Ni Kosa gani la ovyo ulilowahi kufanya tangu uanze kuendesha gari?

Ni Kosa gani la ovyo ulilowahi kufanya tangu uanze kuendesha gari?

Mimi niliunga kama naenda mwananyamala ile barabara ya mwinjuma. Hata sijui hatma yake japo siku kadhaa niliulizia pale hakuna anayekumbuka hilo tukio so nadhani hakufa.
Unaweza Kukuta kwa huo uzembe wako bodaboda kakatwa mguu ni kilema na hawezi tena kuendesha boda yake [emoji1787][emoji1787]
 
kuendesha nikiwa nimevaa sendo ya masai ya kuchomeka, ikateleza nyuma wakati nataka kufunga breki,nikalamba ukuta, nilijilaumu bora ningeendesha peku
[emoji23][emoji23][emoji23] Kumbe traffic wako sahihi kushauri kutovaa hizo sendoz au kandambili
 
View attachment 2183189
Namfukuza Ranger.. Ameshaingia kwenye radar yangu.. Kumbe kuna Lorry mbili kati.. Nikahisi ninaweza kuzimaliza.. Aisee Lorry la kwanza limeisha naona TD42 Civilian inapanda.. Breki nimeshachelewa nitagusa Lorry.. Ikabidi nidownshift gear niingie pembeni..!uzembe..
MUNGU ni mwema..!
Huyo mwenye Nissan ni boya sanaa kwann asinge slow down na kupaki kushoto kwake anhekuacha ww umalize salama ..
Maana nyuma ya nissan hakukuwa na hatari yoyote ya gari
 
Huyo mwenye Nissan ni boya sanaa kwann asinge slow down na kupaki kushoto kwake anhekuacha ww umalize salama ..
Maana nyuma ya nissan hakukuwa na hatari yoyote ya gari
Makosa yalikuwa yangu.. Pia hiyo Ranger iliblock vision yetu.. Mimi sikumuona na yeye hakuniona.. Tumekuja kuhamaki baada ya Ranger kurudi lane yake..!
 
Pale studio kinondoni nikaunga kumbe taa zimeruhusu magari yanayonyoosha likiwemo mwendokasi. Pale kwenye ile njia ya kwenda mwananyamala.

Nilikanyaga mafuta sana sasa kumbe bodaboda kachomoka. Alijibamiza kwenye gari akaenda chini na mimi nikaunganisha spidi. Ilinitoka hela ya maana kurekebisha mlango uliopondwa.

Pale huwa nawakosa kosa sana bodaboda ipo siku nitaunga na mmoja
 
Na matukio mengi ila hili ni la kwanza, nilikua na week toka ninunue chuma. Nilikua bado na ule ulena sasa bhana unajua ukiwa na chuma kipya unakua na mapepe flani hv unaona kama foleni unachelewa hapo ushaanza kujua ku overtake kutembea na gari 100+ kwako ndo ujanja.

Sasa nilikua shekilango road napanda kutokea ustawi chuo pale niko spidi sasa pale mataa ya africa sana nikaona kijani ina count ipo 3 nikasema hapa nakanyaga wese niwai mataa aisee nikafanikiwa pita niko spidi balaa

kwa mbele ya mataa kama mita 50’hivi kuna tuta na nilikua sina hiyo idea kama kuna tuta aisee niko spidi balaa kufika pale nashtuka tuta hili break ikafeli aisee nilipaaa kama niko kwenye ndege nilibamiza gari sana kutua ikabd niingie kituon baada ya lile tuta. Nadhani mmepata picha lile tuta lilivyo kubwa.

Nashukuru Mungu gari ilikua salama sikuharibu chochote ilibd daladala aliyekuwa nyuma yangu ashuke kuniangalia alihis nimelewa lile tuta bila shaka wahanga ni wengi sana usiku huwa halionekani sana.
 
Me mwaka 2020 hapo nipo na gari jipya (kwangu jipya), sasa nikaona ngoja nilionje maana speed 260 wapi hapa Dar nitaitest, nikaenda Tanga kupitia Bagamoyo.

Baada ya siku mbili nikarudi. Sasa njiani nikasema ngoja nijaribu kupiga kibati hadi mwisho. Mvua ilikua imetoka kunyesha barabara ina madimbwi dimbwi ya maji.

Nikatafuta mahali njia imenyooka. Bwana nikakoleza kibati hadi 200 hivi. Kwa bahati mbaya nikapishana na Roli kubwa sasa ile likarusha maji yakajaa kwenye kioo cha mbele.

Ile kupanic nikataka kuwasha wiper zipunguze maji, sasa hapo nimetoka kutumia gari la Toyota nimehamia Mjerumani, aisee Toyota wipers zipo kushoto hafu taa kulia, mjerumani kinyume chake, dah aisee nilipanic sioni kitu mbele hafu nipo kibati mbaya.

Nashukuru Mungu njia ilikua imenyooka na haina magari zaidi ya ilo roli tuliopishana. Ilipokuja kukubali wipers nilirudisha speed maximum 80 aisee.
Hahahaha 😂😂😂😂🤣 nimecheka sanaaaaa!!! Jinsi ulivyoingia CHA KIKE...kwahiyo ulivyogusa upande WA kushoto uliwasha taa au?.

Mwaka Jana na Mimi nilijichanganya kipindi naenda mwanza nakumbuka gari ilikuwa speed 120 alafu nikashindwa kubalance speed na Kona ingawa Ile Kona haikuwa Kali Ila niliamini gari inalala vizur,aisee Ile Kona ilikuwa ya upande WA kushoto kwahiyo ilinazalimu nikae kulia kabisa upande WA pili ili kuipunguza makali.

Abiria walikuwa hawajui lolote linaloendelea Ila Ile situation ilikuwa mbaya sanaa maana Akili ilishakata Tamaa
 
Na matukio mengi ila hili ni la kwanza, nilikua na week toka ninunue chuma. Nilikua bado na ule ulena sasa bhana unajua ukiwa na chuma kipya unakua na mapepe flani hv unaona kama foleni unachelewa hapo ushaanza kujua ku overtake kutembea na gari 100+ kwako ndo ujanja.

Sasa nilikua shekilango road napanda kutokea ustawi chuo pale niko spidi sasa pale mataa ya africa sana nikaona kijani ina count ipo 3 nikasema hapa nakanyaga wese niwai mataa aisee nikafanikiwa pita niko spidi balaa

kwa mbele ya mataa kama mita 50’hivi kuna tuta na nilikua sina hiyo idea kama kuna tuta aisee niko spidi balaa kufika pale nashtuka tuta hili break ikafeli aisee nilipaaa kama niko kwenye ndege nilibamiza gari sana kutua ikabd niingie kituon baada ya lile tuta. Nadhani mmepata picha lile tuta lilivyo kubwa.

Nashukuru Mungu gari ilikua salama sikuharibu chochote ilibd daladala aliyekuwa nyuma yangu ashuke kuniangalia alihis nimelewa lile tuta bila shaka wahanga ni wengi sana usiku huwa halionekani sana.
Ila barabara zetu Tanzania sio rafiki kabisaa sometimes ni MUNGU Tu anatulinda na ajali
 
View attachment 2183189
Namfukuza Ranger.. Ameshaingia kwenye radar yangu.. Kumbe kuna Lorry mbili kati.. Nikahisi ninaweza kuzimaliza.. Aisee Lorry la kwanza limeisha naona TD42 Civilian inapanda.. Breki nimeshachelewa nitagusa Lorry.. Ikabidi nidownshift gear niingie pembeni..!uzembe..
MUNGU ni mwema..!
Ndugu yangu kama huku pembeni kungekuwa na mtaro pengine Leo usingekuwepo duniani yaani hapa ni MUNGU Tu
 
Siku ingine actually haikuwa kosa langu
Nlikuwa Dar kikazi nikamaliza saa saba mchana nikasema acha nikate km nikalale singida fyaaaaaaaa saa tano usiku nlikuwa singida nikalala pale. Ile naingia singida nikakuta mssd calls za kutosha za mkuu wangu wa kazi. Nikaangalia upande wa sms kaandika najua upo safari unarudi ukipata upenyo unipigie na hapo ulipo ulale keho utarudi morogoro kikazi.
Basi nikampigia akaniambiwa natakiwa morogoro kwa kazi maalum kwa week zingine 10 hapo nina miezi 2.5 nipo kikazi dar.
Nliagiza dem wa kukaza kutoka musoma so ilikuwa lazima nilale palena dem angekuja kesho yake so nlimuwahi singida anikute nishapumnzika then tugeuze wte hadi mwanza apande gar kurudi.
Ilikuwa ijumaa so ikabidi nispenda hadi jumapili saa sita nikamwacha akapanda mabasi ya musoma mm nikatafuta abiria wangu wa moro nikala level seat safari ikaanza. Mida ya saa 12 jion nlikuwa nishavuka dumila niko mbelembele sijui panitwaje
Sasa napenda sana ligi na gari yangu ni babywalker ila huwa nasumbua hatar
Nikawa nafukuzana na noah moja tuko kwenye kidown nimaiachia babywalker nipo kama 140kmh ndo top speed ya babywalker nyingi.
Nikanza kupishana na misururu ya masemi ya mizigo yalikuwa kama 10+ yanapanda, mara paaap jaaa wa rav4 kachomoka kuovertake yale madude nyuma yangu noa yupo takoni, nikamuwashia taa ya kuashiria anachofanya ni hatari, anakuja tu nikawasha taa ya pili plus honi , jamaa anakuja tu distance ishagoma nikahesabu hapa mzinga tayari warning ya tatu ni honi na brake kali hadi lami ikapiga makelele

Nlichokuwa najaribu ni kupunguza speed ya gari yangu ili pasiwe na impact kubwa angalau iumie tu gari sisi tubakie salama. I did this with all my conscious sikuwa nimepanic kabisa abiria wa mbele nashukuru alikiwa mzee naye hakupanic aliangalia ule mchezo wote. Tumebakiza kama mita 10 before impact noa ikabidi atoke nje ya barabara kushoto ili asiniingie nyuma maana kesi ingekuwa yake, mshkaji wa rav 4 naye akatoa gari nje ya barabara kulia ili kuepuka kesi, mm nlishika usukani ka nguvu ili baada ya impact gari isiingie uvunguni mwa semi
Basi nia na rav4 wakumana sijui hawakuumana mm sikusimaa na sikutaka maongezi maana lazima tungezipiga na mshkaji wa rav4
Mzee alinipongeza akaniambia mwanangu we jasiri sana, baadae noa alinikuta msamvu nashusha abiria tukacheka hapo tukaachana
 
Me mwaka 2020 hapo nipo na gari jipya (kwangu jipya), sasa nikaona ngoja nilionje maana speed 260 wapi hapa Dar nitaitest, nikaenda Tanga kupitia Bagamoyo.

Baada ya siku mbili nikarudi. Sasa njiani nikasema ngoja nijaribu kupiga kibati hadi mwisho. Mvua ilikua imetoka kunyesha barabara ina madimbwi dimbwi ya maji.

Nikatafuta mahali njia imenyooka. Bwana nikakoleza kibati hadi 200 hivi. Kwa bahati mbaya nikapishana na Roli kubwa sasa ile likarusha maji yakajaa kwenye kioo cha mbele.

Ile kupanic nikataka kuwasha wiper zipunguze maji, sasa hapo nimetoka kutumia gari la Toyota nimehamia Mjerumani, aisee Toyota wipers zipo kushoto hafu taa kulia, mjerumani kinyume chake, dah aisee nilipanic sioni kitu mbele hafu nipo kibati mbaya.

Nashukuru Mungu njia ilikua imenyooka na haina magari zaidi ya ilo roli tuliopishana. Ilipokuja kukubali wipers nilirudisha speed maximum 80 aisee.

Hahahah dah pole mkuu.

Maana najua ulipiga wiper ukajikuta umewasha indicator. Ukahisi kama wiper mbovu hivi.

Hiki kitu huwa kinachanganya sana ukitoka kwenye mjerumani ukaingia kwenye gari ya mzungu.

Sema tu huwa inakuwa vice versa, moment ya kuwasha indicator unajikuta umepiga wiper.
 
View attachment 2183189
Namfukuza Ranger.. Ameshaingia kwenye radar yangu.. Kumbe kuna Lorry mbili kati.. Nikahisi ninaweza kuzimaliza.. Aisee Lorry la kwanza limeisha naona TD42 Civilian inapanda.. Breki nimeshachelewa nitagusa Lorry.. Ikabidi nidownshift gear niingie pembeni..!uzembe..
MUNGU ni mwema..!
Aiseeee pole mkuuu.

Hii ilikuwa ni risk sana.

Shukuru huyo mwenye Nissan naye hakuhama maana mngevaana uso kwa uso.

Ni DashCam gani hiyo unatumia?
 
Back
Top Bottom