Ni kitu gani hupendi kuambiwa ambiwa kuhusu wewe yaani kinakukera?

Unaoa lini mbona vijana wenzio wote wameoa hili swali naulizwa na marafiki zangu, mama yangu, majirani, wadogo zangu. lakini kusema ukweli siwaamini wanawake na ndiyo maana sijaoa
 
Hujamaliza digrii tu mbona ada sio kubwa? Utafikiri wanajua nazongwa na mangapi
 
We nae unapenda kujifungia fungia ndani😅😅...
 
Hili suala la kunipangia watoto linakera sana, wengine wanataka tuzae kama visungura tuteseke kama wao.


Mimi nina falsafa yangu, nimejipangia utaratibu wangu kuwa nitazaa wachache kwa kuwa malezi nayo gharama siku hizi so sitaki nizae malezi yanielemee mpaka nishindwe kuishi.

Mimi napenda majukumu na bata, sasa jitu linataka kuniletea utaratibu wake kama sio kutaka tutaabike kama wao ni nini?

Ama wasio na watoto wananyanyasika, kama tu ukiws nao unasemwa usipokuwa nao itakuwaje?
 
Usiingize yote ingiza kichwa tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…