Hiyo Amri ya Sabato ni siku ambayo Wana wa Israeli waliamriwa katika Torati kupumzika shughuli zote za mikono,(Kutoka20:8-10)
Ile Siku haiko tena,ile ilikuwa Kivuli cha Ile Sabato ya Kweli iliyokuwa inakuja,
(Wakolosai2:16-18)
(Waebrania4:4-9)
Katika Agano Jipya sasa kila iitwapo LEO ni Sabato,Yesu Kristo ndiye Sabato (Pumziko) yetu! Alikuja kutupumzisha na kutuweka huru mbali na Utumwa wa dhambi,na anasema
(Mathayo11:28-29)
(Yohana8:34)
Kwa kuwa Yesu Kristo ni Yeye yule yule Jana,LEO hata Milele,tumpelekee mizigo ya dhambi (tumwamini ili atupumzishe na kutuweka huru)
Kwa maana hiyo hatushiki Siku au Miezi au Mwaka,hayo ni Mafundisho Manyonge,tunamshika Yesu ambaye ndiye BWANA wa Sabato,(Wagalatia4:8-11)
Siku zote ni za Kumwabudu,Kumsifu na Kumtukuza Mungu,(Matendo2:46-47)