Ni kosa gani ambalo utalijutia maisha yako yote?

Ni kosa gani ambalo utalijutia maisha yako yote?

Inauma mpaka natamani tujilipue wote bora watoto wabaki yatima ,najitahidi kuvumilia maisha yanavyoniwia magumu ndio hali ya malipizo inavyonijia sijawai kukaa dk 10 bila kufikilia na kujuta na hayo madogo niliyoeleza nikisema yote utoamini nilivumilia vipi na kwanini (alinifanyia dawa za kienyeji ) nae alishawai kukili,duniani kunawatu wanaloho mbaya shetani anasubili.
Mwanamke pambana usirudi nyuma hâta, Kama umelia Sasa sema basi songa mbele na piga hatua, wengi tupo kwenye matatizo na maisha yanakwenda, pigana kiume usiku na mchana, jiingize kwenye vikoba na michezo ya upatu hakika yataisha, hiki Ni kipindi cha mpito tu
 
Najuta kuachana na bf wangu baafa ya kuona hatuna future. Sasa hiv anataka kumuoa mwanamke mwingine kila nikiwaza ninavyompenda bado natamani kupasuka au nipotee nisishuhudie ndoa yao. Nimegundua ye ndo pekee ninaemuona kama mume kwa sasa. Huwa namwambia mwanamke alie nae ana bahati sana.
Nabukizingatia umri nao umeenda
 
Inauma mpaka natamani tujilipue wote bora watoto wabaki yatima ,najitahidi kuvumilia maisha yanavyoniwia magumu ndio hali ya malipizo inavyonijia sijawai kukaa dk 10 bila kufikilia na kujuta na hayo madogo niliyoeleza nikisema yote utoamini nilivumilia vipi na kwanini (alinifanyia dawa za kienyeji ) nae alishawai kukili,duniani kunawatu wanaloho mbaya shetani anasubili.
U need Jesua only to rescue u
 
Najuta sana nilitumia ujana wangu vibaya ,kuwa na demu kila kona ,nipo uzeeni sasa sina hata kibanda hii inauma sna
ha ha ha,kibanda cha nini tena mkuu?.

Anyway hujachelewa,afterall hata ujenge orofa 100 utaiacha tu,
kaburi lako ndo kibanda chako cha milele na milele
 
sasa tumekutana tena sasa ninampenda kupitiliza ila sitakubali anivue chupi, sababu nimeshaolewa na nina watoto wawili nae kashaoa, ila wote tunapenda na nimemkisi mala kibao sababu lips zake nitamu kwa kukisi....
Huyo lazima atakugegeda tu
 
Mi najutia kusoma SUA wakati huo nilikuwa na multiple admission ya SUA na UDSM. Ninajutia maana probation za zilinitesa sana hasa jamaa moja anaitwa SEMBUCHE. Ila naendelea kujuta pia kwa kozi niliosomea maana haina maslahi kabisa na haina heshima
 
Katika maisha yako huenda kuna kosa moja ulilotenda ambalo unajutia kulifanya na kama ungepewa nafasi usingerudia tena.

Mimi katika maisha yangu kosa kubwa nililotenda na ambalo nitalijutia katika maisha yangu yote ni kuchelewa kuanza shule. Nimeanza darasa la kwanza nikiwa na umri wa miaka 12 na kuhitmu darasa la saba nikiwa na umri wa miaka 19. Baada ya kuhitimu s/msingi nikakaa kwa muda wa miaka 6 kabla sijarudi shule tena na kurudia darasa la saba. Hapa nilikuwa na umri wa miak 25. Kwa bahati nzuri nikafaulu kwenda sekondari na kuanza kidato cha kwanza nikiwa na umri wa miaka 26. Bahati nzuri ni kwamba zamani hakukuwa na age sealing. Ingekuwa zama hizi nisingeruhusiwa kusoma shule. Namshukuru Mwalimu Nyerere kwa kuondoa ubaguzi wa kiumri kwenye elimu.

Nimesoma hivyo hivyo nikiwa babu hadi nimehitimu kidato cha sita. Kosa la pili ambalo nalijutia ni kusoma kozi ya ajabu ajabu ambayo haina tija wala mantiki ya kimaisha. Kama umri ungekuwa unaweza kurudishwa nyuma nikarudi kuwa mvulana kamwe nisingesoma kozi hii niliyosoma. Ningejitahidi nisomee udaktari au sheria.

Je, kuna kosa gani ulilotenda katika maisha yako ambalo litaendelea kukutesa maisha yako yote na ambalo usingependa kulirudia kama ungepewa nafasi ya kujisahihisha?
Mkuu tpaul mimi huwa naamini kuna mambo mengine yanatokea ''with purpose''. Na hata ulivyoelezea wewe nadhani huna haja ya kujuta bali ni kijipongeza kwa kuweza kufanya kitu ambacho watu wengine wengi wangekata tamaa. Nina mfano wangu hai: Miaka ya nyuma nilihudhuria interview moja kwenye shirika moja la umma matata sana kipindi hicho i.e. BIMA. Kwenye interview tulikuwa vijana 8 na walitaka kuchukua 5 wa kuajiri halafu wafanye mafunzo ya computer kwa ajili ya kuanzisha kitengo cha computer. Zilikuwa ni posts ''hot'' sana na mshahara mzuri mno. Halafu kipindi hicho sio wengi wanajua hata computer ni nini achilia mbali kuitumia. Basi tukafanya interview na kuambiwa turudi nyumbani kusubiri majibu. Nilikuwa na mtu aliyekuwa anafanyakazi ndani ya shirika hivyo nilikuwa na uhakika wa kuchaguliwa. Baada ya wiki moja nikakutana na mmoja wa wale wenzangu kwenye interview akaniambia yeye na wenzake watatu wameshaitwa hivyo nifuatilie. Nikaenda moja kwa moja ofisini kwa yule jamaa yangu na akanichukua moja kwa moja mpaka kwa mhusika. Ile tunaingia akatuambia zile nafaa zimeshajaa (kwani yule jamaa yangu alisahau kufuatilia). Basi nikarudi huku nikimlaani yule mzee. Basi wale wenzangu 5 wakafanya mafunzo na kuanza kazi. Lakini ninapoandika hivi sasa wote hawapo tena duniani. Ilikuwaje? Kipindi hicho ndio Ukimwi ulikuwa haujajulikana sana. Na BIMA enzi hizo ilikuwa na vimwana kweli kweli. Basi walipoanza kazi wakawa wanaonja onja kumbe ndio hivyo tena. Na kipindi hicho ukiwa na UKIMWI hamna dawa ya kupunguza makalio bali unasubiri kifo..
 
Back
Top Bottom