Tanzania hatuna tatizo zaidi ya hili ulilo litaja kwenye hii mistari miwili ya mwisho.
Korea Kusini, wana kitu gani zaidi cha kuishinda Tanzania? Hivyo hivyo na mifano mingi sana mingine, kama Taiwan; Israel wana nini? Vietnam, Thailand, wana nini cha ziada? Hivi vi-inchi vyote vya Ulaya vilivyo kuwemo kwenye Himaya ya ki-Soviet, ambavyo sasa ndio wanaotuamrisha na uana chama wao wa 'European Union' na EPA yao, wana kitu gani cha ziada kuliko tulicho nacho sisi Tanzania?
Na wao walihangaika sana kama anavyo hangaika kiongozi wetu kwenda kutafuta watu/makampuni ya kutumia raslimali zao kama anavyo fanya Samia, ndipo wakapata maendeleo waliyo nayo leo?
Na wao waliambiwa na viongozi wao wakuu kuwa ni wavivu, wezi,n.k. kuwa ni kazi bure kuwategemea wao kuziletea nchi zao mabadiliko?
Leo hii, hata mambo madogo kabisa tunayo weza kuyafanya sisi, inalazimu tukatafute watu nje? Viongozi hawana muda wa kufanya kazi na watu wao hapa hapa nyumbani; hata kuchimba vyoo vya mashimo,; kutunza mapori yetu na kupanda miti na kuitunza, hatuwezi?
Ndiyo, sasa furaha yetu angalau ni kuwaona wenzetu akina Mo, akina Roast; akina Abdallah Nahdi na pengine akina Abdul wakisahamiri; wakati wengi wetu tunaandaliwa kuwa watwana tu, wa kuwatumikia hao wanao leta mitaji yao hapa kuvuna na siyo kutunyanyua kama taifa!
Nina imani tutaachana na upumbavu huu hivi karibuni.
Man, hii inchi isingekuwa huku kwa wapumbavuu yaani ingekuwa hata Bara la Asia, leo hii inafukuzana na mataifa kama France,Japan,Uk na mengine makubwa unayoyajua wewe kiuchumi na global influence.
Tunaambiwa kilimo ndio backbone ya uchumi wa nchi hii, lakini tangu tumepata uhuru miaka 63 iliyopita ni 15% ya arable land ambayo ndio watanzania wanaitumia kwa kufanyia kilimo na hapo hapo Bado tuna import zaidi mazao ya chakula kuliko hata ya biashara.... Yaani tunaagiza Michele kutoka kwa vinchi kama Thailand? Na watu tunaowaita watunga sera hapa nchini wapo tu wanakula mishaara na posho????
Nchi ndogo kama Estonia Ina wawekezaji wengi kuliko Tanzania ilihali population yao haizidi hata 2m na rasilimali tumewazidi, mind you Hawa Estonia walikuwa kwenye USSR, Kuna mambo ukiwaza mpaka unajiuliza watunga sera wetu huwa wanawaza nini...
The fact that nchi hii haijawahi kuvurugwa na vita vya aina yoyote ile zaidi ya ile ya Kagera lakini mpaka leo hii zaidi ya 70% ya wanainchi wake hawana stable accessibility ya maji safi na salama majumbani mwao licha ya kuzungukwa na Maziwa pamoja na bahari ni Moja ya maajabu ya dunia...!! Yaani Kuna vitu ambavyo haviitaji kabisa kutumia nguvu Wala akili nyingi ni commitment tu basi, lakini sisi tumeshindwa.
Nchi za kiarabu(Middle Eastern countries)hazina wataalamu kulinganisha na nchi za magharibi, ila wao wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kutumia rasilimali zao(Mafuta) kupunguza umasikini kulinganisha na sisi.
Na waarabu waliweza kufanya hilo kwa kuwa na sera thabiti tu basi, mtu anakuja kuchimba mafuta ila mnufaika mkubwa ni serikali, ambapo serikali inatumia fedha hizo kuboresha maisha ya jamii kwa ujumla(general wellbeing of the society) kwa maana ya kuhakikisha huduma zote muhimu zinapatikana kwa usahihi kabisa.
Njoo kwetu sisi hapa, ku utilize hizo rasilimali lukuki tulizonazo hatuwezi, sera zenyewe tulizonazo ni za kipuuzi na kinyoji na wanyonywaji ni sisi wenyewe... Pesa tunazopata kwenye rasilimali zetu ni kidogo sana na Bado hizo hizo kidogo zinaishia kwenye matumbo ya watu wachache, Sasa hapo kwanini tusiwe na idadi kubwa ya watwana?
Viongozi wetu wanachoweza kufanya ni kutunga ineffective policies pasipo kuangalia mustakabali mzima wa taifa hasa vizazi vya mbeleni, mathalani tu hizo sera zinawanufaisha wawekezaji na wao wenyewe binafsi baasi na ukihoji unatukanwa au kupotezwa kabisa.
Leo tunatamani kuwakabidhi Kila kitu wageni ndio watuendeshe kisa na mkasa eti sisi hatuwezi na tunaendekeza sana wizi na hivyo kupeleka ufanisi kukosekana..... Sasa kama tumeshindwa kuzuia huo wizi sisi kwa sisi ndio hao wageni watashindwa vipi kutuibia??? Kuna maswali huwa najiulizaga kuhusu mambo yanayoendelea kwenye hii awamu nnabaki kuuma meno tu.
Kuhusu kwamba eti sijui Kuna siku tutatoka kwenye huu ujinga tulionao sio leo Wala kesho kaka, hiyo kitu sahau.. sana sana tu tutazidi kudumbukia shimo zaidi hapa... Sasa hivi sio vijana Wala wazee wameamua kudadecate kwenye uchawa hili wale kirahisi na watawala kama hili lisen.ge tunalobishana nalo hapa