🤣🤣Nilivyouziwa sikua nagari, nikajenga nikamaliza na njia ya kuingilia na kutokea ilikuwepo kwasababu wakati wa ujenzi gari ya vifaa ilikuwa inaingia Hadi site.
Sasa nimehamia nikakaa miezi 6 nikanunua gari Alieniuzia tukaanza mgogoro mara apande miti sehemu ninayo pita mara aanzishe biashara ya tofari sehemu ninayo pita kiasi cha kubakisha kichochoro cha wapita kwa miguu.
Nikampeleka kwa mjumbe akaambiwa angoe miti yake akingoa siku chache ana panda tena, nikaona Bora niuze nikajenga sehemU salama yenye majirani wanaojielewa sio yule chawivu anaetamani kila mtu atembee kwamguu.
HakikaKutoweka wiring system ya solar! Mnaojenga saivi hili nalo mlitizame..
Unaovuka kiuno ,,fanya jaribio weka meza yenye urefu wa kiuno chako kisha weka karai fanya kama unafua ama unaosha vyombo hapo utapata kimo kizuri kwa matumizi yenu ,Urefu kiasi gani usiohitajika
Kwa nini mkuu mbona mimi napendaKujenga basement najuta sana
bati 150? Unayaweka mawili mawili au
Duh! Mimi nilifikiri ni utani kumbe kweli kuna mafundi wa hivyo? Hii ni hatari sana.Ilibakia kidogo niingie huu msala. Fundi alinitamanisha Kwa kuwa tofali za msingi zillingia nyingi sana so Kwa ndani chooni kulikuwa na shimo kubwa
ngoja tushirikiane kuifufuaNaifufua thread mafundi waumbuke
Kabisangoja tushirikiane kuifufua
Hapa waswahili wenzangu wakiona umeandika nyumba ya billion moja wanaogopa. wengi watasema hii ni chai. YET KIUHALISIA kwa mtu anayekaa Europe au North America, hiyo ni pesa inayofikika kabisa kiutafutaji. Hapa bongo hizo nyumba zipo nyingi tuu ila zinajengwa na watu ambao (wengi wao) ni wezi wa pesa za serikali.Nilitoka Ulaya nakiwa nime-save bilioni moja nikitaka nijengewe nyumba yenye ubora sawa na Ulaya. Mafundi wa Dar es Salaam ambar walikuwa wanafisiwa na watu wengi walinifanyia kazi ya hovyo kiasi kwamba maji ya moto yalikuwa hayatoki, nyumba inavuja, rangi haijapakwa vizuri. Tulikaa mwaka mmoja, tukaamua kuhama. Kwa kuwa kiwanja kilikuwa ni prime plot na ilinichukua miaka mingi kukusanya pesa za kukinunua. Sikutaka kuishi kwenye nyumba ambayo sikuwa na furaha. Nikaamua kuibomoa nyumba yote, nikakopa benki halafu nimkatafuta architect kutoka Afrika ya Kusini, nikachora ramani mpya. Nikatafuta kampuni ya ujenzi kutoka Cape Town (Wana uzoefu wa kujenga nyumba za kwenye fukwe au mija yenye joto). Nyumba mpya imenipa furaha kubwa. Somo: Mafundi na wachoraji wa ramani wetu (with all due respect) wanakosa exposure lakini wanaamini wanajua kila kitu. Tanzania tumejifungia Saną; tunahitaji kujifunza kutoka nchi nyingine. Tunahitaji kuwatia moyo watt wasafiri kwenda Afrika ya Kusini, Kenya na kwingine kote tukiwa tumefungua moyo na akili wa kutaka kujifunza. Kama unataka prime property/high end house, nakushauri uangalie njee ya mipaka ya Tanzania.
Nipo hapa ifufukengoja tushirikiane kuifufua