Ni kosa gani ambalo utalijutia maisha yako yote?

Ni kosa gani ambalo utalijutia maisha yako yote?

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] afu aliye kwambia mm mdada nani mkuu

Hahaha usiniambie na mimi nimekosea kama wewe ulivyokosea kwa yule jamaa yako aliyevuka barabara kijasiri wakati mnaonana
 
Katika maisha yako huenda kuna kosa moja ulilotenda ambalo unajutia kulifanya na kama ungepewa nafasi usingerudia tena.

Mimi katika maisha yangu kosa kubwa nililotenda na ambalo nitalijutia katika maisha yangu yote ni kuchelewa kuanza shule. Nimeanza darasa la kwanza nikiwa na umri wa miaka 12 na kuhitmu darasa la saba nikiwa na umri wa miaka 19. Baada ya kuhitimu s/msingi nikakaa kwa muda wa miaka 6 kabla sijarudi shule tena na kurudia darasa la saba. Hapa nilikuwa na umri wa miak 25. Kwa bahati nzuri nikafaulu kwenda sekondari na kuanza kidato cha kwanza nikiwa na umri wa miaka 26. Bahati nzuri ni kwamba zamani hakukuwa na age sealing. Ingekuwa zama hizi nisingeruhusiwa kusoma shule. Namshukuru Mwalimu Nyerere kwa kuondoa ubaguzi wa kiumri kwenye elimu.

Nimesoma hivyo hivyo nikiwa babu hadi nimehitimu kidato cha sita. Kosa la pili ambalo nalijutia ni kusoma kozi ya ajabu ajabu ambayo haina tija wala mantiki ya kimaisha. Kama umri ungekuwa unaweza kurudishwa nyuma nikarudi kuwa mvulana kamwe nisingesoma kozi hii niliyosoma. Ningejitahidi nisomee udaktari au sheria.

Je, kuna kosa gani ulilotenda katika maisha yako ambalo litaendelea kukutesa maisha yako yote na ambalo usingependa kulirudia kama ungepewa nafasi ya kujisahihisha?
hapo kwenye red umesema ukweli, hii nchi ukijua sheria umemaliza kazi, mwangalie lissu anavyojiamini mbele ya maccm?
 
Kuna dada mmoja nljua nampenda sana imean that true love ila sikumwambia thinking alikua na mtu...baada ya miaka kadhaa nilikuja kukutana nae mie nshakua na girlfrnd nikamwambia kuhusu mpenzi nlonayo kwake..yule dada ali lilia sana akanambia hakuna mwanaume amewai kumpenda kama anavyonipenda Mimi..tulibaki kulaumiana tu kwann hatukuambiana..na kwa mda huo mia nlikua na girlfrnd mwenyewe mimba ndo ikawa bas tena....
duuuh inauma sana mkuu...i see u wish you could turn back the hand of time
 
Mi najutia kusoma SUA wakati huo nilikuwa na multiple admission ya SUA na UDSM. Ninajutia maana probation za zilinitesa sana hasa jamaa moja anaitwa SEMBUCHE. Ila naendelea kujuta pia kwa kozi niliosomea maana haina maslahi kabisa na haina heshima
Mkuu umenikumbusha mbali sana. G.D.C. Sembuche bado hajastaafu? Ila yule babu anajua sana hesabu...anazeeka na hesabu zake.
 
Mkuu tpaul mimi huwa naamini kuna mambo mengine yanatokea ''with purpose''. Na hata ulivyoelezea wewe nadhani huna haja ya kujuta bali ni kijipongeza kwa kuweza kufanya kitu ambacho watu wengine wengi wangekata tamaa. Nina mfano wangu hai: Miaka ya nyuma nilihudhuria interview moja kwenye shirika moja la umma matata sana kipindi hicho i.e. BIMA. Kwenye interview tulikuwa vijana 8 na walitaka kuchukua 5 wa kuajiri halafu wafanye mafunzo ya computer kwa ajili ya kuanzisha kitengo cha computer. Zilikuwa ni posts ''hot'' sana na mshahara mzuri mno. Halafu kipindi hicho sio wengi wanajua hata computer ni nini achilia mbali kuitumia. Basi tukafanya interview na kuambiwa turudi nyumbani kusubiri majibu. Nilikuwa na mtu aliyekuwa anafanyakazi ndani ya shirika hivyo nilikuwa na uhakika wa kuchaguliwa. Baada ya wiki moja nikakutana na mmoja wa wale wenzangu kwenye interview akaniambia yeye na wenzake watatu wameshaitwa hivyo nifuatilie. Nikaenda moja kwa moja ofisini kwa yule jamaa yangu na akanichukua moja kwa moja mpaka kwa mhusika. Ile tunaingia akatuambia zile nafaa zimeshajaa (kwani yule jamaa yangu alisahau kufuatilia). Basi nikarudi huku nikimlaani yule mzee. Basi wale wenzangu 5 wakafanya mafunzo na kuanza kazi. Lakini ninapoandika hivi sasa wote hawapo tena duniani. Ilikuwaje? Kipindi hicho ndio Ukimwi ulikuwa haujajulikana sana. Na BIMA enzi hizo ilikuwa na vimwana kweli kweli. Basi walipoanza kazi wakawa wanaonja onja kumbe ndio hivyo tena. Na kipindi hicho ukiwa na UKIMWI hamna dawa ya kupunguza makalio bali unasubiri kifo..
Du kweli kabisa mkuu. Huu ushuhuda wako umenikumbusha mbali sana. Kuna jamaa mmoja alifukuzwa kazi TRA akaamua kusoma sheria...sasa hv ni lawyer mzuri tu. Rafiki zake aliowaacha TRA wote wamepukutika kwa ngoma.
 
Mkuu umenikumbusha mbali sana. G.D.C. Sembuche bado hajastaafu? Ila yule babu anajua sana hesabu...anazeeka na hesabu zake.
Mkuu kama unamjua sembuche maana na wewe ulisoma SUA!! mimi nimemaliza pale, kipindi tunaanza mwaka wa kwanza ndio jamaa aliacha kufunsha wahandisi...nadhani alistaafu!! niliskia sana habari zake mkuu
 
Mie nimejifunza mengi
Mimi nakumbuka na kujuta kwa kujifunza kwa nn sikuchagua mchumba kipindi niko chuo kikuu, sasa nimeajiriwa sehemu toka 2014, hamna wadada, siwaelewi kbs, fujo , nilitaka nioe mwaka huu lkn sina Mdada!!! Du sijui nifanyaje? Au nisubiri walimu wapy nimuombe DIO nikae na dawati pembeni nijifanye nakagua vyeti nijichagulie m1.
I am totally frustrated, nataka kuoa
 
Mie nimejifunza mengi
Mimi nakumbuka na kujuta kwa kujifunza kwa nn sikuchagua mchumba kipindi niko chuo kikuu, sasa nimeajiriwa sehemu toka 2014, hamna wadada, siwaelewi kbs, fujo , nilitaka nioe mwaka huu lkn sina Mdada!!! Du sijui nifanyaje? Au nisubiri walimu wapy nimuombe DIO nikae na dawati pembeni nijifanye nakagua vyeti nijichagulie m1.
I am totally frustrated, nataka kuoa
Relax, mkabidhi Mungu hitaji lako then endelea na maisha yako. Usiwe frustrated na kitu kimoja, kikakukosesha amani while una mambo mengine mia ya kushukuru na kukupa furaha. Usiwe desperate sana coz unaweza ukaishia kuangukia pua kwa sababu tu unataka kuoa mwaka fulani, ukishaingia ndani ya ndoa ndo unaona kumbe ulikurupuka. Usitake kuwa na deadline ya kuoa, ila concentration yako iwe juu ya aina ya mwanamke unayemuhitaji na juu ya kusudi la Mungu juu ya ndoa kwenye maisha yako. Ukishayajua hayo, then hutojali kuhusu muda. Let love find you + everything happens in God's perfect time
 
Mkuu kama unamjua sembuche maana na wewe ulisoma SUA!! mimi nimemaliza pale, kipindi tunaanza mwaka wa kwanza ndio jamaa aliacha kufunsha wahandisi...nadhani alistaafu!! niliskia sana habari zake mkuu
Yeah! Namjua sana mkuu. Ni mwalimu mzuri wa hesabu.
 
Relax, mkabidhi Mungu hitaji lako then endelea na maisha yako. Usiwe frustrated na kitu kimoja, kikakukoseshsa amani while una mambo mengine mia ya kushukuru na kukupa furaha. Usiwe desperate sana coz unaweza ukaishia kuangukia pua kwa sababu tu unataka kuoa mwaka fulani, ukishaingia ndani ya ndoa ndo unaona kumbe ulikurupuka. Usitake kuwa na deadline ya kuoa, ila concentration yako iwe juu ya aina ya mwanamke unayemuhitaji na juu ya kusudi la Mungu juu ya ndoa kwenye maisha yako. Ukishayajua hayo, then hutojali kuhusu muda. Let love find you + everything happens in God's perfect time
Bonge ya ushauri!
 
Najuta nilivyo mvumilia mwanaume miaka 20 bila matunzo na kujimudu mwenyewe kimaisha na kulea watoto mwenyewe yeye analeta pumbu tu na kipigo juu na alikuwa mdokozi wa vijisenti vyangu vya biashara nikamvumilia tu sababu akutetelesha msingi wangu lakini kilicho nifanya nilivue pendo na mwishoo wangu kwake na kilio kikubwa zaidi ya majuto alicho nifanyia kuniibia pesa zangu zote za mtaji mpaka sasa natangatanga nadaiwa pesa za mashure (private) mpaka wamenichoka kulialia wakati enzi zangu ilikuwa pesa ya madafu kulipia watoto 4 najuta kumvumlia mwanaume malio na kupoteza muda wangu na umri wangu wa ujana nikitegemea ataacha yanii daaa! Simsame mpaka uchumi wangu urudi tena ata Nikifa asije kwenye mazishi yangu ata jeneza asiguse atakuwa ananijoki tu nae anajua haya![emoji24] [emoji24] [emoji24]
hii kali
 
Dahhh ni mengi mabaya nimeyafanya lakini sijutii kitu chochote. Nielewavyo kila unachofanya maishani somo . Unapokosea au unapofanya jambo baya Umefeli Hilo somo .

Hakuna haja ya kugonga kichwa ukutani. Jifunze kutoka kwenye makosa yako endelea na safari .
Kujuta ni kupoteza muda tu .
 
Back
Top Bottom