Ni kwa namna gani Julius Nyerere aliwazidi "Ujanja" wazee wa Kariakoo waliompokea kwenye siasa za Dar es Salaam?

Ni kwa namna gani Julius Nyerere aliwazidi "Ujanja" wazee wa Kariakoo waliompokea kwenye siasa za Dar es Salaam?

Huyo mzee mudi anaumia sana moyo wake kuiona hii nchi inastawi kwa umoja na amani kwa kila raia bila kujari utikadi na imani yake,yeye alitaka nchi zima wavae kobazi,balaghashia na kanzu.

Huyu mzee ni wa kumuonea huruma mana ni fanatic na lunatic. Chuki aliyonayo itamfuata hadi kaburini.
Pengine wewe ndio una chuki? Mpaka Jamiiforums wamempa Tuzo ya Heshima, Melo mwenyewe anatambua mchango wake,

Msome Prof James L Giblin

Ana Tuzo 17 mbalimbali level za Chuo hadi Nchi, Vitabu na Journal za Kutosha, Speciality yake ni History ya Tanzania na East Africa, Huwezi kuwa Recorgized na Mtu kama huyu kwa kuwa na Chuki tu na udini,
 
Umepewa historia, mtu amekutana na Kenyata, ameenda Uganda hadi Kuunganisha Uganda na kenya kwenye Screenshot iliyowekwa, Bado unaona mtu ana Akili ya Kariakoo? Mtu alieweza kuanzia Chama nchi nzima na kuweka Branch mikoani na kukusanya Maelfu ya Watu kudai uhuru unahisi fikra zake ziliishia kariakoo?
Hao ni Islamophobes.
 
Mzee Mohamed ungekuwa na uwezo ungetaka iandikwe kwamba Sykes ndo alipambania uhuru kuliko hata Nyerere. Siku moja kubali tu kuwa Nyerere alikuwa mbali sana kifikra kuliko Sykes na wazee wengine wa Kariakoo. Hatumdharau Sykes ila ndo uwezo wake ulipokuwa umefikia kina Mwalimu Nyerere wakaanzia pale alipoishia yeye.
Mama...
Mimi nitakuwa mjinga sana kama nitapuuza uwezo wa Mwalimu Nyerere.

Kwanza fikiria uwezo watu hawa ambao ndiyo walikuwa ndani ya TAA Political Subcommittee mwaka wa 1950: Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.

Mshauri wa hii kamati akiwa Earle Seaton.

Sijui kama wewe unajua uwezo waliokuwanao watu hawa.

Hawa ndiyo walikuwa wanapanga mipango ya kuikomboa Tanganyika na hawa ndiyo waliomtia Nyerere katika uongozi wa juu wa TAA.

Kwa kipande hiki cha historia kinaonyesha uwezo mkubwa wa Mwalimu Nyerere.

Swali langu kwako ni hili.

Wewe ulikuwa unawajua hawa niliokutajia kuwa walipigania uhuru wa Tanganyika?

Mimi nimenyanyua kalamu kusahihisha historia iliyokuwa inamtaja Nyerere peke yake na kueleza historia ya TANU kama ilivyotakiwa kuandikwa.

Kubwa na hili ndilo wengi hapa linawaumiza ni kutaja mchango wa Waislam na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika katika kupigania uhuru.

Mufti Sheikh Hassan bin Ameir akiuza kadi za TANU misikitini na aliwaongoza Waislam kumuunga mkono Julius Nyerere.

Je, wewe hupendi haya yakaelezwa katika historia ya uhuru?

Hakuna mahali unaweza kusema hawa wazalendo waliishia hapa katika kudai uhuru na Nyerere akaanzia hapa.

Hawa na wazalendo wengine walikuwapo na Nyerere toka walipompokea 1952 hadi uhuru unapatikana 1961.

Nyerere angekuwa mbali sana angeunda TANU nje ya watu hawa na labda angeunda chama chake.

Lakini Nyerere kamkuta Abdul na wenzake katika harakati za uhuru katika African Association (1929) na Al Jamiatul Islamiyya (1933) iliyoundwa na baba yake.

Iweje historia hii ifutwe?

Unaweza vipi kuwafuta wazalendo hawa katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ukambakisha Nyerere peke yake?

Sikuandika kitabu kumdogosha Nyerere.

Nimeandika kitabu kusahihisha historia iliyojaa makosa mengi sana.

Hii ndiyo sababu Prof. Haroub Othman alimshauri Mwalimu akubali iandikwe historia ya maisha yake ipatikane nafasi ya kufanya marekebisho ya historia iliyokuwapo ambayo kitabu cha Abdul Sykes iliibomoa.

Unasema ningekuwa na uwezo?
Uwezo ninao na umetambulika.

Kleist Sykes ametiwa katika Dictionary of African Biography (DAB) Oxford University Press, New York 2011.

Kitabu nilichoandika "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924-1968)," Minerva Press London 1998 kimechapwa matoleo manne tunakwenda la tano na kipo kwa Kiswahili pia Phoenix Publishers, Nairobi 2002.

Niko hapa JF sasa mwaka wa 11 nafundisha historia hii.

Kimeandikwa kitabu cha Nyerere (2020) nimeshirikishwa na nimenukuliwa sana ndani ya kitabu hicho.

1679023386363.jpeg
1679023619963.jpeg
Mahojiano na TBC kuhusu Nyerere Biography
1679023713998.png
 
Umeua uzi haya ni mauaji ya kimbali
Mpe...
''Kimbari''
Zamani walimu walikuwa makini sana katika ''R'' na ''L.''
Naona siku hizi hili halizingatiwi.

Vipi hadi mtu anafika kiwango cha ukubwani iwe shida katika kutofautisha kati ya L/R?
Jitahidi sana kwani ukiingia katika mjadala na huwezi kuandika vyema inakuwa ni tatizo kidogo.
 
Pengine wewe ndio una chuki? Mpaka Jamiiforums wamempa Tuzo ya Heshima, Melo mwenyewe anatambua mchango wake,

Msome Prof James L Giblin

Ana Tuzo 17 mbalimbali level za Chuo hadi Nchi, Vitabu na Journal za Kutosha, Speciality yake ni History ya Tanzania na East Africa, Huwezi kuwa Recorgized na Mtu kama huyu kwa kuwa na Chuki tu na udini,
Baba...

1679023958867.jpeg

Prof. James Giblin na kitabu cha Abdul Sykes akiwa ofisini kwake
University of Iowa
qRvJdizi4a49PW4M1zlj1kVCZS8YE_4dRL1CDRdr-Km1_VBu1fIPmBg6RlTnp-LdNF4Go9DDaYISXpJn4gXgJBzUEuMVuSysrMiMz46OS5a04pujCA-JjEpv9g9lLR1evj5spwK4HJCjfw6AZ9XketXpfgMvAfW5Co65UHkMJZL3efKy3WoOowUnoCDqOO8Xc8uo12dWpqQuk9H8497TSXh3ioLyJ4I0NPelINsPBKm1Lpcy9-mozHtM0kTc6acoRYjHK6_1RHZ_oYZxWNeqAVIgO8LbTgDRXYfvb2Vpv55KpVLo49f5dYpcXecZeUrPnYkpPOQfYODIlufGRIyhNiW-WUejADsCeGwjiYv6sT62tpamu2_YDaIqGOrRCve1I7VrrTzeQhHbAK5YfUkcEOXNSO9lrQKRrTvOphrBTjjP6ahLbWkfEgF3gh9N8iDGCqSyEOVT3J8m8y5gKdJ5JjJ-595ry4hxuDhF2aOHkBLYqKo5W0639C1heG5sOjP-i7LtO-O2l7gogn1FsSEYjriNemOlgZRkiZKdb4QXmRduYCqJC2Da9htiwNjY4pVtLF31iFPAv428BLEEnd57x8ChQJcxKspIPLi24esb_z_2Fu-Sq82pbVCg1OdBiEoWhDRttXPzWSaHnMY0cbI8TrNGAMLhvCQb6fzOgxDRKAsmOnMEEjCzVgXz7todFCc5hA7bHGUWGoTIrflrDA2PO4_BT2CE9wvjBVUUI0gJKHJDSJs3FY9rdJcVU1wVPc5VDoxJ1pVLw8As-sOptpSg9jFoDzbTMYoiPAfPWvfUGQhD1pwyo_f3ElQUJOeyjnEYdqWZEWT8820Ohg9u_TtGFMW6TDqP7TDySoEKQfwIPgX7FpcX58PuFGUG63x2-PVcQ4ypK2eYhNMrtVVh55cB0CDVT7w64_LOBXFbV5RmMuHkB7wKkgYJXneCWIz7fpQIEWM696aHlaC7E5Z4tMg=w480-h360-s-no

Prof. Giblin tukiwa darasani University of Iowa
1679025519825.jpeg

Maxence Melo​
 
Hii comment yako sasa ndo imetupa mwanga kamili kumbe suala lako la udini liko katika ngazi ya juu mno. Pole sana Mzee ila muda bado upo unaweza ukabadilika.
Mama...
Pole ya nini?

Mimi nakushukuru wewe kwa kunipa fursa ya kujieleza hapa kwani bila comment hii yako nisingefikiri kueleza hayo hapo chini.

Kwanza hapana udini katika kalamu yangu.

Nisingeweza kuwa ndani ya miradi ya Oxford University Press, Nairobi na New York ningekuwa mdini.

Nisingealikwa vyuoni, Afrika, Ulaya na Marekani kama ningekuwa nahubiri Uislam.

Hii habari ya dini mnayo nyie tu.
Kote duniani naalikwa kama mtaalamu wa historia ya Tanzania.

Hakika taarifa zangu zilifika juu kabisa toka niko mwanafunzi Chuo Kikuu.

Siku moja mwalimu wangu mmoja aliniita ofisini kwake akaniambia siogopi kusema kuwa historia ya TANU imekosewa?

Huyu mwalimu akinipenda na akifurahishwa sana na ''essays'' zangu kuhusu historia ya TANU na jinsi nilivyokuwa naeleza mchango wa Waislam katika historia hii.

Huyu mwalimu wala hakuwa Muislam.

Unaniambia nibadilike.
Nibadilike niwe nani au nini?

Kuwa mimi nikane kuwa babu yangu Salum Abdallah hakupigania uhuru wa Tanganyika au hakuwa mwanachama wa African Association toka 1929 na Al JamiatulIslamiyyafiTanganyika 1933?

Kuwa babu yangu Salum Abdallah hakuwa mwasisi wa TANU na TRAU Tabora na nikane yote yale aliyofanya.

Yaani ni dhambi kuandika historia yake kuwa aliongoza migomo mitatu 1947, 1949 na 1960?

Yaani unataka mimi niwakane wazee wangu kisa sitakiwi kuonyesha mchango wa Waislam katika historia ya uhuru wa Tanganyika?

Ati unanipa pole.

Wape pole wale ambao hawakujaliwa kuwa na cha kujivunia katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Historia hii hakuna tena wa kuifuta.
 
Ulichoandika ni sahihi. Wazee wa Kariakoo fikra zao ziliishia Kariakoo.
Mama...
Naamini kabisa unasema hayo kwa kuwa huijui historia ya uhuru wa Tanganyika.
Soma hapo chini kisha rejea tuendelee na mjadala.

Nimekuta historia hii katika Nyaraka za Sykes:

WANYASA WANAULIZA DENIS PHOMBEAH NI NANI KATIKA HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA ?

Raia Mwema la 14 - 20 Agosti limechapa makala ambayo kwanza ilikuwapo hapa Majlis, ''Tulikotoka Kufika SADC Kisa Cha Ally Sykes, Denis Phombeah na Kenneth Kaunda.''

Nia yangu ya kuweka hapa makala ile ilikuwa baada ya kupigiwa simu na kuombwa nishiriki katika kipindi cha Channel Ten Zahir Hotel ambako wajumbe wa SADC wangefika pale na kuniuliza maswali kuhusu historia ya mgahawa huu na wapigania uhuru wa nchi za Kusini.

Kwenye mlango wa kuingia mgahawa huu kuna kibao kinachoeleza kuwa hapo palikuwa sehemu wakikutana wapigania uhuru wa nchi Kusini ya Afrika.

Kipindi hiki nilifahamishwa kitarushwa mubashara.

Ukweli nilimkatalia huyo aliyenipigia simu na sababu kubwa ni kuwa mwaliko wenyewe umenifikia mchana milango ya saa saba hivi na kipindi kinakwenda hewani saa kumi jioni kwa hiyo hapakuwa na muda wa matayarisho.

Mambo kama haya yanahitaji maandalizi hasa ikiwa kipindi ni mubashara kwa kuchukua tahadhari kusema maneno siyo.

Nikamfahamisha hilo ndugu yangu aliyenifikishia mwaliko nikamwambia hawa ni wageni wa serikali wasije wakaniuliza maswali ambayo majibu yake yanapishana na historia rasmi inayofahamika.

Ikawa nimekataa kushiriki katika kipindi kile.

Lakini ikanijia fikra kuwa ninao bado mchango wa kuchangia katika historia ya Tanganyika na SADC.

Ndiyo nikaamua kuweka hapa safari ya mwaka wa 1953 ya Ally Sykes na Denis Phombeah kwenda Lusaka Northern Rhodesia kuhudhuria mkutano wa vyama vya siasa kutoka nchi Kusini ya Sahara ulioitishwa na Kenneth Kaunda akiwa Rais wa ANC ya Northern Rhodesia.

Ndugu zetu Wanyasa baada ya kusoma gazeti la Raia Mwema na kukuta Mnyasa anaiwakilisha Tanganyiaka katika mkutano ule wamepiga simu nyingi Raia Mwema kutaka kujua mchango wao katika uhuru wa Tanganyika.

Kisa hiki hiki kilichosomwa na wengi hapa Majlis kama ningekieleza mbele ya camera za televisheni tena mubashara athari yake kwa watazamaji ingekuwa nyingine kabisa.

Lingeweza kuja swali kwangu, ''Ally Sykes na Denis Phombeah ni nani na iweje hawa wawakilishe Tanganyika kwani Julius Nyerere alikuwa wapi?''

Unajibu vipi mtu maswali kama haya?

Mhariri wa Raia Mwema kakwepa kuliunganisha jina la Ally Sykes, Denis Phombeah na jina la Kenneth Kaunda.

Si bure kwa yeye kuamua kufanya hivi.

Anazo sababu zake.

Picha: Ally Sykes na Denis Phombeah wakiwa Chileka Airport, Blantyre Nyasaland wakiwa njiani kurudi Dar es Salaam.

69348214_512164766197573_5950547411876184064_n.jpg
68880598_512197066194343_5065484712370241536_n.jpg


 
EeeenHeeee!

Unaji'promote' kwelikweli.

Katika kujiuza huna mfano wa kukufikia.

Tatizo ni kuweka chumvi nyingi katika baadhi ya mambo na kupotosha mengine kukidhi ajenda zinazokupa msukumo.

Sifa hii ya ku'exagerate' katika baadhi ya mambo, na kwingine kutunga uongo kabisa inaharibu taswira nzima ya unayoyasimamia.
Umeambiwa weka ushahidi unaendelea kuja na porojo zako.
 
Usiende huko kwa "kujua 'University'"; labda kama unataka kujifunza toka kwangu.
Hizi habari za kujifanya wewe mtaalam wa kuheshimiwa na vyuo mashuhuri duniani kwa kutunga hadithi usidhani kuwa ndio utaalam.

Kama nilivyosema huko nyuma, sifa pekee uliyojaaliwa kama kipaji ni huko kupamba habari ambazo sehemu kubwa ya habari hizo ni uongo.
Umeandika uongo umestukiwa na sasa unajishaua.

Mwandiko wako ni ule ule(arrogantly) haufichiki hata ukija na id nyingine, tunaukumbuka miaka ile mkaungana kikundi mkijidai mtakuja na kitabu, mkadondokea pua mpaka leo hii.
 
Huyo mzee mudi anaumia sana moyo wake kuiona hii nchi inastawi kwa umoja na amani kwa kila raia bila kujari utikadi na imani yake,yeye alitaka nchi zima wavae kobazi,balaghashia na kanzu.

Huyu mzee ni wa kumuonea huruma mana ni fanatic na lunatic. Chuki aliyonayo itamfuata hadi kaburini.
Siyo "kujari" ni kujali.

Amani ni jadi yetu Waislam, hata neno Uislam linaashiria salama na amani (peace).

Unataka kulinganisha pwani na kwa wakurya? Usitake kuchekesha watu.

.
 
Japo na Mimi sikubaliani nae kwenye mambo flani.. lakini si busara kuita takataka maandishi ya huyu mzee..
Mzee aheshimiwe Ni mwandishi mzuri..
Ninakubaliana na wewe, lakini umekosa kufahamu lengo ni nini.
Anapong'ang'ania kuniwekea vitu ambavyo sikubaliani navyo, basi inalazimu nitumie njia hiyo.
Usingesikia nikiendelea kujibishana naye kama angeachana nami baada ya kujua kuwa siafiki hayo anayoyalazimisha niyasome.
Kwa hiyo hapa nina haki kabisa ya kutumia hiyo lugha niliyotumia.
 
Hapa umedhihirisha ujinga wako, nilikuwa nakuona mtu wa maana sana na msomi humu jukwaani ila hii imenionesha upande mwengine,

Nimefuatilia mjadala mzima, mzee wa watu anakuomba umuoneshe huo uwongo wake ila huoneshi chochote badala yake unamkashifu, mzee wa watu analeta evidence na Hadi picha kuthibitisha.

Huna Tofauti na wale chawa wa ccm, so sad
Mkuu 'Baba-mwajuma', mimi siyo mwanasiasa, na wala sitegemei hata siku moja nitafute sifa maalum za upendeleo toka kwa yeyote. Mimi nawasilisha mawazo yangu, uyapende usiyapende hiyo ni juu yako mwenyewe kufanya uamzi.

Maoni yangu kuhusu haya ya mzee ni hayo hayo hayabadiliki. Huyu ni 'con' mkubwa aliyechota akili za watu kama wewe kwa mtindo wa uwasilishaji wake wa utapeli mkubwa.
 
Back
Top Bottom