Ni kwa namna gani Julius Nyerere aliwazidi "Ujanja" wazee wa Kariakoo waliompokea kwenye siasa za Dar es Salaam?

Bwana Kalamu, ungetupa historia unayoifahamu kwa upande wako, ili sisi wasomaji wengine tufaidike.
kuishia kusema "takataka" unatunyima haki kuujuwa ukweli.

Tafadhali bwana Kalamu.
Sina neno na wewe.
Nipo hapa kwa minajiri ya Mzee Mohamed Said.
Asante sana kwa kunivumilia.
 
Taka ni zako siyo za hao wenye picha.
'Kalamu,
''...barua isiyokuwa na tarehe kutoka TAA kwenda kwa Malkia Elizabeth iliyotiwa saini na viongozi wote wa TAA: Rais Julius Nyerere, Makamu wa Rais Abdulwahid Sykes, Katibu Mkuu Dome Okochi, Naibu Katibu Dossa Aziz, Mweka Hazina John Rupia, Naibu Mweka Hazina Ally Sykes ikimpongeza Malkia kwa kutawazwa; barua ya mwaka 1952 toka kwa Rashid Mfaume Kawawa kutoka Bukoba kwenda kwa Ally Sykes ikimfahamisha juu ya hali ya siasa katika Kanda ya Ziwa; barua ya mwaka 1963 toka kwa Lady Judith Listowel, Kenneth Kaunda, Julius Nyerere, Kasela Bantu, Chifu Thomas Marealle ...orodha haina mwisho.

1679494696068.jpeg

Nyaraka ya Sykes yenye majina ya viongozi wa TAA 1953
 
View attachment 2561677
Nyaraka ya Sykes yenye majina ya viongozi wa TAA 1953
Spidi yako ya uzoaji wa hizi taka ni hafifu mno. Zilete haraka ili tupate muda wa kufanya mambo mengine.
 
Bwana Kalamu, ungetupa historia unayoifahamu kwa upande wako, ili sisi wasomaji wengine tufaidike.
kuishia kusema "takataka" unatunyima haki kuujuwa ukweli.

Tafadhali bwana Kalamu.
Pesaa,
Kuhusu historia hii ya TANU na uhuru wa Tanganyika huyu hawezi kuwa na la kusema kwa kuwa hajui.

Na si yeye ambao hawakujua historia ya kweli ya TANU.
Prof. Haroub Othman yeye alipata mshtuko aliposoma kitabu changu.

Prof. Haroub hakuweza kukaa kimya alitaka kujua ukweli.

Alimkabili Mwalimu Nyerere kutaka kujua kama yale aliyosoma katika kitabu changu ni kweli.

Hili nishalieleza mara kadhaa hapa JF.
Ndiyo sababu ya kuandikwa ''Nyerere Biography,'' kujaribu kujibu kitabu changu.

Na hata kilipokuwa kinatafitiwa kitabu cha Mwalimu Nyerere jopo la waandishi likiongozwa na Prof. Issa Shivji walikuja nyumbani kwangu na tulifanya vikao viwili wakitaka niwaeleze historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na uhusiano wake na wazee wangu.

Sasa huyu ndugu yetu amegeuza mjadala wa kisomi kuwa vita kati yangu mimi na yeye hataki mtu mwingine amuulize swali lolote.

Anataka aachiwe anitukane.

1679496276718.jpeg

Kulia Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Othman na Dr. Ng'wanzi Kamata​
 
Spidi yako ya uzoaji wa hizi taka ni hafifu mno. Zilete haraka ili tupate muda wa kufanya mambo mengine.
Kalamu,

Dibaji
Usomi makini unadai kuwa kila mtafiti anapashwa kuwa hadhiri na kile ambacho wenzake wameandika kuhusu utafiti ambao yeye anataka kufanya.

Jambo hili zito busara yake ni kutia hima kwa watafiti wapya kuanzia utafiti pale wenzake walipoachia.

Ni siri iliyo wazi kuwa jambo hili azizi linafuatwa katika kulikwepa kuliko kulitimiza.

Katika kitabu hiki mwandishi amejitokeza kama msomi makini.

Kitabu hiki, ‘’Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968) Kisa Kilichofichwa Kisifahamike Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza Katika Tanganyika,’’ kwa hakika ni kazi ya kupigiwa mfano.

Inajitokeza kuwa Mohamed Said amefanya juhudi za makusudi kupata na kufahamu utafiti uliokwishafanywa katika historia ya siasa Tanzania.

Umuhimu zaidi wa kazi hii ni kuwa mwandishi alikuwa na bahati maalum ya kupata habari muhimu kabisa kutoka katika majalada, barua, shajara na kumbukumbu za ukoo wa Sykes (ambao unahesabika kama ndiyo chimbuko la siasa Tanganyika katika kupambana na ukoloni wa Waingereza), kumbukumbu ambazo watafiti waliopita hawakubahatika kuzipata.

Kwa ajili hii basi matokeo ya utafiti wao ulifikiwa bila na kuwa na kumbukumbu za kuaminika.

Hata hivyo Mohamed Said anasema kuwa makosa haya hayakutokea kwa bahati mbaya, la hasha, huo ulikuwa mpango maalum wa kufifilisha historia ya kweli ili isifahamike.

Mwandishi ana ushahidi wa kushangaza kuwa historia rasmi ya Tanzania imejaa makosa ya makusudi na siyo yanatokana na kutojua.

Katika kitabu hiki Mohamed Said anatoa uchambuzi wa makosa ya historia pamoja na usaliti uliopitika.

Hii ni kazi ya kishujaa na ya ukweli kuhusu matatizo ya kijamii yatokanayo na historia kama Tanzania inavyokumbwa nayo, kitabu hiki huenda kikaleta mjadala wa wasomi kuanzisha ubishani mkubwa.

Ikiwa mtu anakubaliana na mtazamo wa mwandishi au la bado ni wazi kuwa watafiti wa baadae watakuta hazina yenye thamani kubwa katika kitabu hiki hasa katika rejea ambazo kabla yake zilikuwa hazifahamiki.

Vilevile ifahamike kuwa juu ya kuwa mwandishi amezama sana katika somo lakehili bado uandishi wake ni mwepesi na wa kuvutia.

Dr Hamza Mustafa Njonzi
Mwenyekiti, Idara ya Fasihi
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam

nqG9dlfLYcTjplFrTULGc1Pmcvfc1N_dimOkE85RY_0kAyjNc3RaE7snY84ct7nOovrV1l5RCA-IFtqzb3acZwwfVttgwSeleibDKU7FYgUvfsa_0SHB3QhLZ4S67hedF7C5trorlQfaZ7LPwvPhvw-DenMRlBtimqPQ1KriQGma2hn-cKhh6_HoChIpbKdx7gQYDQpPbrCSfYJ_CSc4BMs68O_qGmS4jYtHGdyDeb0Ls5q8WO_9IyOaujXGEAW30uKedrmXcxkt-0yMQJx47NCBE9bWXtDenSZYXdOep9pkS8WmfE6cP--FLraS6fFFLeLpXkIwnNxEXOSwhLhkCpuFjiZZTc-wuxdWV9okPzLp0Z8nemfZ6mam1VDYxr-OfTBMjCQKJxd63UVzhTSpxo7mseR7cBx0buTin2NTWWXblVafAYAKhZG5ZPAZ2CKQsOJMp9GL3HXv_7mxZ5BgZlFYMKTk5BtLjVHPx7AaB4zguZGjUdLb9uKVTHr_KVMoIS9Af_M5kktEcLdFWklR6lpaZ0EZz8KpbLI8BT7ZGI09S9AUdh2AyW8jMtu6GSJuJ-3IlvS_s-4EtGvCgyLj1sbvD49MF-A18iBYNW3bY99Xk4t9UMlJNvgfrykxaRM_AaZSu_yjfHmo_Y2VhRkQseYXN7c2wvFQwa_UiChvtL4oy0p4Eq-csa_GcOhwW8eCHeL92agRBt3uCYPYSK0ybZq8uYmo6oxE2HgKabzESMxb-QbcgqMks1mEbAGWDvJ5apjj3OXbqZ2HhO8aAuk8lsPn8uF6C4M_G0Zu8exTToLO8COY9DRSFbcmDxDOQQKykH7uoHFFSoGvvBPOQsWd9U3EkVKaGH5wkM5onVjDiv_r8b_HXlpnHbLz0l7URk9C0ItsRCC6u-xTTXrM7V8UEAvUHdwELtScqQwlde3QgtLtygtnTk8iRA7NmJFs92GiEZN--OW7vGcj8XUydQ=w957-h650-s-no

Prof. Hamza Mustafa Njozi na Mwandishi
Kenyatta University, Nairobi
 
Fanya haraka nahizi taka zako bwana.

Weka mbilimbili au zaidi twende haraka
 
Fanya haraka nahizi taka zako bwana.

Weka mbilimbili au zaidi twende haraka
Kalamu,

MAISHA NA NYAKATI ZA ABDULWAHID KLEIST SYKES
(1924 – 1968)
Utangulizi 1

Kazi hii ni matokeo ya mambo niliyoyapata kuyafahamu mimi mwenyewe kutokana na masimulizi niliyopokea kutoka kwa watu wengi, kuhusu mambo yalitokea Dar es Salaam.

Nikiwa nimezaliwa Dar es Salaam ambako ndipo kulipokuwa na chimbuko la harakati za kupinga ukoloni Tanganyika, kama Tanzania ilivyokuwa ikijulikana wakati huo, nina kumbukumbu nyingi za watu mashuhuri na matukio yaliyotokea.

Kauli za watu waliyoyaona mambo kwa macho yao wenyewe yakitendeka zilikuza maarifa yangu.

Nilipokuwa mwanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mahali ambapo utafiti wa kitabu hiki ulipoanza, niligundua kuwa mambo yaliyokuwa yakifundishwa kuhusu harakati za kudai uhuru wa Tanganyika hayakulingana na ukweli kama niliyokuwa nikiujua.

Kidogo kidogo nikatambua kuwa kulikuwa na jaribio la makusudi kabisa la kufifilisha kazi kubwa iliyofanywa na baadhi ya wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Nikiwa kijana mdogo, baba yangu Said Salum Abdallah alikuwa akinisimulia habari za ushujaa wa babu yake, Samitungo Mwekapopo.

Samitungo alivuka mpaka toka Belgian Congo na kuingia Tanganyika kupitia sehemu ya kaskazini ya ziwa Tanganyika katika miaka ya mwishoni 1800.

Wakati huo Tanganyika ilikuwa chini ya utawala wa Wajerumani. Wajerumani walikuwa wamewashinda Waarabu chini ya Abushir bin Salim Al Harith katika ukanda wa pwani na machifu kama Mkwawa waliokuwa wakitawala bara.

Samitungo alipata kupigana na chui, akamuua na yeye akanusurika kuuwawa.

Hata hivyo yule chui alimtia kilema cha maisha. Babu yangu Salum Abdallah Popo alizaliwa Shirati huko Musoma ambako baba yake Samitungo alikuwa askari katika Boma la Wajerumani.

Nasikia kuwa boma hilo lingalipo hadi leo.
Babu yangu Salum Abdallah alikuwa mtu jasiri kama baba yake.

Ingawa vitabu vya historia havimtaji, lakini babu yangu yeye ndiye aliyeongoza mgomo wa kwanza wa Tanganyika mwaka 1947 dhidi ya Waingereza katika majimbo ya kati ya Tanganyika.

Babu yangu Salum Abdallah alikuwa mmoja wa wazalendo wa kwanza wakati wa ukoloni kuanzisha harakati za vyama vya wafanyakazi.

Vilevile alikuwa kati ya watu wa mwanzo kuiunga mkono Tanganyika African National Union (TANU), chama cha kizalendo kilichopigania na kunyakua uhuru kutoka kwa Waingereza mwaka 1961.

1679504461229.jpeg

Salum Abdallah
1894 - 1974​
 
View attachment 2561836
Salum Abdallah
1894 - 1974​
bado spidi hairidhishi jinsi unavyoziweka hizi takataka humu jamvini.

Ongeza spidi zaidi.
 
MAISHA NA NYAKATI ZA ABDULWAHID SYKES
(1924 – 1968)
Utangulizi 2

Babu yangu alipendelea kuitwa kwa jina lake la utani ‘’Kapipi,’’ ambapo neno la Kimanyema lililokuwa na maana ‘’Mweusi.’’

Baadaye alipostaafu kazi na akiwa na mtu wa kujiweza kidogo na akiishi Tabora, wale waliokuwa karibu naye walimwita kwa jina la utani ‘’Gulamsojo,’’ likimaanisha ‘’Bwana.’’

Lakini jina hili hawakuthubutu kulitamka mbele yake kwa sababu babu yangu alijulikana kuwa hakuwa mtu wa maskahara hasa kwa yale mambo yasiyompendeza.

TAA ilipofanya mkutano wa siri katika shule moja pale Tabora ili kuchangisha fedha kumwezesha katibu wa TAA Jimbo la Magharibi Germano Pacha kusafiri Dar es Salaam kuhudhuria mkutano mkuu wa kuanzishwa TANU Julai mwaka 1954 mchango mkubwa kupita yote ilikuwa shilingi ishirini.

Fedha hizi alitoa babu yangu.

Mkutano huu ulihudhuriwa na watu maarufu wa Tabora pamoja na baadhi ya waalimu kama Abubakar Mwilima, Harub Said na George Magembe.

Hawa walikuja kuwa watu muhimu sana wakati wa harakati za kudai uhuru.

Hata hivyo, babu yangu alitupana mkono na Julius Nyerere kama wengi walivyofanya, na alitiwa kizuizini na serikali mara baada ya uhuru chini ya Preventive Detention Act ya mwaka 1962.

Mara nyingi nilipodadisi baadhi ya mambo katika historia ya TANU jibu nililopata kutoka kwa waalimu wangu na wanafunzi wenzangu lilikuwa, ni ‘’Lete ushahidi wako.’’

Nilipomtaja baba yangu kuwa ndiyo shahidi wangu, wenzangu walinifanya kichekesho na kuniona mpumbavu.

Baba yangu Said Salum alizaliwa Tabora lakini aliishi maisha yake yote ya utoto na ujana wake Dar es Salaam.

Kupitia kwake nilijifunza mambo mengi kuhusu mji wenyewe na kuhusu maisha yake ya utoto akiwa na rafiki zake, Abdulwahid Sykes na mdogo wake Ally.

Waliingizwa shule pamoja katika Al Jamiatul Islamiyya Muslim School na baadae katika shule ya serikali Kitchwele Boys Government School.

Baba yangu alinieleza jinsi Abdulwahid na Ally walivyopenda kujinasibu na asili yao ya Kizulu na baba yangu kaka yake mkubwa Humud walijinasibu kuwa wao ni Wakongomani.

Jina jingine la baba yangu mkubwa lilikuwa Popo - jina la babu yake, Samitungo Mwakapopo.

Hili lilikuwa ndiyo jina ambalo alijulikana mjini Dar es Salaam katika miaka ya 1950, ambako aliishi, akafanya kazi na kufia hapo.

Babu yangu Salum Abdallah na Kleist Sykes walikuwa majirani katika miaka ya 1930 nyumba zao zikitazamana katika Mtaa wa Kipata (Sasa Kleist Sykes) na wote wakiwa wameajiriwa na Tanganyika Railways.

Babu yangu akifanya kazi katika karakana ya kuyeyusha chuma.

Lango kuu la kuingia Loko Shedi kama sehemu hiyo ilivyokuwa ikijulikana ilikuwa limeelekea katika mtaa ambao sasa unajulikana kama Mtaa wa Nkrumah, siku hizo ulikuwa Arab Street.

Hii ndiyo ilikuwa karana kuu ambayo treni na mabehewa yake yalikuwa yakifanyiwa matengenezo na vipuli kutengenezwa hapo.

Kazi yake ilikuwa ngumu inayohitaji kufanyika katika hali ya joto la juu kabisa kutoka katika moto ambao ulihitajika ili kukunja chuma kwa moto mkali.

Hii ilikuwa kazi ngumu iliyohitaji nguvu na afya nzuri, kazi hasa iliyomfaa babu yangu kwa tambo lake kubwa la Kimanyema.

Kleist alikuwa amesoma katika shule ya Wajerumani. Kwa ajili hii basi alikuwa na kazi isiyokuwa na sulubu, wakati ule akiajiriwa kama Accounts Clerk (Karani wa Mahesabu).

Kleist na Salum Abdallah, baba yangu alinifahamisha, hawakuwa kwa hakika watu waliopendana sana.

Wazulu wanafahamika kwa sifa ya shari kama walivyo Wamanyema.

Lakini mke wa Kleist Bi. Mruguru bint Mussa na bibi yangu Bi. Zena bint Farjala walikuwa marafiki wakubwa.

Watoto wa Kleist Sykes na Salum Abdallah walikuja kujenga urafiki ambao ulidumu miaka mingi na mimi nikaukuta hivyo nilipozaliwa mwaka wa 1952.

Wakati nakua, nilikuja kujua kuhusu watu hawa na mambo yaliyotokea Dar es Salaam hata kabla sijazaliwa.

Baba yangu, ndugu zake na watu wengine wa Dar es Salaam walikuwa ndiyo walimu wangu kwa yote niliyojifunza kuhusu mji wenyewe na historia yake.

1679519003830.jpeg

Mohamed Said
1679519233443.jpeg

Al Jamiatul Islamiyya Muslim School​

Itaendelea In Shaa Allah...
 
View attachment 2562072
Mohamed Said
View attachment 2562075
Al Jamiatul Islamiyya Muslim School​

Itaendelea In Shaa Allah...
Hizi takataka kama kasi yake ndiyo hii itakuchukua mwaka mzima, na pengine itabidi nifanye utaratibu wa ku'automate' majibu yangu.
Ngoja nitafute njia sahihi ya kukufanyia hilo. Sitakuacha, tupo pamoja sana.
 
Soph...
Hupendi kusoma historia ya Dar-es-Salaam ya zamani?

Inaelekea watu wengi wanavutiwa.
Tuko 8K ...and counting...
Bwana mudi

Ukikuta uzi wa mtu ameuliza swali jibu hoja, sio kuleta historia ya maisha yako na za babu zako, zinaweza zikawa na maana kwa upande wako na sio kwa watu wote au kila mahali .
 
Sopho...
Naona umekasirika.
.
Umesema, ''Huyu mzee ashavuruga thread ya mtu na habari zake za kleist''
Hapa sijaona swali.

Lakini ukipenda niulize swali nitajitahidi kujibu.

Historia ya maisha yangu umuhimu wake unakuja katika kuwepo nyakati Mwalimu Nyerere anakuja Dar es Salaam na anapokelewa na wazee wangu.

Hawa wazee wangu ndiyo walionieleza mimi historia ya harakati za uhuru.
Ikiwa hupendi kusoma historia hii yangu acha kusoma.

Lakini mimi kumjua Nyerere kwa kiasi nilichomjua na kuandika kitabu ambacho watu wengi wakamjua ndiyo iliponifikisha hapa kuwa namweleza Nyerere na historia ya uhuru na watu wanakuja hapa kunisoma.

Ukiifuta historia hii ninayoileza mimi ya wazee wangu na Nyerere hutokuwa na historia ya TANU.

Leo watu wanaisoma upya historia ya Nyerere na TANU na sababu ni mimi kumuandika kama anavyostahili kuandikwa.

Angalia hiyo picha hapo chini niko na Abbas Sykes kwa ajili ya kipindi cha TV kuhusu historia ya TANU na Mwalimu Nyerere.

Abbas Sykes kamuona mara ya kwanza Nyerere nyumbani kwao mwaka wa 1952 alipoletwa na Kasella Bantu kwa kaka yake Abdul Sykes wakati huo Act. President wa TANU na Secretary.

Ikiwa historia hii inakughadhibisha kuisikia ikielezwa hii ni bahati mbaya sana kwako.

1679546868334.jpeg
 
Hizi takataka kama kasi yake ndiyo hii itakuchukua mwaka mzima, na pengine itabidi nifanye utaratibu wa ku'automate' majibu yangu.
Ngoja nitafute njia sahihi ya kukufanyia hilo. Sitakuacha, tupo pamoja sana.

Kalamu,

MAISHA NA NYAKATI ZA ABDULWAHID SYKES (1924 – 1968)

Utangulizi 3

Wakati huo mjini Dar es walikuwako Wazulu wanne maarufu kutoka Afrika ya Kusini; Kleist Sykes.

Hili ni jina alilosajiliwa na Wajerumani alipozaliwa.

Udogoni akijulikana kama Kleist Plantan, hili jina la Plantan alilipata kutoka kwa Afande Plantan, mlezi wake baada ya kifo cha baba yake Sykes Mbuwane.

Affande lilikuwa ni cheo katika jeshi la Waturuki.

Huenda liliingizwa ndani ya majeshi ya Wajerumani wakati wa vita Kuu Vya Kwanza ya Dunia wakati Uturuki na Ujerumani zilipokuwa washirika katika vita hivyo).

Kwa kweli jina la Kizulu la Affande Plantan lilikuwa Shangaan.

Hili jina lilitokana na kijiji Inhambane Msumbiji, walikotoka Sykes Mbuwane na Affande Plantan.

Wajerumani waliwaajiri Wazulu 400 kutoka Msumbiji kama mamluki na kujanao Tanganyika ili wapigane na Abushiri na Chifu Mkwawa.

Pamoja na Kleist katika mji wa wa Dar es Salaam walikuwepo ndugu wa mbali watatu, Mwalimu Thomas Plantan, (hilo jina Mwalimu alipewa kwa sababu alikuwa Mwalimu wa shule), Schneider Abdillah Plantan na Ramadhani Mashado Plantan.

Hawa Wazulu waliweza kutambulika kwa urahisi kutokana na majina yao ya Kikristo ingawa wao wenyewe walikuwa Waislam.

Majina hayo yalikuwa na mchanganyiko wa majina ya Kijerumani, Kireno na Kiingereza; kama vilevile Kleist na Schneider ni majina ya Kijerumani; Mashado ambalo ni jina la Kireno na Thomas ni la Kiingereza.

Wote hao, Kleist, Mwalimu Thomas, Schneider na Mashado baadaye walifanya kazi kubwa katika kupiga vita ukoloni na katika kuupeleka mbele Uislamu, kabla na baada ya uhuru.

Bahati mbaya majina haya ya Kiislamu ya wazalendo hawa hayakujitokeza sana badala yake walijulikana zaidi kwa majina yao ya Kizungu waliyoyarithi kutoka Wajerumani kupitia wazee wao wa Kizulu.

Vilevile kulikuwa na idadi kubwa kidogo ya Wamanyema mashuhuri, kama vilevile Mzee bin Sudi (ambaye alikuwa ndiyo kiongozi wa Wamanyema mjini Dar es Salaam), Nassoro Kiruka aliyekuwa mtu tajiri mwenye majumba ya kupangisha na mtu wa kujipendekeza sana kwa Waingereza; na Iddi Tosiri ambaye pamoja na Kleist na Ali Jumbe Kiron a Waislam wengine walijenga Al Jamiatul Islamiyya Muslim School katika miaka ya katikati ya 1930, shule ambayo baba yangu na wengi wa marika yake walipata elimu yao ya dini na ya dunia.

Halikadhalika alikuwepo Erika Fiah, Mganda maarufu aliyeamua kulowea Tanganyika baada ya Vita Vikuu vya Kwanza.

Hawa ‘’wageni’’ ikiwa tunaweza kuwaita hivyo, waliacha athari kubwa katika siasa za mji wa Dar es Salaam.

Nilipokua napata makamo nilikuja kuwajua watu hawa na juu ya matukio yaliyotokea mjini Dar es Salaam hata kabla sijazaliwa katika mwaka 1952.

Baba yangu, ndugu na jamaa na watu wa Dar es Salaam walikuwa ndiyo walionioeleza kila kitu nilichokujakukifahamu kuhusu mji na historia yake.

Ninakumbuka siku moja miaka mingi iliyopita, nilikuwa ninatazama picha ya waasisi wa TANU.

Wakati huo ilikuwani desturi wakati wa kuadhimisha kuasisi kwa kwa TANU mnamo Julai 7, 1954, inapofika tarehe hiyo kila mwaka ilikuwa ni sikukuu.

Ilikuwa kawaida kuchapisha katika magazeti ya serikali na chama, picha ya pamoja ya wale waasisi kumi na saba iliyopigwa mbele ya ofisi ya TAA.

Mmoja wa baba zangu, Abdallah Mohamed aliyefahamiana na Abdulwahid kwa miaka mingi na wakiishi jirani alitazama picha ya Abdulwahid kisha akasema, ‘’Huyu ndiye mtu aliyeasisi chama cha TANU na angekuwa rais wa nchi hii, kama angetaka.’’

Vilevile baba yangu aliniambia, mara yake ya kwanza kumuona Julius Nyerere ilikuwa mwaka 1952 nyumbani kwa Abdulwahid Mtaa wa Aggrey na Stanley.

Wote wawili baba yangu, na Abduwahid walikuwa vijana umri wao miaka 28.

Baba yangu alikuwa mbali sana na siasa.

Ally Sykes alipata kuniambia kuwa alijaribu mara nyingi sana kutaka kumwingiza baba yangu katika harakati za TANU lakini alishindwa.

Kitu kimoja tu kilichomuunganisha na marehemu Abdulwahid ilikuwa ni utanashati na kwa enzi zile wao ndiyo walikuwa vijana maarufu wa mjini.

Walichanganya utamaduni wa Kiswahili na ule wa Ulaya na sehemu nyingine za dunia. Walisikiliza muziki wa Edmund Ross, Victor Silvester, Nat King Cole, Louis Amstrong, Alma Cogan, Bing Crosby na wanamuziki wengine.

Wakati mwingine waliwasikiliza waimbaji wa Kiarabu, Um Kulthum, Mohammed Abdulwahab, Farid Atrash, Abdul Halim Hafidh, Feiruz na Sabah.

Santuri za baba yangu za muziki wa jazz zimedumu kwa muda mrefu zaidi ya miaka ya arobaini.

Familia yangu ilifahamiana na Dome Budohi, mmoja wa wanaharakati kutoka Kenya.

Wakati ule wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika alikuwa akiishi Dar es Salaam.

Budohi alikuwa mmoja wa wazalendo walioasisi TANU na kadi yake ya uanachama ni nambari sita aliyopewa Julai 1954.

Mwaka 1955 alikamatwa na serikali ya kikoloni kwa tuhuma ya kuwa mmoja wa askari wa Mau Mau harakati za wazalendo takriban wengi wao wakulima wadogo waliokuwa wakipigana na ukoloni wa Waingereza nchini Kenya.

Ninazo kumbukumbu nyingi za utoto nikimtembelea Budohi Kituo Cha Kati cha Polisi.
Hivi sasa jengo hilo ni Makao Makuu ya Shirika la Reli la Tanzania.

Wakati huo mimi nilikuwa mtoto, si zaidi ya miaka minne hivi.

Jambo la kwanza ninalokumbuka kuhusu Budohi ni kuwa kila mara tulipokwenda kumtembelea tulimkuta anasoma gazeti.

Baadae Budohi alihamishiwa Kenya na aliwekwa kizuizini katika kisiwa cha Lamu.

Alipofunguliwa toka kizuizini mwaka wa 1963 miezi michache kabla ya uhuru wa Kenya, Budohi alikwenda Uganda na akaajiriwa na gazeti la Uganda Argus.

Hivi sasa ninaelewa kwa nini siku zile kila mara nilikuwa namkuta amezama ndani ya gazeti kila tulipokwenda kumtembelea pale rumande mjini Dar es Salaam.

Niliweza kwa msaada wa rafiki yake Maxwell aliyelowea Tanganyika, kumpata Budohi mjini Nairobi mwaka 1972.

Nilimtembelea mjini Nairobi wakati huo alikuwa akiishi Ruiru maili chache kutoka Nairobi mjini.

Budohi alikuwa ametundika picha ya Nat King Cole sebuleni kwake. Mwaka 1974 nilimtembelea tena, safari hii akiishi Ngei Estate.

Budohi alikuja kuwa mtu wa kwanza kabisa kunipa habari kuhusu historia ya harakati za Tanganyika dhidi ya ukoloni wa Waingereza.

Hata hivyo wakati ule nilikuwa bado sijapata hamu wala kuwa na hamu ya kuandika kitabu kuhusu uhuru wa Tanganyika.

Katika hali kama hii vipi mimi nisijione kuwa ni sehemu ya historia hiyo?

Katika hali kama hii vipi nitamudu kukaa kimya wakati historia ya uongo ndiyo inatoenziwa na ile ya kweli inafichwa?

Nilipoanza kupitia vitabu na maandiko mengine juu ya historia ya TANU nilistaajabu kuona kuwa hakuna hata mmoja kati ya watu mashuhuri niliowajua ambao walihusika na harakati za uhuru walikuwa wametajwa katika vitabu hivyo.

Nilipigwa na butwaa nipogundua kuwa hata Abdulwahid Sykes, mzalendo ambae baba yangu akimtaja sana katika historia ya TANU hakuwa ametajwa popote na badala yake kila mahali lilikuwa jina na Julius Nyerere peke yake.

1679547637448.png

Thomas Plantan 1964
1679547830152.png

Kleist Sykes 1942
1679547915176.jpeg

Mwandishi na Dome Okochi Budohi Nairobi 1972
Kadi yake ya TANU No. 6

Hizi takataka kama kasi yake ndiyo hii itakuchukua mwaka mzima, na pengine itabidi nifanye utaratibu wa ku'automate' majibu yangu.
Ngoja nitafute njia sahihi ya kukufanyia hilo. Sitakuacha, tupo pamoja sana.
1679549150332.jpeg
 
Back
Top Bottom