo haujawah toka kichwan na niwe mkweli sometime nakaaaga na watu kwangu na hali inakuwa haiko poa biashara haziend but hatujawah kupungukiwa chakula ndani kamwe.
Inategemea ntu na ntu,

Binafsi nimeishi na watu ndugu/sio ndugu fresh tu,

Na home tumeishi na watu hasa vijana na wana maisha yao sasa MashaaAllah,na mama ni kama mama yao sasa,

Unajua nini??? Chakula,chakula,chakula.shida inaanzia hapa.
 
Nilishushwa kazi na mtu niliyemsaidia apate kazi kwenye kampuni nilipo.

Akawa hanisalimii Wala kuongea na mimi, pia akawa ananicheka baada ya kurudi chini yaani kutoka kuangaliana na Computer hadi kushika Spana kama fundi, sikujali kushuka kwa mshahara na marupurupu.

Nililazimisha furaha machoni pa watu huku Kila mtu akinishangaa wengine waliniita chizi au nimerogwa sikujali, nilizungukia Equipments zote za kampuni huku yule jamaa akinifanya kunisifia kuwa Mimi ni fundi Bora kwa vifaa vyote vinafanya kazi kwa usahihi.suti na tai vilimpendeza akajiona kamaliza maisha

Lakini acha MUNGU aitwe MUNGU, nilipeleka CV zangu mahali, nikapokelewa freshi , huku nikiwaonesha Nini maana ya
Mechanical engineering, nikapewa na dereva juu maanina.
Duh pole nyie,watu km hao ndo wanasababisha tusipate connections
 
Wamekupa likes za bure lakini huyo ndugu yako ni mtu mzuri sana. Ni mkweli. Ulitaka aseme unakula kuku na ngombe kila siku wakati siyo kweli? Huoni angekuchongea kwa ndugu zako na wangetaka ''uwapunguzie'' raha zako? Au siku akija ndugu mwingine na akute unakula maharage na kabeji kila siku na huku huyu alisema vingine, angedhani umeamua kumkomoa?
Hahaha hajasema uwongo of course. Ila ni kama ananinanga fulani. Pia lile pilau la Kila jumapili ambalo sio la maharage hajalisema.
 
Nilishawahi kuajiriwa na muhindi mmoja kama project manager. Ali apply tender iliyohusisha kuweka signage (mabango) nchi nzima kutoka kampuni moja maarufu ya Makaburu (South Africans). Kipindi hicho ilikuwa project yenye thamani ya kama $100,000.

Kabla ya kupata tender kulikuwa na bidding ambapo moja ya sharti ilikuwa ni kuwakilisha installation plan (proposal) iliyohusisha uchambuzi wa matumizi ya budget, utekelazaji wa kazi mpaka kukamilika kwake.

Nilifanya kazi ya kuandaa plan wiki 2 nzima usiku na mchana maana ilikuwa inahitajika haraka. Ilipotimia na kuwakilishwa muhindi akashinda tender.

Ilipoidhinishwa tu kuwa kashinda jamaa akaniambia kuna muhindi mwenzie toka India (expatriate) atasimamia hiyo project (kutumia plan yangu), moja ya makubaliano yetu ya awali ilikuwa nitaisimamia mimi hiyo project yote endapo proposal yangu itapita.

Aliposema mambo ya expatriate tu nikatoa notice yangu ya mwezi mmoja ya kuacha kazi.

Kipindi nataarisha plan ya hiyo project nilifanya research ya kutosha nikijua nitasimamia mimi mwenyewe hivyo niliweza kuhalalisha baadhi ya matumizi ya budget nikijua nitafanikisha vipi baada ya research yangu.

Phase ya kwanza ya project ilianzia mikoa ya Tanga, Arusha na Moshi. Muhindi alipopewa mzigo installation ianze akachemka baada ya kumaliza Tanga tu. Pesa ilikata na kazi hata robo haijaisha.
Kila sehemu ilikuwa na time limit kama ilivyoanishwa kwenye proposal plan, muhindi alichemka phase ya kwanza tu huku ikiwa keshachukuwa advance ya Mkaburu.

Nilifanya presentation mimi mwenyewe kwenye bidding kwa niaba ya muhindi, hivyo sharti aliliopewa na makaburu ni kuwa aliendaa na kufanya presentation ya proposal ndio asimamie project la sivyo atanyang'anywa kazi.

Ilibidi muhindi anitafute tukae chini tena akiahidi offer kubwa kulinganisha na ya awali. Nilimkatalia na wakati huo huo nili apply kivyangu kwa makaburu wanipe project mimi kama mimi.

SIkuwa na kampuni yangu hivyo ile project ikahamishiwa kuwa in house project kumaanisha walianzisha kitengo maalum cha signage ndani ya kampuni yao kuanzia production mpaka installation na mimi nikapewa hicho kitengo kukisimamia. Hivyo badala ya Project Manager nikawa Division Manager.

Kwa ile phase ya kwanza ilimlazimu muhindi kumaliza na ilibidi areport kwangu moja kwa moja kwa niaba ya kaburu, karma is real.

Sehemu ya kazi iliyobaki iliisha kwa wakati na mpaka sasa kupitia hiyo project kitengo cha signage kwenye kampuni ya kaburu kimekuwa one of the leading signage companies kwa Tanzania.

Katika maisha chochote kinachopaswa kuwa chako kitakuwa chako tu haijalishi kitachelewa kwa kiasi gani.
Nimekosa double like...hongera sana champ
 
Mi nililogwa na mtu niliyekuwa namstahi na kumfadhili kwenye mambo mbalimbali ilikuwa kidogo nilale mavumbini ila Mungu mwema alinipigania na kunitoa kwenye kamba za Mauti.
Adui zetu hawatoki mbali
 
Ila Sijui wahindi wanashida gani,

Kuna skin Product na import kutoka India, week kadhaa zilizopita nikapata ujio wa muhindi ofisini kwangu, akidai namuharibia soko kwa kuingiza bidhaa aliyokua anaingiza yeye.

Hivyo nikimaliza mzigo ni lazima nichukue kwake la sivyo atanipeleka polisi.

Ajabu ni kwamba Bei anayoniuzia kwa 500pcs ni Bei nnayouza kwa mteja wa less than 6pcs

Sasa nimekataa ananifata anaomba tufanye Kazi pamoja..
Kwa kweli nimekataa kata kata.
Mpeleke yeye Polisi kwa kukutishia
 
Back
Top Bottom