Tatizo kubwa la hii nchi ni mitanzania yenyewe imeamua kuacha tu serikali ya CCM ifanye lolote lile bila bugudha yoyote ile na ndio maana wanaona Haina hata haja kujulisha umma kwenye baadhi ya mambo maana huo umma wenyewe hauwezi kufanya lolote.Hapa ndipo Tanzania ina kasoro kubwa sana, na CCM na serikali yake wanatumia mwanya huu kufanya uchafu wowote wautakao wao.
NGOs za hapa nazo zimekuwa kama sehemu ya serikali. Wasomi wenye uelewa, wao wanajisalimisha na kuwa "maprofesa walio okotwa majalalani".
Serikali imehakikisha Mahakama hakuna kitu, hata kama kutakuwepo na mtu au kundi litkalo pinga chochote kinacho fanywa na serikali bila ya taratibu kutimizwa.
Rejea IGA ya DPWorld ilivyo vungwa vungwa hadi Bungeni!
Hii ya hapa, ni tofauti kabisa na kule Kenya. Shuhudia jinsi Adani na uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta ilivyo kaliwa kooni hadi sasa!
CCM na viongozi wake wa serikali wanasubiri tafaruku kubwa, ndipo wajue kuwa hali imekuwa mbaya sana.
Tazama wanayo fanya na uchaguzi wa serikali za mitaa! Hawa watu kweli bado wanazo akili timamu vichwani mwao?
Sasa hivi akili za watanzania walio wengi hasa wasomi Wala sio kulisaidia taifa, Bali ni jinsi gani na yeye atapata nafasi ya kuingia kwenye system hili na yeye awe ni sehemu ya wanufaikaji na huu mfumo corrupted. Sasa unapokuwa na taifa ambalo watu tarajiwa wakuletea maendeleo ndio wanakuwa na mawazo haya, basi wewe sahau kabisa kitu kinachoitwa maendeleo.
Nchi imeoza karibu kwenye angle zote muhimu sio mahakamani, sio bungeni Wala sio kwenye muhimili uliojichimbia chini zaidi.
Mahakama na Bunge zimekuwa ni vyombo vya kulinda maamuzi yanayotoka ofisi kuu haijalishi ni maamuzi yanayoashiria matokeo gani huko mbeleni.
Binafsi Mimi naamini hata ikitokea leo hii mwarabu akahitaji kukabidhiwa mkoa mmoja hapa Tanzania mfano kama Tabora, kwa kigezo Cha kwamba anataka kufanya uwekezaji wa asali, Basi chura Kiziwi atawaondoa wakazi wote wa Tabora kwa lazima na kuuacha mkoa mweupe na kisha kumkabidhi mwarabu na Hawa wasomi wetu tulionao wakamsifia kwamba ni uamuzi wa busara.
Huwa sipendi kuilinganisha nchi yetu hii na majirani zetu Kenya, maana kama ni suala la kujitambua kati yetu sisi na wao ni kama mbingu na aridhi.... Hii nchi ni Aibu sana hata kusema wewe unatokea humu.
Binafsi nilisha give up kuwa na matumaini yoyote kwamba Kuna siku hili taifa litasonga mbele na kutoka hapa lililopo, maana kadri siku zinavyozidi kwenda naona tunazidi kwenda shimoni tu..
nchi hailewiki, uchumi wa watu mmbovu, umasikini inaongezeka, haya hata usalama wa watu nao pia siku hizi haupo.... Watu wanatekwa mchana kweupe na watekaji wanajitambulisha kabisa wao ni maaskari bila kuogopa, halafu Kuna wajinga wanataka sijui eti tuwe wazalendo serious?
Nchi imekufa kisiasa na kiuchumi na hakuna Cha kijivunia kwenye hili taifa.... Labda machawa