Daaaah acha kabisa kuna siku nimetoka dar saa 12 jion kuja mwanza niko peke yangu kwenye gari, basi nikafika moro nikaona isiwe shida acha nitafte abiria, bahati nzuri nikapata wa mwanza na shy gari ikakaa level seat. Mida ya saa tisa usiku nlikuwa singida sehem reli inapishana na barabara, and kabla ya hapo huwa kuna kona ya mushoto sasa nlikuwa nimetanguliza semi nikaona inanichelewesha, usiku nikitaka kuovertake kwenye zero visibility huwa naangalia taa za gari inayokuja mbele yangu nikiona kimya huwa nachomoa tu. Bwana eeeeh ila nimetokeza tu hivi nipo ubavuni mwa semi katikati gjafla naona semitrail ingine inapandisha ipo speed, jamaa ilibidi tu awe mstaarabu akaitoa nje ila nlikuwa nishakubali yaishe. Abiria wangu hakuna alojua kitu walikuwa wamelala wote