Kuna wakati nawaonea huruma watu wanaoa na wenye mipango ya kuoa kama wanawake wenyewe kumbe wako hivi wakishaolewa na kupata mtoto au watoto wengi huanza harakati za kurudisha mahusiano yao na ex wake wa zamani.
Kipindi cha nyuma nilikuwa nina amini wanawake wengi wakishaolewa huwa hubadilisha namba za simu kuepuka usumbufu na kukata mawasiliano kabisa na wanaume aliowahi kudate nao ila kumbe hili jambo huwa ni la muda tuu baada ya muda kupita huanza kuwatafuta ma ex wao na tena cha kushangaza kumbe wanawake huwa hawafutagi namba kabisa za ex wao nasema hivyo jamani kwa sababu nina mifano mingi.
Je shida huwa nini
kwa nini tunaoa au kuolewa na je ni kwa namna impendezayo Mungu? Kwenye jibu hapana hilo lazima litokee.
Pilau ya nyumbani huzoeleka na pilau ya harusini haizoeleki. Na hii mazoea ni katika himaya ya shetani kifikra na kimatendo.
Historia ya uasherati hutibiwa kabla ya kuingia kwenye ndoa, toba ya amri ya sita.
Upendo dhidi ya sababu kuhusu uwepo wa ndoa na katika kupitia milima na mabonde ya furaha na huzuni katika ndoa.
Wapo wanaoendelea na maex wao muda wote kabla na ndani ya ndoa muda wote,
Wapo wanaongoja au kuanguka nyakati ngumu kimaisha aidha kiuchumi,na mengine
Wapo ambao ni kukosa kutimiza malengo yao ya kuingia kwenye hip ndoa
Mafanikio au Maisha ya Maex ukilinganisha na yeye na mwanandoa wake kama ex anavutia zaidi
Ex anaishi katika ujirani mkoa,mtaa,wilaya etc
Hulka ya mwanandoa mfano umalaya au mama cha wote.
Asiyekuwepo nafsini huwezi kumpa ya nafsi. Ex ananipatia sana je mume umemwambia.
Furaha ya nafsi ni maandalizi ya nafsi yenyewe na ushiriki wake. Kuridhika kunaanza na wewe na mwenye vigezo na tafsiri ni wewe ukimya haunihusu. Kuridhika ni relative term.
Dunia inasemaje na wewe akili yako inaonaje dunia.
Mungu ana nafasi gani katika maisha yake au yenu?
Dhambi ya mwanandoa kamwe haibebwi na mwenza.
Kama ilivyo kaburi basi hata dhambi kila mtu hubeba zake.
Uvumilivu, subra, umoja, ndoa ni taasisi mali ya watoto ni msingi wa elimu ya ndoa.
Maarifa ya chochote ni ushindi.
Amani VS Ushindi
Ushindi VS Amani.
Kataa vita ushindwe na uwe na amani au ingia vitani ushindwe na ukose amani, kataa vita ushindwe na ukose amani, kubali vita ushinde na ukose amani au pigana vita ushinde na uwe na amani.
kupanga ni kuchagua na kuchagua nako kuna vigezo na kuna muongozo.
Chagua muongozo wa Mungu au Muongozo wa Dunia.
A teacher with bad experience but with helpful teachings.
Altruism isn't costly but a blessing.