Ni kosa gani ambalo utalijutia maisha yako yote?

Du pole sana mkuu. Huyo mwalimu alikuwa kauzu kuliko dagaa na alaaniwe kwa tabia yake hiyo chafu. Kumbe kuna walimu wapuuzi kiasi hiki?
 

Dah.... nikikumbuka niliyoyafanya...[emoji24][emoji24][emoji24]
 
Dah! Mimi najutia sana kwenda kusoma coz ya ajabu ajabu kweli UDOM...niliacha coz ya maana ya SUA Na Mzumbe nikakimbilia DOM..... Hilo jambo najutia hadi huu mda ninavyoandika hapa ....labda badae Mungu akinisaidia nitaacha kujutia.....
bila shaka ulibabaika na majengo mkuu
 
Ndo mana nasemaga huna akili wewe hadi unagongewa. Next time unagongwa ww
 
Pole mtoto wa Mafinga, afu utakuwa na Chura si haba.
 
.....yamwage hapa watu wajifunze mkuu.

Siku moja huko nyuma nilikua naendesha gari moja ya kijerumani.. dah nikaamua nijaribu kuzifikisha speed zile za ukweli..! Zile 200+.. kwa bahati mbaya sana kwenye kona flani hivi nikiwa kwenye site yangu.. nikaona ghafla watu kama saba hivi wapo pembeni yangu upande wa kushoto..! Walikua jamaa kama nane hivi..! Watatu kwa ghafla wakaingia kwenye ile yellow line kwa ndani na mimi nilikua 200+.. mkuu niliwazoa mazima.. niliogopa sana yani..! Moyo mmoja ukaniambia nisimame na mwingine ukaniambia nikimbie..! Na kwa splitsecond iyo nilikanyaga brake..! Na apo apo nikaachia mafuta..! Ila wakati huo naskia sauti ya kuburuzwa kwa bamper ya mbele na ilikua usiku nikaona mwanga wa mbele umefifia.. mzazi niliamsha ile mashine..! Niliamsha mbaya..! Baada ya siku kama tano hivi kwa ule mshtuko baada ya kufika safari yangu..! Nikapelega gari garage na kutunga story nzuri tu..! Ndipo nikaamua kurudi safari njia ile na kuamua kusimama maeneo yale (this time nilikua na gari ya mshkaji wangu)..! Asee kilicho niuma ni kwamba nilikuta msiba wa watu watatu.. na mmoja alikua kilema.. bro nilijikaza sana..! Na nikakuta watu wanalalamika kwamba hawa watu wanaopita njia hii wanakimbia sana..! Kaka niliumia mno kwa kujaribu high speed kizembe na kupelekea kifo cha jamaa..! Dah yani niliumia njia nzima..! Na nili late sana kurudi kwenye makazi yangu..! Laiti ningalikua kwenye speed ndogo ningali weza kuwakwepa wale jamaa.. lakini kwasababu ilikua speed kali nilishindwa..! Asee nikikumbuka inaniuma kweli yani..!
 
du pole sana mkuu...tubu kwa mola wako atakusamehe. mwendokasi unaua!
 
Nillikosea kutuma text ya kimahaba kwa shemeji yenu nkamtumia mother
du, ila mother huwa hawana noumer sana....sipati picha kama ingeenda kwa dingi hali ingekuwaje.
 
Najuta kua na yule msiachana fulani kipindi niko form 6, nilipata division 1 form 4, kipindi naingia form 5 nikapiga sana class, shule nzima nasifiwa. Nilipofika form 6 alitokea msichana mmoja wa kitajiri na kunipenda, nilidrop kutoka malengo uhodari wangu wote wa kutegemewa pale shuleni mpaka kupata division 3, sitomsahau yule msichana na najuta kua nae. Ndo nlipoamini majuto ni mjukuu maana nlitamani nirudie mtihani wa form 6
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…