Ni kiumbe gani hukipendi/ unakiogopa mpaka leo?

Ni kiumbe gani hukipendi/ unakiogopa mpaka leo?

kinyonya aisee.nilienda kwabibi uwani kuna kiwanja kizuri kimestawi nyasi zakijani kibichi

nikajilaza zangu naburudika upepo mzuri kumbe kinyonga kaja kunikalia kwenye bega lakulia katulia

mdogowangu kanifata kuniita alivyomuona tu akaanza kupayuka kaka angalia begani kwako unanini
nikageuka kuangalia tuna onana ana kwaana Mimi nakinyonga katulia begani kwanguu

nikamkimbilia dogo anitoe dogo anakimbia muoga nae
nilipata tabusana

nilipiga mayowe hukunakimbia kuelekea bondeni kilanikikaza moyo nikimpangusa kwamkono hatoki kuchazake zimeshika kwenye shati mkia unanigusa shingoni aloo

nikaona kukimbia haitoshi nikaanza kuruka sarakasi hukunapiga mayowe watu nao wananifata kunisaidia

nikijaribu kuvua shati inagoma kutoka vivungo vyake ilimladi niteseke tuu nikaruka misarakasi nakujitupa tupa chini akaishiwa uzalendo akadondoka

Ile shati nilivuta vifungo nikaivua nakuitupa hukohuko shambani sikuichukua nilirudi nyumbani kitumbo wazi huku raia wananicheka[emoji1787][emoji1787]mdahuo nimenuna balaa.

Hadi leo nikiendo kijijini nakaambali na sehem zakijani kibichi mana vinyonga wanapenda sana sehemu hizo

nikimuona kinyonga nakosa amani kabisa namtupia mijiwe apotee alinitesa sana
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787]
 
Back
Top Bottom