Bwana Kalamu, ungetupa historia unayoifahamu kwa upande wako, ili sisi wasomaji wengine tufaidike.Taka ni zako siyo za hao wenye picha.
kuishia kusema "takataka" unatunyima haki kuujuwa ukweli.
Tafadhali bwana Kalamu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bwana Kalamu, ungetupa historia unayoifahamu kwa upande wako, ili sisi wasomaji wengine tufaidike.Taka ni zako siyo za hao wenye picha.
Sina neno na wewe.Bwana Kalamu, ungetupa historia unayoifahamu kwa upande wako, ili sisi wasomaji wengine tufaidike.
kuishia kusema "takataka" unatunyima haki kuujuwa ukweli.
Tafadhali bwana Kalamu.
'Kalamu,Taka ni zako siyo za hao wenye picha.
Spidi yako ya uzoaji wa hizi taka ni hafifu mno. Zilete haraka ili tupate muda wa kufanya mambo mengine.'Kalamu,
''...barua isiyokuwa na tarehe kutoka TAA kwenda kwa Malkia Elizabeth iliyotiwa saini na viongozi wote wa TAA: Rais Julius Nyerere, Makamu wa Rais Abdulwahid Sykes, Katibu Mkuu Dome Okochi, Naibu Katibu Dossa Aziz, Mweka Hazina John Rupia, Naibu Mweka Hazina Ally Sykes ikimpongeza Malkia kwa kutawazwa; barua ya mwaka 1952 toka kwa Rashid Mfaume Kawawa kutoka Bukoba kwenda kwa Ally Sykes ikimfahamisha juu ya hali ya siasa katika Kanda ya Ziwa; barua ya mwaka 1963 toka kwa Lady Judith Listowel, Kenneth Kaunda, Julius Nyerere, Kasela Bantu, Chifu Thomas Marealle ...orodha haina mwisho.
Pesaa,Bwana Kalamu, ungetupa historia unayoifahamu kwa upande wako, ili sisi wasomaji wengine tufaidike.
kuishia kusema "takataka" unatunyima haki kuujuwa ukweli.
Tafadhali bwana Kalamu.
Okw...Shida ya MS hayuko objective. Ana upande
Sina neno na wewe.
Nipo hapa kwa minajiri ya Mzee Mohamed Said.
Asante sana kwa kunivumilia.
Kalamu,Spidi yako ya uzoaji wa hizi taka ni hafifu mno. Zilete haraka ili tupate muda wa kufanya mambo mengine.
Fanya haraka nahizi taka zako bwana.Kalamu,
DibajiUsomi makini unadai kuwa kila mtafiti anapashwa kuwa hadhiri na kile ambacho wenzake wameandika kuhusu utafiti ambao yeye anataka kufanya.
Jambo hili zito busara yake ni kutia hima kwa watafiti wapya kuanzia utafiti pale wenzake walipoachia.
Ni siri iliyo wazi kuwa jambo hili azizi linafuatwa katika kulikwepa kuliko kulitimiza.
Katika kitabu hiki mwandishi amejitokeza kama msomi makini.
Kitabu hiki, ‘’Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968) Kisa Kilichofichwa Kisifahamike Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza Katika Tanganyika,’’ kwa hakika ni kazi ya kupigiwa mfano.
Inajitokeza kuwa Mohamed Said amefanya juhudi za makusudi kupata na kufahamu utafiti uliokwishafanywa katika historia ya siasa Tanzania.
Umuhimu zaidi wa kazi hii ni kuwa mwandishi alikuwa na bahati maalum ya kupata habari muhimu kabisa kutoka katika majalada, barua, shajara na kumbukumbu za ukoo wa Sykes (ambao unahesabika kama ndiyo chimbuko la siasa Tanganyika katika kupambana na ukoloni wa Waingereza), kumbukumbu ambazo watafiti waliopita hawakubahatika kuzipata.
Kwa ajili hii basi matokeo ya utafiti wao ulifikiwa bila na kuwa na kumbukumbu za kuaminika.
Hata hivyo Mohamed Said anasema kuwa makosa haya hayakutokea kwa bahati mbaya, la hasha, huo ulikuwa mpango maalum wa kufifilisha historia ya kweli ili isifahamike.
Mwandishi ana ushahidi wa kushangaza kuwa historia rasmi ya Tanzania imejaa makosa ya makusudi na siyo yanatokana na kutojua.
Katika kitabu hiki Mohamed Said anatoa uchambuzi wa makosa ya historia pamoja na usaliti uliopitika.
Hii ni kazi ya kishujaa na ya ukweli kuhusu matatizo ya kijamii yatokanayo na historia kama Tanzania inavyokumbwa nayo, kitabu hiki huenda kikaleta mjadala wa wasomi kuanzisha ubishani mkubwa.
Ikiwa mtu anakubaliana na mtazamo wa mwandishi au la bado ni wazi kuwa watafiti wa baadae watakuta hazina yenye thamani kubwa katika kitabu hiki hasa katika rejea ambazo kabla yake zilikuwa hazifahamiki.
Vilevile ifahamike kuwa juu ya kuwa mwandishi amezama sana katika somo lakehili bado uandishi wake ni mwepesi na wa kuvutia.
Dr Hamza Mustafa Njonzi
Mwenyekiti, Idara ya Fasihi
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
![]()
Prof. Hamza Mustafa Njozi na Mwandishi
Kenyatta University, Nairobi
Kalamu,Fanya haraka nahizi taka zako bwana.
Weka mbilimbili au zaidi twende haraka
bado spidi hairidhishi jinsi unavyoziweka hizi takataka humu jamvini.Kalamu,
MAISHA NA NYAKATI ZA ABDULWAHID KLEIST SYKES
(1924 – 1968)
Utangulizi 1
Kazi hii ni matokeo ya mambo niliyoyapata kuyafahamu mimi mwenyewe kutokana na masimulizi niliyopokea kutoka kwa watu wengi, kuhusu mambo yalitokea Dar es Salaam.
Nikiwa nimezaliwa Dar es Salaam ambako ndipo kulipokuwa na chimbuko la harakati za kupinga ukoloni Tanganyika, kama Tanzania ilivyokuwa ikijulikana wakati huo, nina kumbukumbu nyingi za watu mashuhuri na matukio yaliyotokea.
Kauli za watu waliyoyaona mambo kwa macho yao wenyewe yakitendeka zilikuza maarifa yangu.
Nilipokuwa mwanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mahali ambapo utafiti wa kitabu hiki ulipoanza, niligundua kuwa mambo yaliyokuwa yakifundishwa kuhusu harakati za kudai uhuru wa Tanganyika hayakulingana na ukweli kama niliyokuwa nikiujua.
Kidogo kidogo nikatambua kuwa kulikuwa na jaribio la makusudi kabisa la kufifilisha kazi kubwa iliyofanywa na baadhi ya wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika.
Nikiwa kijana mdogo, baba yangu Said Salum Abdallah alikuwa akinisimulia habari za ushujaa wa babu yake, Samitungo Mwekapopo.
Samitungo alivuka mpaka toka Belgian Congo na kuingia Tanganyika kupitia sehemu ya kaskazini ya ziwa Tanganyika katika miaka ya mwishoni 1800.
Wakati huo Tanganyika ilikuwa chini ya utawala wa Wajerumani. Wajerumani walikuwa wamewashinda Waarabu chini ya Abushir bin Salim Al Harith katika ukanda wa pwani na machifu kama Mkwawa waliokuwa wakitawala bara.
Samitungo alipata kupigana na chui, akamuua na yeye akanusurika kuuwawa.
Hata hivyo yule chui alimtia kilema cha maisha. Babu yangu Salum Abdallah Popo alizaliwa Shirati huko Musoma ambako baba yake Samitungo alikuwa askari katika Boma la Wajerumani.
Nasikia kuwa boma hilo lingalipo hadi leo.
Babu yangu Salum Abdallah alikuwa mtu jasiri kama baba yake.
Ingawa vitabu vya historia havimtaji, lakini babu yangu yeye ndiye aliyeongoza mgomo wa kwanza wa Tanganyika mwaka 1947 dhidi ya Waingereza katika majimbo ya kati ya Tanganyika.
Babu yangu Salum Abdallah alikuwa mmoja wa wazalendo wa kwanza wakati wa ukoloni kuanzisha harakati za vyama vya wafanyakazi.
Vilevile alikuwa kati ya watu wa mwanzo kuiunga mkono Tanganyika African National Union (TANU), chama cha kizalendo kilichopigania na kunyakua uhuru kutoka kwa Waingereza mwaka 1961.
bado spidi hairidhishi jinsi unavyoziweka hizi takataka humu jamvini.
Ongeza spidi zaidi.
Soph...Huyu mzee ashavuruga thread ya mtu na habari zake za kleist [emoji706][emoji1005]
Hizi takataka kama kasi yake ndiyo hii itakuchukua mwaka mzima, na pengine itabidi nifanye utaratibu wa ku'automate' majibu yangu.MAISHA NA NYAKATI ZA ABDULWAHID SYKES
(1924 – 1968)
Utangulizi 2
Babu yangu alipendelea kuitwa kwa jina lake la utani ‘’Kapipi,’’ ambapo neno la Kimanyema lililokuwa na maana ‘’Mweusi.’’
Baadaye alipostaafu kazi na akiwa na mtu wa kujiweza kidogo na akiishi Tabora, wale waliokuwa karibu naye walimwita kwa jina la utani ‘’Gulamsojo,’’ likimaanisha ‘’Bwana.’’
Lakini jina hili hawakuthubutu kulitamka mbele yake kwa sababu babu yangu alijulikana kuwa hakuwa mtu wa maskahara hasa kwa yale mambo yasiyompendeza.
TAA ilipofanya mkutano wa siri katika shule moja pale Tabora ili kuchangisha fedha kumwezesha katibu wa TAA Jimbo la Magharibi Germano Pacha kusafiri Dar es Salaam kuhudhuria mkutano mkuu wa kuanzishwa TANU Julai mwaka 1954 mchango mkubwa kupita yote ilikuwa shilingi ishirini.
Fedha hizi alitoa babu yangu.
Mkutano huu ulihudhuriwa na watu maarufu wa Tabora pamoja na baadhi ya waalimu kama Abubakar Mwilima, Harub Said na George Magembe.
Hawa walikuja kuwa watu muhimu sana wakati wa harakati za kudai uhuru.
Hata hivyo, babu yangu alitupana mkono na Julius Nyerere kama wengi walivyofanya, na alitiwa kizuizini na serikali mara baada ya uhuru chini ya Preventive Detention Act ya mwaka 1962.
Mara nyingi nilipodadisi baadhi ya mambo katika historia ya TANU jibu nililopata kutoka kwa waalimu wangu na wanafunzi wenzangu lilikuwa, ni ‘’Lete ushahidi wako.’’
Nilipomtaja baba yangu kuwa ndiyo shahidi wangu, wenzangu walinifanya kichekesho na kuniona mpumbavu.
Baba yangu Said Salum alizaliwa Tabora lakini aliishi maisha yake yote ya utoto na ujana wake Dar es Salaam.
Kupitia kwake nilijifunza mambo mengi kuhusu mji wenyewe na kuhusu maisha yake ya utoto akiwa na rafiki zake, Abdulwahid Sykes na mdogo wake Ally.
Waliingizwa shule pamoja katika Al Jamiatul Islamiyya Muslim School na baadae katika shule ya serikali Kitchwele Boys Government School.
Baba yangu alinieleza jinsi Abdulwahid na Ally walivyopenda kujinasibu na asili yao ya Kizulu na baba yangu kaka yake mkubwa Humud walijinasibu kuwa wao ni Wakongomani.
Jina jingine la baba yangu mkubwa lilikuwa Popo - jina la babu yake, Samitungo Mwakapopo.
Hili lilikuwa ndiyo jina ambalo alijulikana mjini Dar es Salaam katika miaka ya 1950, ambako aliishi, akafanya kazi na kufia hapo.
Babu yangu Salum Abdallah na Kleist Sykes walikuwa majirani katika miaka ya 1930 nyumba zao zikitazamana katika Mtaa wa Kipata (Sasa Kleist Sykes) na wote wakiwa wameajiriwa na Tanganyika Railways.
Babu yangu akifanya kazi katika karakana ya kuyeyusha chuma.
Lango kuu la kuingia Loko Shedi kama sehemu hiyo ilivyokuwa ikijulikana ilikuwa limeelekea katika mtaa ambao sasa unajulikana kama Mtaa wa Nkrumah, siku hizo ulikuwa Arab Street.
Hii ndiyo ilikuwa karana kuu ambayo treni na mabehewa yake yalikuwa yakifanyiwa matengenezo na vipuli kutengenezwa hapo.
Kazi yake ilikuwa ngumu inayohitaji kufanyika katika hali ya joto la juu kabisa kutoka katika moto ambao ulihitajika ili kukunja chuma kwa moto mkali.
Hii ilikuwa kazi ngumu iliyohitaji nguvu na afya nzuri, kazi hasa iliyomfaa babu yangu kwa tambo lake kubwa la Kimanyema.
Kleist alikuwa amesoma katika shule ya Wajerumani. Kwa ajili hii basi alikuwa na kazi isiyokuwa na sulubu, wakati ule akiajiriwa kama Accounts Clerk (Karani wa Mahesabu).
Kleist na Salum Abdallah, baba yangu alinifahamisha, hawakuwa kwa hakika watu waliopendana sana.
Wazulu wanafahamika kwa sifa ya shari kama walivyo Wamanyema.
Lakini mke wa Kleist Bi. Mruguru bint Mussa na bibi yangu Bi. Zena bint Farjala walikuwa marafiki wakubwa.
Watoto wa Kleist Sykes na Salum Abdallah walikuja kujenga urafiki ambao ulidumu miaka mingi na mimi nikaukuta hivyo nilipozaliwa mwaka wa 1952.
Wakati nakua, nilikuja kujua kuhusu watu hawa na mambo yaliyotokea Dar es Salaam hata kabla sijazaliwa.
Baba yangu, ndugu zake na watu wengine wa Dar es Salaam walikuwa ndiyo walimu wangu kwa yote niliyojifunza kuhusu mji wenyewe na historia yake.
Itaendelea In Shaa Allah...
Bwana mudiSoph...
Hupendi kusoma historia ya Dar-es-Salaam ya zamani?
Inaelekea watu wengi wanavutiwa.
Tuko 8K ...and counting...
Sopho...Bwana mudi
Ukikuta uzi wa mtu ameuliza swali jibu hoja, sio kuleta historia ya maisha yako na za babu zako, zinaweza zikawa na maana kwa upande wako na sio kwa watu wote au kila mahali .
Hizi takataka kama kasi yake ndiyo hii itakuchukua mwaka mzima, na pengine itabidi nifanye utaratibu wa ku'automate' majibu yangu.
Ngoja nitafute njia sahihi ya kukufanyia hilo. Sitakuacha, tupo pamoja sana.
Hizi takataka kama kasi yake ndiyo hii itakuchukua mwaka mzima, na pengine itabidi nifanye utaratibu wa ku'automate' majibu yangu.
Ngoja nitafute njia sahihi ya kukufanyia hilo. Sitakuacha, tupo pamoja sana.