Ni kituko kuingia mkataba wa USD billion 42 za mkopo kwa ajili ya mradi mmoja tu wa kutengeneza natural gas refinery

Tatizo kubwa la hii nchi ni mitanzania yenyewe imeamua kuacha tu serikali ya CCM ifanye lolote lile bila bugudha yoyote ile na ndio maana wanaona Haina hata haja kujulisha umma kwenye baadhi ya mambo maana huo umma wenyewe hauwezi kufanya lolote.

Sasa hivi akili za watanzania walio wengi hasa wasomi Wala sio kulisaidia taifa, Bali ni jinsi gani na yeye atapata nafasi ya kuingia kwenye system hili na yeye awe ni sehemu ya wanufaikaji na huu mfumo corrupted. Sasa unapokuwa na taifa ambalo watu tarajiwa wakuletea maendeleo ndio wanakuwa na mawazo haya, basi wewe sahau kabisa kitu kinachoitwa maendeleo.

Nchi imeoza karibu kwenye angle zote muhimu sio mahakamani, sio bungeni Wala sio kwenye muhimili uliojichimbia chini zaidi.

Mahakama na Bunge zimekuwa ni vyombo vya kulinda maamuzi yanayotoka ofisi kuu haijalishi ni maamuzi yanayoashiria matokeo gani huko mbeleni.

Binafsi Mimi naamini hata ikitokea leo hii mwarabu akahitaji kukabidhiwa mkoa mmoja hapa Tanzania mfano kama Tabora, kwa kigezo Cha kwamba anataka kufanya uwekezaji wa asali, Basi chura Kiziwi atawaondoa wakazi wote wa Tabora kwa lazima na kuuacha mkoa mweupe na kisha kumkabidhi mwarabu na Hawa wasomi wetu tulionao wakamsifia kwamba ni uamuzi wa busara.

Huwa sipendi kuilinganisha nchi yetu hii na majirani zetu Kenya, maana kama ni suala la kujitambua kati yetu sisi na wao ni kama mbingu na aridhi.... Hii nchi ni Aibu sana hata kusema wewe unatokea humu.

Binafsi nilisha give up kuwa na matumaini yoyote kwamba Kuna siku hili taifa litasonga mbele na kutoka hapa lililopo, maana kadri siku zinavyozidi kwenda naona tunazidi kwenda shimoni tu..

nchi hailewiki, uchumi wa watu mmbovu, umasikini inaongezeka, haya hata usalama wa watu nao pia siku hizi haupo.... Watu wanatekwa mchana kweupe na watekaji wanajitambulisha kabisa wao ni maaskari bila kuogopa, halafu Kuna wajinga wanataka sijui eti tuwe wazalendo serious?

Nchi imekufa kisiasa na kiuchumi na hakuna Cha kijivunia kwenye hili taifa.... Labda machawa
 
Hata upasuke mishipa ya fahamu, Samia atabaki ni vchaguo la Mungu. Sina masilahi yeyote zaidi ya Utanzania wangu. Yule Mrundi wa Chato alikuwa anaharibu nchiyetu na Mungu akamuona. Kisha kampeleka jehanam!!
 
Mwaka 1979 huyo rafiki yako Muammar Qaddafi alipomsaidia Nduli Idd Amin askari pamoja na silaha za kivita kuipiga Tanzania nina imani ulikuwa haujazaliwa. Gaddafi alikuwa kiongozi mbaya. The worst despotic leader in history of Africa.

Zaidi ya hapo ni muhimu ukajenga utamaduni wa kusoma historia na kupitia taarifa za vyanzo mbalimbali ili kupanua uelewa. Libya chini Muamar Gadafi ilitunza magaidi, wateka nyara au hukumbuki Lockerbie bombing ya 1988 kwa flight namba 103 ya Pan Am

Gaddaf wala siyo shujaa huwa namuona ni mpuuz mmoja tu kama akina Mobutu au Nguema au Bokassa.
Kiongoz shujaa lazima usikilize wananchi wanasema nini. Kwanini asingewaachia nchi wananchi? Aliifanya Libya kuwa ni ya kwake na familia yake, huyo ndiyo umamsifia. Alikosa nini mpaka ang'ang'anie madarakani?
 
Katika maisha kama kupishana maono ni uchawa basi hata wewe ni chawa wa unayemtetea.
 
Hata upasuke mishipa ya fahamu, Samia atabaki ni vchaguo la Mungu. Sina masilahi yeyote zaidi ya Utanzania wangu. Yule Mrundi wa Chato alikuwa anaharibu nchiyetu na Mungu akamuona. Kisha kampeleka jehanam!!
Haya sikatai kwamba huyo Samia ni chaguo la mungu wa huko kwenu, maana Mungu wenu huyo anayeabudiwa na nyie machawa na mafisadi alishirikiana na nyie kumfanya akae hapo kwenye hicho kiti.

Kuhusu mrundi Mimi sijui kama taifa lenu hili limewahi kutawaliwa na mrundi, hiki nacho ni kiashiria kingine Cha udumavu wa akili kuongea vitu ambavyo huna uthibitisho.

Na kama huyo mrundi aliiharibu hii nchi yenu, basi hichi kibibi Cha kizanzibar ndio kinaenda kuizika kabisa huku waking kama wewe mkimpigia makofi sababu ya vijisent mnavyonufaika navyo ambavyo ni matokeo ya udhaifu alionao!

Anyway, kupitia comment zako nazidi kuamini ule msemo wa kwamba hata nyie wapumbavuu uzeeka.
 
Katika maisha kama kupishana maono ni uchawa basi hata wewe ni chawa wa unayemtetea.
Siwezi kuwa chawa kwenye maisha yangu hata iwe vipi...!! Hiyo kazi ntawaachia binadamu mliokosa thamani ndani ya nafasi zetu kama wewe.

Yaani unajua kabisa hii sio sahihi, ila unajikaza na kutoa povu kwamba ni sahihi.... Upumbavuu huo mtafanya nyie na wenzako wenye akili kama zako
 
Zanzibar ni sehemu ya Muungano wa JMT wewe pimbi. Mnakula makande na kuvuta bangi chooni na haya ndiyo matokeo yake. Mnaandika vitu vya HOVYO
 
Watekelezaji wa maovu anayo panga Samia ni hao hao "machawa", kwa hiyo chawa ni hatari kubwa kwa taifa letu.
 
Huwa sipendi kuilinganisha nchi yetu hii na majirani zetu Kenya, maana kama ni suala la kujitambua kati yetu sisi na wao ni kama mbingu na aridhi.... Hii nchi ni Aibu sana hata kusema wewe unatokea humu.
Sijui wewe ni mtu wa umri gani mkuu 'Muhimbu', lakini kuna nyakati za huko nyuma ilikuwa ni heshima kubwa sana kwa mtu kujitambulisha kuwa yeye ni mTanzania, popote duniani. Sisemi haya kwa kuambiwa, nayasema kwa kutambua na kujuwa heshima kubwa iliyo kuwa nayo nchi hii.
Sasa hivi ni aibu kubwa kujitambulisha kwa jina hilo; kwanza hata ni nani anajuwa hiyo nchi ilipo sasa hivi. Sana sana utaulizwa habari za Taiwan au Tasmania!

Nchi hii ina kila kitu cha kuipa heshima, lakini kwa jinsi viongozi hawa wanavyo tupeleka, miaka mingine mtano ya aina hii, hatutakuwa tofauti sana na Haiti. Siwezi kushangaa Kenya wakileta olisi kusaidia raia wanaotekwa na kuuawa hovyo na magenge ya wana CCM.
 
Huna Cha kuniambia kuhusu historia ya watu viongozi mahiri kama Gaddafi, najua ukweli ni upi na propaganda na zipi, viongozi kama wale lazima ziwepo propaganda za kuwachafua maana hawakukubali kuwa wajinga.

Viongozi kama Gaddafi anachukiwa na majitu yenye mindset za kifisadi au watetezi wa majizi kama wewe... Kwa ufupi tu watu wenye akili dumavu na ambao hata shule hamjaenda ndio mtamchukia Gaddafi.

Haya Muammar Gaddafi alikuwa anatunza magaidi kama ulivyoaminishwa, lakini sijaona ukikanusha hayo mazuri aliyoyafanya kwa wanainchi wake?? Je, hayakuwepo???

Ni heri uishi chini ya utawala wa kiongozi mzalendo shupavu kama Gaddafi ambaye anajua taifa lake na wanainchi wake linataka nini, kuliko kuishi kwenye utawala dhaifu unaojinasibu ni wa kidemokrasia unaolea mafisadi na rushwa ikitamalaki.

Ni uwendowazimu kujisifu eti una demokrasia wakati serikali yako inafuga wezi, majizi na Wala rushwa na usalama wa raia ukiwa hatarini Kila leo.

Serikali yenu ya Samia ni Moja ya serikali za kipuuzi kuwahi kutokea hapa Afrika kwa yeyote mwenye akili timamu anajionea ni jinsi gani alivyoshindwa na nchi inaelekea korongoni. Na pia vile vile amonesha muda wa wanawake kuongoza taifa changa kama hili Bado sana na kitu kizuri wanaosema hii kauli mara kwa mara ni wanawake.

Ni nyie machawa,watumishi wazembe na majizi ndio mnaona Kuna la maana analofanya, na Kuna uwekano mkubwa huu ukawa ndio mwaka wa mwisho wa yeye kuitwa raisi wa JMT.
 
Kaka Mimi ni mtu mzima ambaye Mpaka kufikia hapa nimeshuudia awamu nne nikiwa na akili zangu timamu, hivyo mambo Mengi kuhusu taifa hili ninayajua hata kama sio kwa upana sana.

Yes, miaka Fulani ya nyuma kipindi Bado viongozi na jamii yetu kwa ujumla Ina hofu ya Mungu na inatambua nini maana ya uadilifu, ilikuwa ni heshima kubwa sana mtu kuwa na passport ya kitanzania...!!

Kwa raia yoyote wa kigeni aliyewahi kuishi Tanzania miaka ya 1990s leo hii Akija Tena Tanzania halafu akakuta eti Bado tuna shida ya umeme na maji lazima atudharau sana, na atakuwa sahihi kutudharau.

Yaani nchi potential kama hii ambayo haina historia yoyote ya civil wars tangu imepata Uhuru miaka zaidi ya 60 iliyopita, eti Bado mpaka leo hii hatuna umeme wa uhakika na karibu 75% ya barabara zetu hazina Rami na kama hiyo haitoshi Bado tunategemea wahisani kukamilisha miradi Mingi ya maendeleo.

Nchi ambayo wanainchi wake wengi wanaingia kwenye system ya Ajira za serikali sio kwa ajili ya kulitumikia taifa lipate maendeleo, Bali ni kwa ajili ya kujipatia pesa za haraka kwa njia za ubadhirifu.... Taifa kama hili ni halali kabisa mtu akilidharau.

Binafsi Mimi huwa naamini kwa huu uelekeo alionao Samia kama atapewa miaka mingine 5 basi hili nchi tayari itakuwa ni ya walowezi na kama kuna kitu ambacho watanzania watabaki wanamiliki basi ni ndala zao tu... Na kwa miaka 10 ijaiyo kama itabaki mikononi mwa CCM naiona ikidumbukia kwenye uharifu uliokithiri na umasikini wa kutisha na hapo tutaanza kuona idadi kubwa sana ya watanzania wakitamani kuikimbia kabisa nchi yao kuhamia kwenye mataifa mengine kama wanavyofanya wanaijeria.

Kiufupi tu kukosekana kwa viongozi wenye maono na badala yake tukapata walafi na majizi wakilindwa na machawa wao kumefanya tiafa liendelee kubaki hapa hapa lililopo miaka nenda miaka Rudi.
 
Pesa iwe kubwa ama kidogo,hakuna mabadiliko chanya atakayopata mtanzania aliye nje ya mfumo wa ulaji.Hapo wanachodiscuss si nchi itafaidika nini bali nini individuals walio kwenye mfumo wataifaidi
 
Maona siyo ya kiongozi bali ni ya Taifa. Na kwa Tanzania tuna Vision 2025. Sasa wewe unasema eti kukosekana kwa kiongozi mwenye maono. Huijui Tanzania wewe bado mtoto mdogo
 
Kiufupi tu kukosekana kwa viongozi wenye maono na badala yake tukapata walafi na majizi wakilindwa na machawa wao kumefanya tiafa liendelee kubaki hapa hapa lililopo miaka nenda miaka Rudi.
Tanzania hatuna tatizo zaidi ya hili ulilo litaja kwenye hii mistari miwili ya mwisho.
Korea Kusini, wana kitu gani zaidi cha kuishinda Tanzania? Hivyo hivyo na mifano mingi sana mingine, kama Taiwan; Israel wana nini? Vietnam, Thailand, wana nini cha ziada? Hivi vi-inchi vyote vya Ulaya vilivyo kuwemo kwenye Himaya ya ki-Soviet, ambavyo sasa ndio wanaotuamrisha na uana chama wao wa 'European Union' na EPA yao, wana kitu gani cha ziada kuliko tulicho nacho sisi Tanzania?
Na wao walihangaika sana kama anavyo hangaika kiongozi wetu kwenda kutafuta watu/makampuni ya kutumia raslimali zao kama anavyo fanya Samia, ndipo wakapata maendeleo waliyo nayo leo?
Na wao waliambiwa na viongozi wao wakuu kuwa ni wavivu, wezi,n.k. kuwa ni kazi bure kuwategemea wao kuziletea nchi zao mabadiliko?

Leo hii, hata mambo madogo kabisa tunayo weza kuyafanya sisi, inalazimu tukatafute watu nje? Viongozi hawana muda wa kufanya kazi na watu wao hapa hapa nyumbani; hata kuchimba vyoo vya mashimo,; kutunza mapori yetu na kupanda miti na kuitunza, hatuwezi?
Ndiyo, sasa furaha yetu angalau ni kuwaona wenzetu akina Mo, akina Roast; akina Abdallah Nahdi na pengine akina Abdul wakisahamiri; wakati wengi wetu tunaandaliwa kuwa watwana tu, wa kuwatumikia hao wanao leta mitaji yao hapa kuvuna na siyo kutunyanyua kama taifa!

Nina imani tutaachana na upumbavu huu hivi karibuni.
 
Maona siyo ya kiongozi bali ni ya Taifa. Na kwa Tanzania tuna Vision 2025. Sasa wewe unasema eti kukosekana kwa kiongozi mwenye maono. Huijui Tanzania wewe bado mtoto mdogo
Sasa wewe ni kipi usicho elewa hapa. Huyo kiongozi na serikali siyo wahusika wa kutunga sera za waTanzania kutekeleza na kunufaika na maono hayo?
Badala ya kufanya hivyo, kiongozi yeye anatumia nafasi hiyo kutumia maono hayo kwa kunufaisha wengine zaidi ya wananchi wake!
Kiongozi anaamini nafasi ya waTanzania katika maono hayo ni kuwa watwana wa kuwatumikia hao anao walinda kunufaika na maono! Hili hulioni!
 
Usipotumia akili yako kisawasawa utapitwa na fursa na utaishia kuwa Mr Malalamiko huku wenzio wanapiga hatua.

Hata Wamalawi wasio na kisomo wameona Tanzania fursa lakini bado wewe unajadili maono ya Rais.
 
Watekelezaji wa maovu anayo panga Samia ni hao hao "machawa", kwa hiyo chawa ni hatari kubwa kwa taifa letu.
Adui namba Moja wa hili taifa kwa Sasa ni Hawa machawa, maana Hawa ni mashetani wanaojifanya ni malaika.

Haya ni majitu ambayo hata nchi ikuzwa yatatetea tu mathalan kuna fungu yanapata. Na hawaangalii kabisa kesho ya taifa na mbaya zaidi Kuna mengine ni masomi kabisa humo humo!

Mfano kama hili lizee tunalobishana nalo hapa, watu kama yeye walipaswa wawe mstari wa mbele kabisa kukemea kabisa utawala wowote unaendekeza ufisadi na wizi maana wanazijua changamoto za hili taifa kiundani kuliko sisi, lakini lenyewe ndio kwanza linakwambia eti Samia ni chaguo la Mungu... Jinga kabisa hili
 
Usipotumia akili yako kisawasawa utapitwa na fursa na utaishia kuwa Mr Malalamiko huku wenzio wanapiga hatua.

Hata Wamalawi wasio na kisomo wameona Tanzania fursa lakini bado wewe unajadili maono ya Rais.
We mzee una laana mpaka matakoni kwako!

Hivi kwenye awamu Kuna yeyote kati yenu wanufaika wa hii serikali dhaifu anayetumia akili hata kidogo zaidi ya kujipendekeza pendekeza ovyo tu?
 
Hilo "lizee" unalo lizungumzia, ni mtu mzima kabisa, tena mwenye uelewa mzuri kabisa wa mambo muhimu ya nchi yetu. Nasema hivi kwa sababu tokea huko nyuma siku nyingi nime badilishana naye mawazo humu humu JF.

Sasa ngoja nikwambie tatizo la baadhi ya hawa watu. Hizi imani tulizo nazo; ambazo kwa kweli ni tamaduni tu za kigeni zinawachukua akili baadhi ya watu kupita kiasi. Mtu wa imani yao tu akiwa madarakani, anachukuliwa kuwa mtu huyo hawezi kufanya makosa. Kiongozi huyo akisemwa kwa kushindwa uongozi, inaonekana kuwa ni imani yake na wao ndio wanao shambuliwa.
Watu wa aina hii wapo pande zote, lakini ni wazi kuwa hawa wa dini ya huyu mama wako mbele sana kumkingia kifua, hata aharibu kiasi gani.
Wao imani ni zaidi ya nchi, ambayo ni huyo huyo Mungu ndiye mlezi wa nchi yenyewe, bila kujali kiongozi mmoja tu.
Kwa hiyo, msukumo wa huyo, unaye muita. "lizee" nimejiridhisha kuwa anasumbuliwa na imani anayo changia na huyu mama kiongozi. Hakuna jingine zaidi ya hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…