Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Kujenga contemporary.

Yule fundi msenge sana, alijifanya mtaalamu aliyeshindikana. Mataokeo yake mjengo mzuri halafu unavuja. Alivyo fala eti anasema labda ndugu hapo kijijini wanaroga nyumba. Nimempa laana kubwa.
Kwa hiyo mwana hivi vinapartment vyangu ni paue kwa mtindo wa zamani?
 
Fundi wako hakikisha anajua kujenga ngazi nilifumua mara 6, na gharama zote kwangu. BOQ nyingi za kiongo fanya homework yako vizuri gharama halisi huwa chini kwa zaidi ya nusu wakati fulani.

Kama unajenga kwa kujiungaunga nenda hardware mwenyewe hapa ndo eneo wenye nyumba wengi hupigwa sana
 
Though sijawahi kuwa na nyumba wala kujenga ila kosa ambalo siwezi kufanya ni kuachia upenyo wowote, nitajipanga vizuri na hela yao yote cash na nitakuwa nao site kufuatilia kila hatua huku nikiwa na nguo za kazi ikibidi kusaidiana nao kabisa.
Ndio ujenzi huo mwanawane mafundi wangese sana...hao nikukaa nao bumpe to bumper.
Cement wanaiba nankuuza kwa kilo alafu wajinga wao wanawaza kumaliza kazi tuu na sio ubora wa kazi.
 
Kujenga kighorofa.
Jameni, hii shughuli si yakitoto. Ningejenga nyumba ya chini ya vyumba viwili, ningesha hamia kitambo!
Hii kaka ili kugharimu kiasi gani kwa square metre ? Nataka kujenga kighorofa na mimi nataka kujua gharama.
 
Habari wana JF

Ni kosa gani ulilifanya kipindi unajenga na ungependa wengine wajifunze ili lisitokee kwao?
Kujenga GOBA ghorofa ambalo lina vyumba 6 , nina watoto wanne na wote wapo. chuo, wakifunga wanaenda kwao, nyumba imebaki ukiwa, tunalala vyumba vya chini na ghorofani analala dada wa kazi na kaka wa kazi.

#Vijana jengeni nyumba za kawaida, vyumba viwili tu#
 
Una watoto wako halafu wakifunga wanaenda kwao wapi?
 
Hii ya kwenda vyuoni na kurudi nyumbani wakati wa likizo, ni trailer tu. Filamu yenyewe itawajia utakapofika wakati wao wa kujitegemea. Kila mtoto atakwenda kuanzisha familia yake. Mtabaki wawili kama wakati mlipooana.
 
Mungu ni mkubwa
Mwakani lnshaallah namimi niezeke kiduku changu cha kujisitiri na wanangu.
 
kama apo unapojenga kuna nyumba kama hizo hapo kwenye picha basi hakikisha nawewe unajenga nyumba za kufanania na hizo za wenzako uliowakuta apo. hatutaki lawama bdae. usiseme hatujakuambia.
👇👇👇
 
1. Kumtafuta fundi ambaye ni ndugu yangu kwa lengo la kuokoa gharama. Aliharibu Foundation ya nyumba, alimanusura nibomoe jengo lote. Niliokoa baada ya kutafuta fundi mwingine.

2. Kujenga nyumba kubwa kinyume na uwezo.
Kujenga nyumba kubwa kuliko uwezo una define vipi hii? Utajuaje kama uko kwenye hii spot?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…