Ni kwa namna gani Julius Nyerere aliwazidi "Ujanja" wazee wa Kariakoo waliompokea kwenye siasa za Dar es Salaam?

Hivi kweli kuna kuna haja na sababu ya kuishi katika jana wakati kesho inatokudolea macho na hatuna hata maandalizi ya kuikabili? Hakuna cha kuzidiana ujanja–––kwa muktadha wowote uliokusudia––––bali hali halisi ya wakati ule. Nyerere alikuwa msomi kuliko wale wazee hasa kama tutatumia mizania ya kikoloni kuwa msomi lazima awe na shahada. Hivyo, Nyerere hakuwazidi ujanja wale wazee wala hapakuna na sababu wala. mazingira ya kufanya hivyo bali kutimiza lengo la kuikomboa nchi. Ni mawazo finyu kudhani kuwa Nyerere aliwazidi ujanja wenyeji wake kana kwamba walikuwa mafala. Tuache kuwadhalillisha wazee wetu bali kushukuru kwa kazi pevu waliyofanya. Yaliiyopita? Basi tugange yajayo badala ya kupoteza muda ku-invent the wheel. Ni ushauri tu. Mzee mwenzangu Muddy Said namkubali japo si kwa kila jambo.
 
Father...
Imetokea kuwa waliounda African Association 1929 kisha Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933 kisha TANU 1954 ni wazee wangu.

Wengine kwa nasaba na wengine kwa ujamaa.

Historia ya uhuru ilipokuja kuandika hawa wazee wangu hawakuwamo ndani ya historia hiyo.

Kwa kuhofia kuwa historia hii itapotea na nchi itakuwa na historia siyo ndiyo nikaamua kuandika historia hii.

Bahati mbaya wale ambao wala hawahusiki na historia ya wazee wangu wakajitokeza kupinga historia hii.

Hili limenistaajabisha sana.

Vipi mtu atoke atokako aniambie mimi kuwa historia ya babu yangu Salum Abdallah si sawa ila historia yake yeye ya uhuru ndiyo iliyo sawa.

Hii ndiyo sababu niko hapa natetea historia yangu.
 
Utakuwa una kichaa fulani.
Hizi ni takataka.
 
Kalamu,
Nimekusikia.
Muda wote unaandika maneno hayo.

Mimi nawasikiliza na wasomaji wangu wengine.
Wao hawaoni hivyo.


Apollo Theatre
Harlem New York​
Takataka.

Ngoja nizungumze na wasomaji, siyo wasomaji wako kama unavyoodai ikiwa ni utapeli ule ule unaokusumbua.

Msomaji, inanilazimu nieleze kwa nini nipo hapa. Usishangae kuona ninayoandika dhidi ya uhuni wa huyu mzee.

Sikubaliani na lolote analosimamia,

Sababu inayofanya niendelee kuwepo hapa niliahidi kwa dhati kabisa, wakati wowote akijibu nilichoandika, hiyo ni kunikaribisha nije na kumpa maneno yale yale niliyompa toka mwanzo, kwamba anayojaza humu, tena kwa kurudiarudia ni TAKATAKA.

Kwa hiyo, uwepo wangu hapa, na ninachoandika hapa ni kutimiza yale niliyoahidi kwa huyu mzee.

Naomba uelewe, bila kujali wewe unasimamia wapi kuhusu maandishi yake, sitaacha kumjibu kila mara anapojibu chochote nilichoandika hapa.

Mzee, kwa sababu zake kaona hawezi kukufikishia ujumbe anaotaka kukufikishia bila kupitia kwa jina langu. Nami nipo tayari kabisa kumpa fursa hiyo, kama ndiyo njia anayoona inafaa kukufikishia wewe takataka zake.

Kwa hiyo, amua mwenyewe utakachotaka kuamua.
 
Kalamu,
Hakuna tatizo.
Tuendelee na mjadala.

Mimi nitaweka hapa kitabu changu chote wasomaji wetu In Shaa Allah wasome.

Nitaweka pia picha kama zinavyosuhubiana na yaliyoko katika kurasa.

Sikupata kufanya kitu kama hiki hapo nyuma.

Huu ni mwaka wa 25 toka kitabu kuchapwa London mwaka wa 1998.

Hadi leo kitabu kimechapwa mara nne.

Hii haijapata kutokea naelezwa na wataalamu.

Nakaribisha maswali kutoka kwa wasomaji.
 
Takataka kama kawaida yako.

Kazi yangu ni nyepesi sana.
 
Kalamu,
Mimi sikutakii uzito katika mjadala huu.
Natimiza wajibu wangu.
Nipo hapa kwa mwaliko wa mzee Mohamed Said.

Anahitaji msaada wangu kumkumbusha mara kwa mara kwamba uandishi wake ni talkataka na yote anayodai katika uandishi huo ni matokeo ya kipaji alicho nacho, yaani utapeli wa kutisha.

Nitaendelea kumfanyia kazi hiyo, hadi hapo atakaporidhika mwenyewe.
 
MAISHA NA NYAKATI ZA ABDULWAHID SYKES
(1924 – 1968)
1
SHUKRANI
Ninatoa shukrani kwa waasisi walioleta mabadiliko ya siasa katika sehemu za kusini ya Tanganyika, Said Alley Mwalimu na marehemu Mohamed Ali Abdallah ‘’Makarios’’ wote wawili wanatoka Mikindani; na kwa Salum Mpunga na Yusufu Chembera wa Lindi wote hawa sasa ni marehemu.

Watu hawa wamenisaidia sana kwa kunieleza maisha yao katika siasa wakati wa ukoloni katika majimbo ya kusini; na kwa Tewa Said Tewa, Dossa Aziz, Zuberi Mtemvu na Sheikh Haidar Mwinyimvua kutoka Dar es Salaam halikadhalika wote hawa sasa ni marehemu.

Natoa shukuruni kwa marehemu Yusuf Olotu maarufu kwa jina la Yusuf Ngozi wa Moshi; Mohamed Kajembe, Rashid Sembe na Mmaka Omar wote hawa kutoka Tanga na wote sasa ni marehemu, kwa kunipa maelezo ambayo si wengi wanayajua kuhusu hali ilivyokuwa wakati wa ukoloni.

Ninatoa shukurani vilevile kwa Omar Suleiman, Haruna Taratibu na kwa marehemu Hassan Suleiman, kiongozi shupavu aliyeishi kati ya Vita Kuu mbili za dunia.

Vilevile nilipata bahati ya kuongea na marehemu Germano Pacha, katibu wa mwisho wa TAA Jimbo la Magharibi na muasisi wa TANU.

Pacha alinifunulia jinsi walivyounda TANU.

Halikadhalika natoa shukurani kwa marehemu Rashid Mussa ambae katika mazungumzo yetu, yeye bila kufahamu kuwa mimi ni mjukuu wa Salum Abdallah Popo alinieleza habari za babu yangu wakati anaanza siasa na jinsi alivyoongoza mgomo wa kwanza wa Tanganyika nzima pale Tabora mwaka 1947.

Napenda kutoa shukrani maalum kwa Bilal Rehani Waikela, muungwana wa Kimanyema na Muislamu wa kweli.

Waikela akiwa na umri wa miaka ishirini na tano mwaka 1955, alikuwa mmoja wa waasisi wa TANU mjini Tabora.

Waikela alinieleza jinsi Waislam kwa umoja wao walivyomuunga mkono Julius Nyerere na harakati za uhuru.

Vilevile alinieleza kwa muhtasari siku zake kizuizini pamoja na babu yangu Salum Abdallah katika gereza la Uyui, Tabora kwa kile kilichoitwa kosa la ‘’kuchanganya dini na siasa.’’

Nina deni kubwa kwake kwa kunipa picha za wakati ule na nyaraka zake binafsi juu ya ‘’mgogoro,’’ wa EAMWS uliozushwa mara baada ya Tanganyika kupata uhuru wake mwaka wa 1961.

Natoa shukrani kwa Waikela kwa kunitia hima na kunipa moyo kuandika kitabu hiki.

Waikela tofauti na watu wengine waliozungumza na mimi aliniruhusu pia kumnukuu kwa jina bila ya woga wowote.

Alifurahi kuona kwamba historia ya kweli ilikuwa inaandikwa na habari alizonieleza zitakuja kutumika katika kuhifadhi historia ya nchi yetu kwa faida ya vizazi vijavyo.

Vilevile Waikela alinikutanisha na wazalendo wengine kama Mohamed Mangiringi, marehemu Ramadhani Singo na wengineo ambao nilizungumzanao kwa kirefu.

Itaendelea In Shaa Allah…

Phoenix Publishers
Nairobi 2002​
 
Hata Babu yangu Mzee Tambaza pia alisahaulika, lkn ukifuatilia historia za harakati za Uhuru kwa Dar es salaam! ambako vugu vugu lilikuwa juu kiasi ukitofautisha na maeneo mengine, wanadai Kambarage aliwazidi ujanja Babu zetu kwa ulaghai wa Kuunda Serikali kwa usawa wa nusu kwa Nusu, akimaanisha Waislam na Wakristo, lkn inasemekana baada ya Uhuru kupatikana akawageuka na kuwasaliti, kiasi cha Mzee wetu wa pale Ilala Suleiman Taqadiri kuitwa Suleiman Mtakadini[emoji24][emoji24], nasikia mzee Taqadir alikuwa amejielekeza sana kwa Mungu wake na akawa anasali ili Mungu amchukue asije shuhudia hayo ya baadae! Mungu alipokea dua yake na akaaga Dunia.

Mwisho: Kambarage alikuwa Mdini na aliwatelekeza na kuwasaliti wazee wetu akiwemo na Babu yangu Mzee Tambaza wa pale Upanga, cha kushukuru tumeambulia kuishi upanga tukiwa ndio mafukara pekee kwa maeneo yale.

NAOMBA KUWASILISHA.
 
Nimeshindwa kujua ni hoja gani hasa iliyo nyuma ya uzi huu. Mwandishi wa uzi anataka kutupa ujumbe gani? Ni la maana lipi Great Thinkers wa jamvi hili watatoka lao kwa kutafakari uzi huu?
 
Nimeshindwa kujua ni hoja gani hasa iliyo nyuma ya uzi huu. Mwandishi wa uzi anataka kutupa ujumbe gani? Ni la maana lipi Great Thinkers wa jamvi hili watatoka lao kwa kutafakari uzi huu?
Ng'wa....
Naanza kuweka ''serialisation'' ya kitabu changu, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,'' Minerva Press, London 1998.

Hapa naweka tafasiri ya Kiswahili.

Nataka watu wasome bure historia hii ambayo kama anuani ya kitabu inavyoonyesha ni ''Untold Story.''

Nitaweka sehemu ya mwisho ya ''Shukrani,'' labda itakusaidia kuelewa ujumbe niliokusudia.

Naamini Great Thinkers watakuja na kitu ingawa itakuwa tumechelewa sana kwani ni miaka 25 sasa toka kitabu kitoke.

Wataalamu wa African History: John Iliffe, Jonathon Glassman na James Brennan walifanya ''book review'' na zote zikachapwa katika Cambridge Journal of African History.
 
Takataka toka kwenye mlima wa taka.
 
Takataka toka kwenye mlima wa taka.
Kalamu,

MAISHA NA NYAKATI ZA ABDULWAHID KLEIST SYKES
(1924 – 1968)

2

Kazi hii isingewezekana kama isingekuwa kwa msaada wa hali na mali nilioupata toka kwa Ally Sykes.

Ally Sykes alinipa wasaa wa kuzungumzanae kila nilipotaka, akanieleza madhila ya ukoloni pamoja na kuwa ni mtu wa shughuli nyingi.

Yeye hivi sasa anaendesha biashara yake toka ofisi yake iliyoko katikati ya mji wa Dar es Salaam.

Aliniruhusu nisome majalada yake binafsi, barua zake, shajara na kumbukumbu nyinginezo za ukoo wa Sykes.

Ally Sykes alinifahamisha kuwa kumbukumbu hizi zilikuwa ndani ya sefu ambayo haikupatwa kufunguliwa kwa zaidi ya miaka therathini.

Nikiyapitia majalada yake nilishangazwa na utaratibu wa Ally Sykes wa kupanga kila kitu na kila kipande cha habari mahali pake hata kingekuwa kidogo namna gani wakati ule wa harakati.

Ally Sykes ana barua ya mwaka 1954 iliyoandikwa kwa penseli kutoka kwa Zuberi Mtemvu kwenda kwake akimtaarifu juu ya mazungumzo aliyokuwanayo (Mtemvu) na Nyerere kuhusu yeye na TANU; stakabadhi ya hundi ya posta toka kwa Ally Sykes kwenda kwa Japhet Kirilo wakati wa Mgogoro wa Ardhi ya Wameru; nakala ya barua isiyokuwa na tarehe kutoka TAA kwenda kwa Malkia Elizabeth iliyotiwa saini na viongozi wote wa TAA: Rais Julius Nyerere, Makamu wa Rais Abdulwahid Sykes, Katibu Mkuu Dome Okochi, Naibu Katibu Dossa Aziz, Mweka Hazina John Rupia, Naibu Mweka Hazina Ally Sykes ikimpongeza Malkia kwa kutawazwa; barua ya mwaka 1952 toka kwa Rashid Mfaume Kawawa kutoka Bukoba kwenda kwa Ally Sykes ikimfahamisha juu ya hali ya siasa katika Kanda ya Ziwa; barua ya mwaka 1963 toka kwa Lady Judith Listowel, Kenneth Kaunda, Julius Nyerere, Kasela Bantu, Chifu Thomas Marealle ...orodha haina mwisho.

Baadaye nilipofanya utafiti kuhusu maisha ya baba yake, Kleist Sykes, nilikuja kufahamu kwamba tabia hii ilirithiwa kutoka kwa baba yake ambae alikuwa akiweka ndani ya jalada kila kipande cha karatasi kilichokuwa na habari iliyostahili kukumbukwa.

Ni jambo la kuhuzunisha kwamba sikuweza kupewa shajara za Abdulwahid ambazo nilielezwa kwamba baadhi ziko katika hati-mkato na hadi leo hazijafasiriwa.

Shajara hizi nimezioana kwa macho yangu lakini kwa kukosa idhini sikuweza kuzifungua na kuzisoma.

Vilevile sikuweza kupata kumbukumbu halisi za Vita Kuu ya Kwanza zilizoandikwa na Kleist Sykes kwa mkono wake mwenyewe.

Hapana shaka yoyote kwamba nyaraka hizi ni hazina zenye thamani isiyo na mfano wake.

Ni matumaini yangu kwamba siku moja nchi yetu itakubali na kuthamini mchango wa Abdulwahid katika taifa la Tanzania na nyaraka hizi kama kielelezo cha harakati dhidi ya ukoloni, zitakubalika na zitawekwa chini ya hifadhi ya Nyaraka za Taifa kwa faida ya vizazi vijavyo.

Kwa miaka kadhaa nimekuwa na mazungumzo na watu mbalimbali katika ukoo wa Sykes na nimeweza kupata mambo mengi muhimu kutokana na mazungumzo yetu ya kawaida tu.

Matokeo ya yote haya ni ile yakini kuwa hii ni simulizi sahihi ya maisha na nyakati za Abdulwahid Sykes; na wazalendo wengine waliosahauliwa ambao taifa letu, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Julius Nyerere wana deni kubwa kwao kwa namna moja au nyingine.

Ninapenda kuwashukuru wale wote waliokubali kuwahojiwa nami lakini wameomba nistiri majina yao.

Na kwa wale waliokataa kuzungumza nami kuhusu somo hili si kwa ubaya bali kwa hofu, na kwa wachapaji walioogopa kuchapisha kitabu hiki na vilevile kwa wale walioona bora kukaa kimya, lazima nikubali, kwamba hao wote kwa ujumla wao na kwa namna yao ya ajabu wamechangia katika kufanikisha kitabu hiki.

Mwisho napenda kutoa shukurani maalum kwa rafiki yangu Faraj Abdallah Tamim ambaye fikra na mawazo yake yameingiliana sana na yangu katika kazi hii kiasi kwamba nashindwa kupambanua fikra zake kutoka zangu.

Naweza kupambanua fikra zake toka zangu pale tu ninaposoma na kuona katika maandishi yangu mpangilio wa mawazo na fikra kwa ustadi.

Wanaomfahamu Tamim wanakijua kipaji chake cha mawazo usiyoweza kuyalinganisha na yangu kutokana na ufasaha na mtiririko wa maneno ambao umo ndani ya kitabu hiki na katika rejea zangu neno kwa neno.

Kisha namshukuru rafiki yangu mwema na jirani yangu Saeed Bamumin.

Yeye alinisabilia kompyuta na nyumba yake ambayo niliifanya mahali pa kujificha ili nifanye kazi katika hatua za mwisho za kuandika kitabu hiki.

Nina deni kubwa kwake kwa ukarimu na hisani yake juu yangu.

Vilevile nawashukuru wale ambao kwa miaka mingi wamekuwa karibu nami na kamwe hawakuchoka kusikiliza ‘’mihadhara’’ yangu juu ya shujaa wangu, marehemu Abdulwahid Sykes na wazalendo wengine.

Katu haikuwa nia yangu kuandika kitabu na wengi katika wale waliopata kuzungumza nami kwa faragha watashangaa kuona kwamba baadhi ya mazungumzo yao na mimi yapo hadharani kwenye kitabu hiki.

Ninaamini kuwa nimeyatumia mazungumzo yetu kwa jambo lenye manufaa na kwa ajili hii basi hawatakereka.

Dar es Salaam.
Ijumaa 11/8/1995.

Bilali Rehani Waikela

Salum Mpunga

Yusuf Chmbera




 
Mzee Mohamed Said, taka zinaendelea kumiminika hapa JF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…