Sipendi kufundishwa napenda kusoma mwenyewe vile vitu nina interest navyo. Tatizo linaanza lazima nifanyie mitihani kile kilichoelekezwa hivyo lazima nisome.
Sipendi kutongoza. Natamani ile mnakubaliana tu kwa mkataba sio mambo ya 'wewe ndo kila kitu kwangu'. Walionilea utotoni waliniharibu kuondoa elements za uongo kabisa. Nalazimika tu nikizidiwa ila nikipata tulizo niliyemtongoza jana akaelekea naweza nisimtafute kwa miezi kadhaa (nitamrejea kumtongoza tena)
Sipendi kukosoa. Mimi ni mkosoaji mkubwa mno, nikipata huduma mbovu sehemu natafuta msimamizi. Nikimuona natoa mapendekezo utadhani nilichangia mtaji. Hii hali siipendi kwa vile inachukiza watu ila inanikereketa sana nisipotekeleza. Wanaonijua wakifanya kitu wananiletea nikosoe.