Me mwaka 2020 hapo nipo na gari jipya (kwangu jipya), sasa nikaona ngoja nilionje maana speed 260 wapi hapa Dar nitaitest, nikaenda Tanga kupitia Bagamoyo.
Baada ya siku mbili nikarudi. Sasa njiani nikasema ngoja nijaribu kupiga kibati hadi mwisho. Mvua ilikua imetoka kunyesha barabara ina madimbwi dimbwi ya maji.
Nikatafuta mahali njia imenyooka. Bwana nikakoleza kibati hadi 200 hivi. Kwa bahati mbaya nikapishana na Roli kubwa sasa ile likarusha maji yakajaa kwenye kioo cha mbele.
Ile kupanic nikataka kuwasha wiper zipunguze maji, sasa hapo nimetoka kutumia gari la Toyota nimehamia Mjerumani, aisee Toyota wipers zipo kushoto hafu taa kulia, mjerumani kinyume chake, dah aisee nilipanic sioni kitu mbele hafu nipo kibati mbaya.
Nashukuru Mungu njia ilikua imenyooka na haina magari zaidi ya ilo roli tuliopishana. Ilipokuja kukubali wipers nilirudisha speed maximum 80 aisee.