Najuta kumsukuma hadi kuanguka chini mwalimu wa masomo ya biashara pale sekondari huko njombe JINA KAPUNI. .(MIAKA HIYOOOO);
kisa kilikuwa wakati niko kidato cha nne kulikuwa na mwalimu aliyekuwa akifundisha masoma ya biashara yaani commerce na book-keeping. nikiwa mwanafunzi muhamiaji, mwalimu huyu alishoboka nami, maana nlikuwa mtoto si haba.
Mwalimu yule akanichagua kuwa MONITOR special wa masomo ya biashara kila mara alikuwa akiniita ofisini kwake hunishikashika kiunoni na kunibusu huku akihema kama nguruwe.tabia ile sikuipenda na ilinichikiza sana kila alipokuwa akiingia darasani haishi kunitolea mifano kwenye mambo kama ya goodwill, suppy and demand ,goods and service, just to mention a few. wanafunzi wenzangu walimwita SHEMEJI
siku moja nliamua kumtolea uvivu , alikuja darasani akasema wote tuonyeshe maksi zetu tulizopata katika mtihani wa MOCK wa b. maths. (mimi sikuwa nimepewa maana wakati mwalimu wa math anagawa sikuwepo na alikuwa anagawa mitihani hiyo kwa viboko maana wengi tulifeli.). nikamwambia mwalimu mie sijapata karatasi. ghafla nikaona aaanza kunipekua kwenye mifuko ya sketi mara akaingiza mkono kwenye sweta eti aangalie kama nimweka katika shati, wanafunzi wenzangu wakaanza kushangilia.....
nikapata hasira nikamsukuma mwalimu akaanguka nikachukua begi ya daftari nikaondoka zangu. kesho yake sasa ilikuwa kimbembe... nilipigwa fimbo na walimu zaid ya 100. nlikuwa siwezi hata kuinuka. nikasingiziwa makosa kibao.... mara eti nimekata sketi mbele ndefu nyuma fupi wasijue ni mambo ya bootiiii, mara mie mjeuri. nikageuziwa kesi eti mie ndo najigonga kwa mwalimu lol sitajasahau. nikaitwa ofisi ya mkuu wa shule alikuwa ameokoka . nikamweleza kila kitu. walimu walitaka nifukuzwe shule ila mkuu akasema nipigwe viboko vitano na nikashone sketi mpya hali akijua kabisa sina kosa. na hata sheti sio ilikuwa fupi nyuma ila kwa sababu ya churaaaaaa!
NINACHOKIJUTA MPAKA LEO ;WALIMU WALINIFANYIA HILA,kunifutia masomo yangu ya biashara kinyemela siku naingia kwenye mtihani wa taifa kufanya mtihani wa book-keeping jina langu halipo the same applies to the commerce. nililia sana.ukizingatia ndio masomo yaliokua yanapanda. kwani mock nlipata dision two;18
pamoja na hila zao nilipata divion four;26 nikiwa na ccb nikaenda private a'level. nikatusua kama kawa. japokuwa ndoto yangu ilikuwa ni kuwa mhasibu kama baba yangu lol.
Natamani ile ingenikuta hivi sasa ningemlia pesa yake yule mwalimu na angepata nunge lol