Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Uliweka floor ngapi wewe kama wewe tuache za wengine. Maana tukijadili za wengine watu wapo na mijengo tofauti.
 
Kuwa na slab haina maana hutafunga ceiling, washua wanafunga ceiling vizuri sanaView attachment 2500021
View attachment 2500024
Grill za ukweli balaa nimezipenda kiukweli. Ila chini ya slub hapo sijaona ulazima wa kuweka hizo boards maana ni extra but unnecessary cost. Maana kuna finishing ingepigwa hapo kwa kutumia ile material ya white cement ya kisasa plus wangetia na mauwa ya gypsum plus taa hapo katikati na kwenye kuta aaaaah ingekuwa si mchezo.
 
Wait, yaani unaweka mawe kwanza, then unalaza zege halafu kuanzia hapo ndio hizo 60cm au iweje maana sijakupata vema kuwa msingi unaanzia juu ya usawa wa ardhi au kutoka chini ya ardhi hadi kufikia usawa wa surface ya ardhi?!

Hebu fafanua vema hapa.
 
Kosa ni lako, kabla ya kuanza ujenzi ilipaswa uangalie mrejesho wa ramani. Hii ni lazima, hata huyo uliemkabidhi ilipaswa akuhoji vitu flan ili ajue ukubwa wa chumba. Mfano chumba cha watoto unataka vikae vitanda vingapi vya ukubwa gani? Hivyo
Hawa wachora ramani hawana hata passion na kazi yao. Mtu anakuwa na pupa ya kukuonyesha uwezo wake hata kabla hajakusikiliza unataka nini.
 
Open kitchen kwa wabongo haifai, uchafu mwingi sana. Unaweza jaza moshi na harufu za samaki nyumba nzima

Yale majiko hayataki uchafu. Yanataka mtu msafi ambaye usafi kwake ni hobby sio kazi ya lazima. Utapenda jiko hilo ila hawa wanawake tunaokutana nao miaka hii akishashiba anapiga teke sahani na bakuli anajilaza kwenye sakafu anaperuzi Instagram hapo mtoto hajamkagua kama amejisaidia unatoka zako huko na wageni unafika ndio anajikurupusha jiko chafu machakula chakula kila kona, mtoto amevunda harufu ya maziwa, jasho na mikojo ya kwenye nepi zao hizi za kisasa zinazokusanya mikojo hata masaa...

Daaaaah basi tafrani. Tunajenga hizi nyumba ila mtu unatamani ubakie pekee yako saa zingine ili ufurahie uzuri wa nyumba yako.
 
Wachache sana wanaofanya kazi za plumbing na tiles kwa ubunifu, wengi wanafanya kama kazi ya kujikimu badala ya kazi ya ubora kwa wateja wao.
 
Yale mataa taa ndo wanajitahidi?
 
Chumba cha choo chatakiwa kiwe masters pekee ili kuangalia usafi wa watoto
 
Wachache sana wanaofanya kazi za plumbing na tiles kwa ubunifu, wengi wanafanya kama kazi ya kujikimu badala ya kazi ya ubora kwa wateja wao.
Halafu bado wengi wana mifumo ya kizamani kwenye kudesign mpangilio wa bafu, vyoo na kitchen
 
Niljenga nyumba kubwa kuzidi mahitaji wa familia yangu na uwezo wangu. Sebule kukwaa, jiko kubwaaa, dinning kubwaaa, stoo kubwaa na coridor kubwa mbele na na jikoni. mwaka wa 10 sasa nyumba haina finishing ya maana.

Mbaya zaidi nikaweka chumba kimoja tu kuwa self wakati vingine vyote vinne vya kulala vikitegemea bafu moja na choo kimoja. Ni makosa ambayo sitakaa niyafanye tena nikifanikiwa kukamata fyedhaa.
 
Una maanisha nini kusema msingi wa chini au wa juu, Ninachoelewa mimi msingi wa nyumba upo chini na ndio unabeba nyumba. Au msingi hasa ulimaanisha nn?
 
Yale mataa taa ndo wanajitahidi?
Bora umenisaidia kusema. Yaani watanzania wananishangaza sana when it comes to Interior design.

Ni mwendo wa kujaza Ma-gypsum yenye konakona na Mataa taa ya rangi rangi. And they do the same thing kwenye panel ya tv (showcase)... Na wao ndio wanaona wamepatia yani!!!

Sebule/nyumba inakuwa "very busy" unnecessarily....
 
Inatakiwa iweje mkuu...tupe mfano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…