Hizi takataka kama kasi yake ndiyo hii itakuchukua mwaka mzima, na pengine itabidi nifanye utaratibu wa ku'automate' majibu yangu.
Ngoja nitafute njia sahihi ya kukufanyia hilo. Sitakuacha, tupo pamoja sana.
Kalamu,
MAISHA NA NYAKATI ZA ABDULWAHID SYKES (1924 – 1968)
Utangulizi 3
Wakati huo mjini Dar es walikuwako Wazulu wanne maarufu kutoka Afrika ya Kusini; Kleist Sykes.
Hili ni jina alilosajiliwa na Wajerumani alipozaliwa.
Udogoni akijulikana kama Kleist Plantan, hili jina la Plantan alilipata kutoka kwa Afande Plantan, mlezi wake baada ya kifo cha baba yake Sykes Mbuwane.
Affande lilikuwa ni cheo katika jeshi la Waturuki.
Huenda liliingizwa ndani ya majeshi ya Wajerumani wakati wa vita Kuu Vya Kwanza ya Dunia wakati Uturuki na Ujerumani zilipokuwa washirika katika vita hivyo).
Kwa kweli jina la Kizulu la Affande Plantan lilikuwa Shangaan.
Hili jina lilitokana na kijiji Inhambane Msumbiji, walikotoka Sykes Mbuwane na Affande Plantan.
Wajerumani waliwaajiri Wazulu 400 kutoka Msumbiji kama mamluki na kujanao Tanganyika ili wapigane na Abushiri na Chifu Mkwawa.
Pamoja na Kleist katika mji wa wa Dar es Salaam walikuwepo ndugu wa mbali watatu, Mwalimu Thomas Plantan, (hilo jina Mwalimu alipewa kwa sababu alikuwa Mwalimu wa shule), Schneider Abdillah Plantan na Ramadhani Mashado Plantan.
Hawa Wazulu waliweza kutambulika kwa urahisi kutokana na majina yao ya Kikristo ingawa wao wenyewe walikuwa Waislam.
Majina hayo yalikuwa na mchanganyiko wa majina ya Kijerumani, Kireno na Kiingereza; kama vilevile Kleist na Schneider ni majina ya Kijerumani; Mashado ambalo ni jina la Kireno na Thomas ni la Kiingereza.
Wote hao, Kleist, Mwalimu Thomas, Schneider na Mashado baadaye walifanya kazi kubwa katika kupiga vita ukoloni na katika kuupeleka mbele Uislamu, kabla na baada ya uhuru.
Bahati mbaya majina haya ya Kiislamu ya wazalendo hawa hayakujitokeza sana badala yake walijulikana zaidi kwa majina yao ya Kizungu waliyoyarithi kutoka Wajerumani kupitia wazee wao wa Kizulu.
Vilevile kulikuwa na idadi kubwa kidogo ya Wamanyema mashuhuri, kama vilevile Mzee bin Sudi (ambaye alikuwa ndiyo kiongozi wa Wamanyema mjini Dar es Salaam), Nassoro Kiruka aliyekuwa mtu tajiri mwenye majumba ya kupangisha na mtu wa kujipendekeza sana kwa Waingereza; na Iddi Tosiri ambaye pamoja na Kleist na Ali Jumbe Kiron a Waislam wengine walijenga Al Jamiatul Islamiyya Muslim School katika miaka ya katikati ya 1930, shule ambayo baba yangu na wengi wa marika yake walipata elimu yao ya dini na ya dunia.
Halikadhalika alikuwepo Erika Fiah, Mganda maarufu aliyeamua kulowea Tanganyika baada ya Vita Vikuu vya Kwanza.
Hawa ‘’wageni’’ ikiwa tunaweza kuwaita hivyo, waliacha athari kubwa katika siasa za mji wa Dar es Salaam.
Nilipokua napata makamo nilikuja kuwajua watu hawa na juu ya matukio yaliyotokea mjini Dar es Salaam hata kabla sijazaliwa katika mwaka 1952.
Baba yangu, ndugu na jamaa na watu wa Dar es Salaam walikuwa ndiyo walionioeleza kila kitu nilichokujakukifahamu kuhusu mji na historia yake.
Ninakumbuka siku moja miaka mingi iliyopita, nilikuwa ninatazama picha ya waasisi wa TANU.
Wakati huo ilikuwani desturi wakati wa kuadhimisha kuasisi kwa kwa TANU mnamo Julai 7, 1954, inapofika tarehe hiyo kila mwaka ilikuwa ni sikukuu.
Ilikuwa kawaida kuchapisha katika magazeti ya serikali na chama, picha ya pamoja ya wale waasisi kumi na saba iliyopigwa mbele ya ofisi ya TAA.
Mmoja wa baba zangu, Abdallah Mohamed aliyefahamiana na Abdulwahid kwa miaka mingi na wakiishi jirani alitazama picha ya Abdulwahid kisha akasema, ‘’Huyu ndiye mtu aliyeasisi chama cha TANU na angekuwa rais wa nchi hii, kama angetaka.’’
Vilevile baba yangu aliniambia, mara yake ya kwanza kumuona Julius Nyerere ilikuwa mwaka 1952 nyumbani kwa Abdulwahid Mtaa wa Aggrey na Stanley.
Wote wawili baba yangu, na Abduwahid walikuwa vijana umri wao miaka 28.
Baba yangu alikuwa mbali sana na siasa.
Ally Sykes alipata kuniambia kuwa alijaribu mara nyingi sana kutaka kumwingiza baba yangu katika harakati za TANU lakini alishindwa.
Kitu kimoja tu kilichomuunganisha na marehemu Abdulwahid ilikuwa ni utanashati na kwa enzi zile wao ndiyo walikuwa vijana maarufu wa mjini.
Walichanganya utamaduni wa Kiswahili na ule wa Ulaya na sehemu nyingine za dunia. Walisikiliza muziki wa Edmund Ross, Victor Silvester, Nat King Cole, Louis Amstrong, Alma Cogan, Bing Crosby na wanamuziki wengine.
Wakati mwingine waliwasikiliza waimbaji wa Kiarabu, Um Kulthum, Mohammed Abdulwahab, Farid Atrash, Abdul Halim Hafidh, Feiruz na Sabah.
Santuri za baba yangu za muziki wa jazz zimedumu kwa muda mrefu zaidi ya miaka ya arobaini.
Familia yangu ilifahamiana na Dome Budohi, mmoja wa wanaharakati kutoka Kenya.
Wakati ule wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika alikuwa akiishi Dar es Salaam.
Budohi alikuwa mmoja wa wazalendo walioasisi TANU na kadi yake ya uanachama ni nambari sita aliyopewa Julai 1954.
Mwaka 1955 alikamatwa na serikali ya kikoloni kwa tuhuma ya kuwa mmoja wa askari wa Mau Mau harakati za wazalendo takriban wengi wao wakulima wadogo waliokuwa wakipigana na ukoloni wa Waingereza nchini Kenya.
Ninazo kumbukumbu nyingi za utoto nikimtembelea Budohi Kituo Cha Kati cha Polisi.
Hivi sasa jengo hilo ni Makao Makuu ya Shirika la Reli la Tanzania.
Wakati huo mimi nilikuwa mtoto, si zaidi ya miaka minne hivi.
Jambo la kwanza ninalokumbuka kuhusu Budohi ni kuwa kila mara tulipokwenda kumtembelea tulimkuta anasoma gazeti.
Baadae Budohi alihamishiwa Kenya na aliwekwa kizuizini katika kisiwa cha Lamu.
Alipofunguliwa toka kizuizini mwaka wa 1963 miezi michache kabla ya uhuru wa Kenya, Budohi alikwenda Uganda na akaajiriwa na gazeti la Uganda Argus.
Hivi sasa ninaelewa kwa nini siku zile kila mara nilikuwa namkuta amezama ndani ya gazeti kila tulipokwenda kumtembelea pale rumande mjini Dar es Salaam.
Niliweza kwa msaada wa rafiki yake Maxwell aliyelowea Tanganyika, kumpata Budohi mjini Nairobi mwaka 1972.
Nilimtembelea mjini Nairobi wakati huo alikuwa akiishi Ruiru maili chache kutoka Nairobi mjini.
Budohi alikuwa ametundika picha ya Nat King Cole sebuleni kwake. Mwaka 1974 nilimtembelea tena, safari hii akiishi Ngei Estate.
Budohi alikuja kuwa mtu wa kwanza kabisa kunipa habari kuhusu historia ya harakati za Tanganyika dhidi ya ukoloni wa Waingereza.
Hata hivyo wakati ule nilikuwa bado sijapata hamu wala kuwa na hamu ya kuandika kitabu kuhusu uhuru wa Tanganyika.
Katika hali kama hii vipi mimi nisijione kuwa ni sehemu ya historia hiyo?
Katika hali kama hii vipi nitamudu kukaa kimya wakati historia ya uongo ndiyo inatoenziwa na ile ya kweli inafichwa?
Nilipoanza kupitia vitabu na maandiko mengine juu ya historia ya TANU nilistaajabu kuona kuwa hakuna hata mmoja kati ya watu mashuhuri niliowajua ambao walihusika na harakati za uhuru walikuwa wametajwa katika vitabu hivyo.
Nilipigwa na butwaa nipogundua kuwa hata Abdulwahid Sykes, mzalendo ambae baba yangu akimtaja sana katika historia ya TANU hakuwa ametajwa popote na badala yake kila mahali lilikuwa jina na Julius Nyerere peke yake.
Thomas Plantan 1964
Kleist Sykes 1942
Mwandishi na Dome Okochi Budohi Nairobi 1972
Kadi yake ya TANU No. 6