Ni kwanini amri ya kuiabudu siku ya sabato tangu enzi za Musa hadi sasa ni jumamosi lakini makanisa mengine huabudu jumapili?

Hilo nalo ni tatizo. Mmeacha kumwabudu Mungu mmekazana kuiabudu siku.
 
Amina 🙏
 
Thibitisha kwa sura na mstari mahali Yesu alikoabudu Sabato.
 
kwa hiyo wewe unataka kufuata desturi za kiyahudi, au unataka kuishi kwa kumwabudu Mungu? kama sabato ilianzia kwa Musa, unawasemeaje wale waliomwabudu Mungu kabla ya Musa? na unamsemaje Musa mwenyewe kabla ya amri 10 ambaye aliishi bila kuheshimu sabato. tuanzie hapo.
 
Maswali ya nyongeza:
1. Kati ya Ibrahimu na Musa ni nani mkuu zaidi?

2. Nani mkuu zaidi kati ya Musa na Yesu

3. Kama ni kuchagua kumtii mmoja, yupi wa kumtii kati ya Ibrahimu, Musa, na Yesu?
 
Sorry, hivi kabla Musa hajapewa amri 10, walikua wanaabudu sabato siku gani?
Hakukuweko na Sabato, walikuwa wakiishia kwa imani.

Abel, Henoko, Nuhu, Shemu, Ibrahimu, Isaka, Yakobo, Yusufu waliishi kwa imani na si kwa Sheria.
 
Yesu aliulizwa na mafarisayo hilo swali,akajibu akasema "Yeye ndiye Bwana wa sabato".
Nikipata mstari naleta hapa.
Ukielewa hii sentensi umepata jibu .
Huu hapa:
"Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato. Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia"
Marko 2:27-28
 
Kwa kusema mwanadamu hajawekwa chini ya utawala wa sabato ndiyo kaitetea sabato?
Soma mwenyewe Marko 2:27-28
 
Huu hapa:
"Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato. Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia"
Marko 2:27-28
Asante sn!

Ukisoma huu mstari ukaelewa hutahangaika na mambo ya siku,ila aliyeiumba hizo siku!
Kimsingi anaetakiwa kuabudiwa ni aliyeumba hiyo siku sio siku!
 
Je, maana ya sabato ni Jumamosi (yaani wakati Mungu anaumba dunia alitumia kalenda tunayotumia leo - the Gregorian calender iliyoanzishwa 1582 - na ambayo inatumika hadi leo)?
 
Je, maana ya sabato ni Jumamosi (yaani wakati Mungu anaumba dunia alitumia kalenda tunayotumia leo - the Gregorian calender iliyoanzishwa 1582 - na ambayo inatumika hadi leo)?
Maana ya sabato sio Jumamosi.. Sabatho ni kitenzi chenye maana sawa na Pumziko ..

Lugha nzuri ni kusema Jumamosi ya Sabatho...
 
Ukristo imeanza na Yesu kabla ya Yesu haukuwepo
Si kweli.. Yesu hajaanzisha ukristo. Paul ndo alianzisha kuwaita watu Wakristo yaani Wafuasi wa Kristo.
 

Attachments

  • Screenshot_20240714-111658~2.png
    25.2 KB · Views: 1

sabato ya kweli iko rohoni;Huwezi kwenda mbinguni just kwa kupumzika na kustarehe tuu peke yake.Haya ni mambo ya sheria za Musa.Ndiyo maana sheria ilisema mtu akifumaniwa apigwe mawe mpaka kufa.Fanya kazi siku sita siku ya saba pumzika.Ile kwamba unapumzika kwa ajili ya ibada nadhani kwa mawazo yangu inatosha.Ikiwa jumapili jumamos inatosha.Kikubwa uwe mtu mwenye hofu ya Mungu ya kweli ndani yako na siyo kuugiza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…