Wapendwa,KILA mtu ana Imani yake lakini pia ana Experience ya hivi vitu.
Kwa Ushauri wangu ,kama anajisikia Amani kumuoa huyo mdada Yeye Amuoe tu. Maandiko katika biblia yanasema hivi"
Ezekieli 18:20
Ezekieli 18:20 SRUV
Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake."
HIVYO BASI tusimhukumu huyu binti kutokana na mambo kwenye Familia Yao,Yeye kama Yeye anao Uwezo wa kujisimamia kuyakataa hayo mambo au kuendelea nayo. UKWELI MCHUNGU NI KWAMBA asilimia kubwa za Familia/koo zetu za Kiafrika,Ndani ya Mwanafamilia Mmoja au zaidi kuna mchawi. Hujapewa tu Neema ya Mafunuo kugundua kinachoendelea but UKWELI ndo huo hasahasa hizi Jamii za Wasukuma,wanyamwezi,wakinga,wahehe,Wanyaturu,wanyiramba,wakurya,wajita,wazigua,wasambaa,warangi,wapare,wamwela nk.
Angalia Amani ya Ndani ya Moyo wako! Kama unaona Pana Utulivu,huna wasiwasi wewe Muoe!