Ni Kitendo cha Nadra sana kuwaona Askari wa Uingereza Special Air Service (SAS) na Navy Seals

Huyo SAS yupo kwa ajili ya kuwapa mafunzo Wakenya nao wana kikosi chao cha kujilinda na ugaidi...Na huyo jamaa anatembea kwenye Gari yake akiwa na vifaa alivyovaa wakati wote na alichonishangaza yeye havai element sijui kichwani ila siraha anayokua nayo ni kubwa sana na ana shabaha sana kila risasi inafika kwenye Target yake na amewaokoa wakenya wengi na ndie aliefanya magaidi kwenda kujificha gorofa ya saba maana alikua haogopi kitu anaingia chumba kwa chumba mwenyewe wakenya wakiwa mbali na kutoka nje kuangalia ramani ya jengo...jamaa yupo fit sana aisee..ameiva vizuri kwa kweli..
 
Kwahyo alikuwa akizurura na hzo silaha katika jiji la Nairobi kabla ya tukio? Au unataka uniaminishe kuwa baada ya tukio wanajeshi wa Kenya walimpa hzo silaha kisha akaungana nao kupambana na magaidi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzungu ni noma, acha kabisa. Fuatilia watu wa kazi walivyoingia Pakistani na kumuua Osama halafu wakaondoka na mwili wake.

Polisi wanaamka asubuhi wanakuta kila kitu kimeshamalizika. Walitua bila ya rada kuziona ndege zao, na ni bahati mbaya tu ndege yao ilipata ajali ndogo, vinginevyo Osama angeuliwa kutokea juu na sio kutokea chini.
 
Kwahyo alikuwa akizurura na hzo silaha katika jiji la Nairobi kabla ya tukio? Au unataka uniaminishe kuwa baada ya tukio wanajeshi wa Kenya walimpa hzo silaha kisha akaungana nao kupambana na magaidi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, huyo SAS yupo Kenya katika kuwapa mafunzo wanajeshi wazalendo, tukio lilipotokea hakujiuliza mara mbili, akavaa magwanda na kuingia kazini.
 
Nimeuliza kuhusu silaha nisome tena ukipendezwa nijibu

Sent using Jamii Forums mobile app
Unauliza silaha wakati yeye ni mwalimu wa mafunzo?. Anawapa vipi mafunzo wanajeshi pasipo yeye kuwa na zana zote mkononi!!.

Hiyo ni dharura mkuu, hao wanajeshi wazalendo wawe na silaha halafu yeye akose, angeweza hata kuazimwa na mmoja wao.
 
Aiseee uko Obsessed na JPM watu wanaongelea mambo ya Special Forces unaleta habari za vidole vipi huyo Kibosile naye alikuwa Special Forces au raia ? Ungeniambia alimtia vidole Navy Seal kidogo ningekuelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeuliza kuhusu silaha nisome tena ukipendezwa nijibu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mbona mgumu hivyo kuelewa.. umeambiwa alikua anatoa mafunzo kambini. Alipo sikia kunatukio la ugaidi aliunga akaja sehemu ya tukio. Swala la silaha kunamwanajeshi anatoka nchi yake Bila yakubeba silaha.? Mbaya zaid ametoka kambini kwa wanajeshi unafikiri atakosa silaha.? Au ww ulivyoelewa tukio limemkuta alikua chumbani au yupo around apo anapiga gambe.?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu SAS meber alikua nchini kenya kwa ajili ya kutoa mafunzo katika jeshi la kenya,
...Ninyi watu ninyi...!!! Kwa hiyo, shambulio la hivi majuzi ilikuwa 'practical' ya trainees wa jeshi la kenya?
====
Acheni masihara katika matukio ya hatari!
 
Walikuwa wanaendesha training kwa vikosi vya kenya,lilivyotokea hilo tukio wakaombwa,hakua mmoja tu bali walikuwepo wengine.
 
Ndugu GSU walikuwa wanajulikana tokea enzi za mzee Kenyatta , ni kikosi madhubuti na hidari sana Africa Mashariki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbwembwe hizi za kusifia zingekuwa na mantiki sana kama kusingekuwepo na ndugu zetu waliopoteza Maisha, vyenginevyo ni mapambio tu
 
Ila mleta mada punguza mahaba!! Eti SAS na SEAL ndiyo vikosi bora ulimwenguni!! Vikosi vya wengine unavijua?? Au series na propaganda za kimarekani zimekupa upofu???
Operesheni nyingi tu za SEAL zimeshindwa, tena huko Somalia, Yemeni ,Afghanistan n.k.
 
Ha ha ha!! Mkuu ati umesema yuko around anapiga gambe?

Ha ha!!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
ndg GSU bado wapo active mpaka leo sio wakati wa moi tu.

maandamano na vurugu zote wanazofanya wakenya, wanatumwa GSU kwenda kutuliza. hayo ndio majukumu yao makuu.
Hivyo unakubalina nami kuwa hawako undercover kama Detective J anavyotaka kuidanganya hadhara hii yaJF cariha please substantiate this!
 
Aiseee uko Obsessed na JPM watu wanaongelea mambo ya Special Forces unaleta habari za vidole vipi huyo Kibosile naye alikuwa Special Forces au raia ? Ungeniambia alimtia vidole Navy Seal kidogo ningekuelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekusoma mkuu, kumbe dhambi yangu ni kumtaja huyo mjomba pembeni ya Ngosha. Aisee sitarudia tena kutenda hili kosa.
 
Ule mpango ni ISI ndiyo walichomesha, wamekuja pale ISI wote wanajua. Wao ndiyo waliwatumia hao makomandoo bila ya wao kujijua baada ya kumaliza shida yao na anayetafutwa

Hivi unajua ISI ndiyo wanafanya wamarekani washindwe kumaliza vita kule Afghanistan. Angekuwa ni noma angeshinda mapigano
 
Mkuu kumbuka kuwa yule aliyekuwa akiishi na Osama aliweza kudukuliwa na CIA, mpaka wakamvuta kwenye satellite ikawa rahisi kujua anaishi nyumba gani. Baada ya hapo kazi ikawa imekwisha. Mzungu akiamua kukufungia kazi ni ngumu kuchomoka.

Unajua wametumia pesa kiasi gani tangu waanze kumuwinda Osama?.
 
Mkuu hapo umechanganya mambo GSU Kenya ni sawa sawa na FFU Tanzania na ndio sababu wanaitwa General Security Unit

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…