Ni kitu gani ulishawahi kudhulumiwa maishani mwako na kinakuuma mpaka leo hii?

Ni kitu gani ulishawahi kudhulumiwa maishani mwako na kinakuuma mpaka leo hii?

Tuanze na mtoa mada.
Dah sisahau pale nilipodhulumiwa zaidi ya 2.5M na mtu niliyemuamini kabisa mwaka 2008. Nilinunua bidhaa kwake na kuzihifadhi kwenye godawni lake, jamaa akanizunguka na kuuza ule mzigo bila ya ridhaa yangu baada ya kuona bei imepanda mara mbili ya ile kipindi nilichonunulia mzigo wangu.
 
Safi sana.! Umempa adhabu nzuri
Niligongwa masaa zaidi ya 6 hd wakavunja miguu, pua
Nililalia upande mmoja miezi zaidi ya 4
Mikono km ilikata mawasiliano sababu ya kuzuia magongo yasinifike usoni
Nilikuwa nikilia kila napotaka kusimama kwa maumivu
Harufu ya damu niliisikia kwa miezi
Bd matusi na kwenda kupiga hd wadogo zangu
Hy nilitakiwa kumuuwa kabisa
 
Maisha haya yana changamoto zake na mara nyingi watu tuliowaamini ndio wanaotuacha na makovu makubwa, hasa unapojitoa mhanga kutafuta ridhiki na mtu akajimilikisha jasho lako bila huruma. Ni vigumu sana kusahau, lakini mwishowe inabidi tu uone kama funzo la maisha ili usiruhusu watu wakutumie kirahisi hapo baadaye. Pole sana kwa yaliyokukuta, ni uzoefu mchungu lakini ndio unaokujenga kuwa makini zaidi na watu wanaokuzunguka.
 
Niligongwa masaa zaidi ya 6 hd wakavunja miguu, pua
Nililalia upande mmoja miezi zaidi ya 4
Mikono km ilikata mawasiliano sababu ya kuzuia magongo yasinifike usoni
Nilikuwa nikilia kila napotaka kusimama kwa maumivu
Harufu ya damu niliisikia kwa miezi
Bd matusi na kwenda kupiga hd wadogo zangu
Hy nilitakiwa kumuuwa kabisa
Kifo ni adhabu ndogo sanaa kwa adui yako watu hamjui tu!
Hiyohiyo ya upofu ndo nzuri ila ungemuongezea na bawasiri
 
Uzi unajieleza wakubwa..

Funguka utueleze ili tupate kujifunza.

karibuni
let me declare interest first: mimi ni risk taker toka utotoni, na sina uoga kwa yeyote.
nikiwa katika 20+ wakati huo dogo tu, nikapewa deal... deal lenyewe ni la biashara ya madini.. nikaambiwa natakiwa nitoe 15M tununue kisha nipate 100M ya mgao, wakishayauza. wakati huo ni heya nyingi sana. niliingiwa na tamaa sana.

nikaparangana nilivyoparangana, nikadanganya nilivyodanganya, nikajinyima mpaka tone la mwisho, nikaipata. nakumbuka gf wangu nilimdanganya akanichangia 5M, sijui aliwadanganyaje ndugu zake.

yule jamaa akaniambia issue hii ni ya siri, na kaulimbiu ni trust.. basi, nakumbuka nilimpa cash kabisa.. na siku hiyo niliiweka hela kwenye begi pamoja na minguo mingi mno ili nizuge...

nahisi kulia.... nisiendelee sana... ila pale kwenye lile daraja, sitopasahau, ndipo pesa zangu zilipokwenda na mpk leo hazijarudi...

ila kwa kuwa mimi ni hustler toka utoto, pia ni mtoto wa mbwa, siwazi... na umri huu wa utu uzima, nimeshajilipa mara nyingi mno ya ile hela. kudhulumiwa kunauma sana
 
Back
Top Bottom