Ni kosa gani ambalo utalijutia maisha yako yote?

Ni kosa gani ambalo utalijutia maisha yako yote?

Huu uzi utaliza watu majumban......nimejikaza kiume ila ningelia maama nimekumbuka makosa yangu mengi sana ambayo nahs siku nkiwahadithia hata ndgu zangu nahs wataniogopa!!!
tugusie kidogo nasi tujue mkuu kwa faida ya wengi
 
Kumuamini mwanaume kuwa ananipenda kama navyompenda. Kumpa moyo wangu wote.
The good side of the story ni kwamba, hakuniua kwa maumivu bali kanifanya kuwa very strong, ninayejiamini kuliko zamani na kutokumjali. Now anatamani nimpende km zamani... Nami siwezi tena
 
Sijutii kinachonitokea bali natafuta njia ya kupambana nayo, kwa sababu yote yalipangwa yanitokee, na najua mengi yanakuja mbele yangu. Ndio maana halisi ya maisha,
Maisha ya ni mitihani na siku ya mwisho itajulikana kama nimeshidwa au nimefeli
Kweli
 
Nilimkosea baba angu kwa makusudi kabisa nikiamini akija atanipiga ili Na mimi TUZIPANGE,ila aliporudi alilia na kutoa machozi mbele yangu huku akiniuliza kwa upole na uchungu "kwanini sam" SITOSAHAU ILE SIKU najuta najuta hadi kesho nikikumbuka ile kitu.
 
Ni kutokana shida, dhiki, manynyaso
Mateso,kejeli.....shida za hapa na pale

Kwa bahati mbaya nikapata ushauri
Kwa rafiki yangu ambaye alikuwa amejiunga na dhehebu ya kishetani
Inaitwa CHURCH OF SATAN/LUCIFER
ambayo makao makuu yapo marekani
Jimbo la network, ilianzishwa 30 /04/ 1966. ambayo kwa jina lingine wanaita THE BLACK HOUSE.
kwa sisi wafuasi wa hili dhehebu huwa
Tunaliita THE BLACK FLAME au THE CLOVE HOOF.
hii dhehebu haina tofauti sana na dhehebu ya ILLUMINATI,

Na kuna kitu watu hawajui, watu wengi ulimwenguni wamezoea kusikia madhehebu ya kishetani aina mbili ambayo ni FREEMASON na ILLUMINATI
lakini kumbuka kuna madhehebu ya kishetani yapatao 30 na zaidi.
( kutokana na masharti sitayataja )
Rafiki yangu aliunganishwa na mzungu
Ambaye ni raia wa marekani, na alinishawishi kwa muda mrefu kujiunga na dhehebu hili, nami nilikataa lakini baadae uvumilivu ulinishinda kutokana kwamba alikuwa akinishawishi kupitia kunipa fedha, kunipa million 2 kwake ilikuwa kawaida, kweli pesa shetani
Nikashawishika na kutaka kujiunga alifurahi mno na kupanga safari kuelekea marekani kwa ajili ya kuunganishwa na kuapishwa kuwa muumini wa dhehebu hilo la kishetani
Nilifanikiwa kwa kiasi kikubwa na baada ya hapo nikawa tajiri na masharti ya kafara yalipangwa,

Hayo ndio maisha niliyopitia hadi sasa
Ninao utajiri Mali za kutosha lakini moyo unauma kwa kutoa ndugu zangu kafara, tena ni kafara mbaya sikuwahi kuona duniani.
Na cha ajabu huwezi kujitoa kujitoa kwake ni lazima ufe ni lazima ulionje mauti. Na adhabu inapewa kuzimu.

Sitaki kuongea sana kwa sababu sheria na kanuni za the black house hairuhusu
Kuzungumzia kwa undani suala hili.
Nafikiri umenipa mkuu.........

[emoji17] [emoji25] [emoji29] [emoji29]
Ni heri anaeua mwili kuliko anaeua roho
 
1.Nina mdogo wangu wa kiume huwa anatembea haangaliagi.Basi siku hiyo asubuhi nikaskia puu nkaropoka huku natoka nje na ukome mana huangaliagi unatembea kama huna macho Laaahaula!kutoka nje ni mdingi kateleza akaanguka nlisikiaje aibu halafu na yeye akanambia sawa bhana.
Ikabidi nijitetee ila niloona aibu na kujiskia vibaya
Mpaka leo nikikumbuka najiskia vibaya japo yeye alielewa

2.Najuta kusoma course ambayo niliisoma tu kwasababu ntakuwa na uhakika wa kupata ajira mapema lakini looo!mpaka sasa nang'aa sharubu
Aisee! [emoji23][emoji23]
 
mpaka sasa sina majuto namshukuru Mungu kwa hilo manake biblia inasema kumcha Mungu ni chanzo cha maarifa! sometimes ukiishi maisha ya kumcha Mungu kuna mambo hutafanya kabisa and so majuto hupungua!kilichopo tuwalee watoto wetu vyema ili huko mbeleni wasitiririke kwa comments kama hizi za majuto yenye kuumiza mioyo
 
nikiwa darasa la 4, nilitaman kunywa sumu kwa aina ya maisha niliyoisha ujombani, maisha ya mateso, manyanyaso, hakuna hata ndugu aliyenipenda, nikifanya kosa ukoo wangu wote unapigiwa sm, kuwa watto wa marehemu wameshindikana mm na pacha wangu...
kwani mama yetu alifarik kwa maambukizi kipindi akijifungua na baba yetu alipata ajal ya mv Bukoba akiwa safarin kuja kutuchukua kutoka ujomban dom....
lakini mipango ya Mungu sio kama ya mwanadamu, mara ya mwisho nimemamaliza chuo, nilirud kijijin, wazee wa kijijini walibaki kulia sana kwa uchungu huku wakisema "akili ya Mungu aichunguziki"nakumrudishia MUNGU sifa na utukufu wake, maana walidhani tushakufa na sisi kwa HIV maana tuliondoka vichanga sana tu wadhaifu kiafya...
Akili ya Mungu si ya mwanadamu Ni kweli
 
Katika maisha yako huenda kuna kosa moja ulilotenda ambalo unajutia kulifanya na kama ungepewa nafasi usingerudia tena.

Mimi katika maisha yangu kosa kubwa nililotenda na ambalo nitalijutia katika maisha yangu yote ni kuchelewa kuanza shule. Nimeanza darasa la kwanza nikiwa na umri wa miaka 12 na kuhitmu darasa la saba nikiwa na umri wa miaka 19. Baada ya kuhitimu s/msingi nikakaa kwa muda wa miaka 6 kabla sijarudi shule tena na kurudia darasa la saba. Hapa nilikuwa na umri wa miaka 25. Kwa bahati nzuri nikafaulu kwenda sekondari na kuanza kidato cha kwanza nikiwa na umri wa miaka 26. Bahati nzuri ni kwamba zamani hakukuwa na age sealing. Ingekuwa zama hizi nisingeruhusiwa kusoma shule. Namshukuru Mwalimu Nyerere kwa kuondoa ubaguzi wa kiumri kwenye elimu.

Nimesoma hivyo hivyo nikiwa babu hadi nimehitimu kidato cha sita. Kosa la pili ambalo nalijutia ni kusoma kozi ya ajabu ajabu ambayo haina tija wala mantiki ya kimaisha. Kama umri ungekuwa unaweza kurudishwa nyuma nikarudi kuwa mvulana kamwe nisingesoma kozi hii niliyosoma. Ningejitahidi nisomee udaktari au sheria.

Je, kuna kosa gani ulilotenda katika maisha yako ambalo litaendelea kukutesa maisha yako yote na ambalo usingependa kulirudia kama ungepewa nafasi ya kujisahihisha?

Habari hii imetumika kwenye Kipindi cha JamiiLeo kinachorushwa kila siku jioni katika Channel ya JamiiForums kwenye mtandao wa YouTube.

Kuona kipindi hicho angalia video ifuatayo, acha maoni yako na kisha Subscribe kwenye Channel ya JamiiForums.

Joining national service after attaining my bachelor degree in a certain Engineering course.
Worst decision ever for the moment.
Maybe itanilipa ngoja niwe mvumilivu tu kiaina...
 
Back
Top Bottom