Ni kosa kuoa katika familia ya kichawi?

Ni kosa kuoa katika familia ya kichawi?

Wapendwa,KILA mtu ana Imani yake lakini pia ana Experience ya hivi vitu.
Kwa Ushauri wangu ,kama anajisikia Amani kumuoa huyo mdada Yeye Amuoe tu. Maandiko katika biblia yanasema hivi"

Ezekieli 18:20​

Ezekieli 18:20 SRUV​

Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake."
HIVYO BASI tusimhukumu huyu binti kutokana na mambo kwenye Familia Yao,Yeye kama Yeye anao Uwezo wa kujisimamia kuyakataa hayo mambo au kuendelea nayo. UKWELI MCHUNGU NI KWAMBA asilimia kubwa za Familia/koo zetu za Kiafrika,Ndani ya Mwanafamilia Mmoja au zaidi kuna mchawi. Hujapewa tu Neema ya Mafunuo kugundua kinachoendelea but UKWELI ndo huo hasahasa hizi Jamii za Wasukuma,wanyamwezi,wakinga,wahehe,Wanyaturu,wanyiramba,wakurya,wajita,wazigua,wasambaa,warangi,wapare,wamwela nk.
Angalia Amani ya Ndani ya Moyo wako! Kama unaona Pana Utulivu,huna wasiwasi wewe Muoe!
 
Hiko hivi kuna rafiki yangu mmoja amekuja kuomba ushauri.

Kampenda mwanamke wako kwenye mahusiano ya mda sasa, alipo fanya maamuzi ya kuoa wazazi wakamwambia "huyo binti kwao ni wachawi" kwamba kuna scenario mama ake huyo binti alikamatwa akiwanga, wazazi hawataki hata kusikia kuhusu huyo binti.

Mimi kwa sababu siamini uchawi wala sijawahi kumuona mchawi nimemwambia aoe tu maana mama ake anaweza kua mchawi lakini yeye sio mchawi. je nimefanya vibaya kumshauri hivyo?.

Then sisi wazazi ukimzaa mtoto sio vizuri kuanza kuingia kwenye maamuzi yake, maana wazazi wengine wanataka kuweka sheria zao hadi kwenye nyumba za watoto wake.

Mzazi mtoto anapofikisha umri mkubwa unachotakiwa ni kushauri tu.

Tawile
 
Najua sio rafiki yako ila wewe mwenyewe. Mkuu usithubutu kuoa ktk familia ya kichawi, watoto wako watachawiwa na mama mkwe utakufa masikini kwa kuhangaika na maradhi yasiyoeleweka ya mara kwa mara ya watoto wako.
Nimeshaoa Mkuu Mwaka wa 6 sasa, huyu dogo tunafanya nae kazi ofsini
 
Hiko hivi kuna rafiki yangu mmoja amekuja kuomba ushauri.

Kampenda mwanamke wako kwenye mahusiano ya mda sasa, alipo fanya maamuzi ya kuoa wazazi wakamwambia "huyo binti kwao ni wachawi" kwamba kuna scenario mama ake huyo binti alikamatwa akiwanga, wazazi hawataki hata kusikia kuhusu huyo binti.

Mimi kwa sababu siamini uchawi wala sijawahi kumuona mchawi nimemwambia aoe tu maana mama ake anaweza kua mchawi lakini yeye sio mchawi. je nimefanya vibaya kumshauri hivyo?.

Then sisi wazazi ukimzaa mtoto sio vizuri kuanza kuingia kwenye maamuzi yake, maana wazazi wengine wanataka kuweka sheria zao hadi kwenye nyumba za watoto wake.

Mzazi mtoto anapofikisha umri mkubwa unachotakiwa ni kushauri tu.
Achawi upo na wazazi wako wana akili kuliko wewe,na wameona mengi kuliko wewe,usioe huyo binti,wanawake wapo wengi sana
 
Back
Top Bottom