Ni kwanini amri ya kuiabudu siku ya sabato tangu enzi za Musa hadi sasa ni jumamosi lakini makanisa mengine huabudu jumapili?

Siku ni nuru na giza vikipita, Mungu aliumba dunia kw siku 6 ya 7 alipumzika, hivyo baada ya siku 7 unaanza upya kuhesabu, maneno ya jumamosi na jumapili yalikuja baadae/

Musa alipopewa amri kumi alishaelekezwa siku ipi itakuwa ya saba ya kuanza rasmi kuiabudu Sabato ambayo kwa sasa ni Ijumaa dakika chache kabla jua halijazama mpaka jumamosi lisaa baada ya jua kuzama
Hilo nalo ni tatizo. Mmeacha kumwabudu Mungu mmekazana kuiabudu siku.
 
Hiyo Amri ya Sabato ni siku ambayo Wana wa Israeli waliamriwa katika Torati kupumzika shughuli zote za mikono,(Kutoka20:8-10)
Ile Siku haiko tena,ile ilikuwa Kivuli cha Ile Sabato ya Kweli iliyokuwa inakuja,
(Wakolosai2:16-18)
(Waebrania4:4-9)
Katika Agano Jipya sasa kila iitwapo LEO ni Sabato,Yesu Kristo ndiye Sabato (Pumziko) yetu! Alikuja kutupumzisha na kutuweka huru mbali na Utumwa wa dhambi,na anasema
(Mathayo11:28-29)
(Yohana8:34)
Kwa kuwa Yesu Kristo ni Yeye yule yule Jana,LEO hata Milele,tumpelekee mizigo ya dhambi (tumwamini ili atupumzishe na kutuweka huru)
Kwa maana hiyo hatushiki Siku au Miezi au Mwaka,hayo ni Mafundisho Manyonge,tunamshika Yesu ambaye ndiye BWANA wa Sabato,(Wagalatia4:8-11)
Siku zote ni za Kumwabudu,Kumsifu na Kumtukuza Mungu,(Matendo2:46-47)
Amina 🙏
 
Siku ya sabato ni amri na amri 10 ni kwajili ya wote sio waisrael tu.

Wakolosai2:16-18 zinazungumziwa sikukuu za sabato zilizofanyika kila mwaka kama ilivyo kwa ezekieli 45:17, wala sio sabato ya kila wiki iliyowekwa kwenye amri.

Waebrania 4:4-9: soma na mistari inayofuate 10 na 11 "kwa maana, mtu anayeingia katika pumziko la Mungu, pia hupum zika kutoka katika kazi zake kama vile Mungu alivyopumzika baada ya kazi zake. 11 Basi tujitahidi kuingia kwenye pumziko hilo (sabato) asije mtu akaanguka kwa kutokuamini kama hao."

Kumwamini Yesu ni Pumziko letu hata tunapofanya kazi nzito lakini Sabato inahitaji pumziko la mwili pia, Utaacha shughuli zako upumzike na kuabudu.

Pia hata Yesu aliitambua Sabato kuwa siku maalum takatifu naye akiiabudu, kuisifia na aliitetea pale aliposhambuliwa na mafarisayo. (Marko 2)
Thibitisha kwa sura na mstari mahali Yesu alikoabudu Sabato.
 
Moja ya amri kumi ni kuabudu siku ya sabato, Siku takatifu iliyotengwa na Mungu kuturuhusu KUPUMZIKA kwa kuziweka kando shughuli zetu na tunashukuru kwa kujumuika pamoja kwenye shughuli za kuabudu ikiwa ni ishara ya shukran kisha tunarudi makwetu kupumzika, Kila siku ni siku ya Mungu lakini sio kila siku ni sabato kwasababu si kila siku ya kuacha shughuli zako KUPUMZIKA.

Mfumo wa kutambua siku upo tangu zamani lakini hakukuwa na majina ya kisasa ya siku kama jumamosi na jumapili ndio maana huwezi yakuta hayo majina kwenye biblia, Musa alipopewa amri kumi ikiwemo ya siku ya sabato alishaelekezwa siku rasmi ya kuanza kuiabudu Sabato ambayo kwa mfumo wa sasa imeangukia Ijumaa dakika chache kabla jua halijazama mpaka jumamosi lisaa baada ya jua kuzama, kisha baada ya hapo zinahesabiwa upya siku sita na ikifika ya saba inakuwa Sabato.

Hata Yesu aliikuta siku ya Sabato, aliiabudu, aliisifia na kuitetea (Marko 2), miaka nenda rudi hado sasa ukienda Israel wanaendeleza huu utaratibu, siku ya jumamosi maduka hufungwa na shughuli nyinginezo husimama.

Yesu ni Pumziko letu kiroho hata tunapofanya kazi nzito tukiwa hoi taaban lakini siku ya sabato tunaweka kando shughuli hizo tunapumzisha na miili
kwa hiyo wewe unataka kufuata desturi za kiyahudi, au unataka kuishi kwa kumwabudu Mungu? kama sabato ilianzia kwa Musa, unawasemeaje wale waliomwabudu Mungu kabla ya Musa? na unamsemaje Musa mwenyewe kabla ya amri 10 ambaye aliishi bila kuheshimu sabato. tuanzie hapo.
 
Maswali ya nyongeza:
1. Kati ya Ibrahimu na Musa ni nani mkuu zaidi?

2. Nani mkuu zaidi kati ya Musa na Yesu

3. Kama ni kuchagua kumtii mmoja, yupi wa kumtii kati ya Ibrahimu, Musa, na Yesu?
 
Sorry, hivi kabla Musa hajapewa amri 10, walikua wanaabudu sabato siku gani?
Hakukuweko na Sabato, walikuwa wakiishia kwa imani.

Abel, Henoko, Nuhu, Shemu, Ibrahimu, Isaka, Yakobo, Yusufu waliishi kwa imani na si kwa Sheria.
 
Yesu aliulizwa na mafarisayo hilo swali,akajibu akasema "Yeye ndiye Bwana wa sabato".
Nikipata mstari naleta hapa.
Ukielewa hii sentensi umepata jibu .
Huu hapa:
"Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato. Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia"
Marko 2:27-28
 
Aliiweka sawa sabato, Mafarisayo walijianzishia sheria zao za ziada kwamba hata ukiona mtoto wako ama mfugo wako unazama hutakiwi kuuokoa kwa kisingizio kwamba ni kushughulisha mwili, Sabato inahusu kuweka kando shughuli zako unazofanya lakini sio kukwepa kujishughulisha kabisa kiasi cha kushindwa kuokoa hata maisha ya mwanadamu ama mnyama.

Soma Marko 2, Yesu aliitambua, aliiabudu, aliisifia na kuitetea Sabato
Kwa kusema mwanadamu hajawekwa chini ya utawala wa sabato ndiyo kaitetea sabato?
Soma mwenyewe Marko 2:27-28
 
Huu hapa:
"Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato. Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia"
Marko 2:27-28
Asante sn!

Ukisoma huu mstari ukaelewa hutahangaika na mambo ya siku,ila aliyeiumba hizo siku!
Kimsingi anaetakiwa kuabudiwa ni aliyeumba hiyo siku sio siku!
 
Moja ya amri kumi ni kuabudu siku ya sabato, Siku takatifu iliyotengwa na Mungu kuturuhusu KUPUMZIKA kwa kuziweka kando shughuli zetu na tunashukuru kwa kujumuika pamoja kwenye shughuli za kuabudu ikiwa ni ishara ya shukran kisha tunarudi makwetu kupumzika, Kila siku ni siku ya Mungu lakini sio kila siku ni sabato kwasababu si kila siku ya kuacha shughuli zako KUPUMZIKA.

Mfumo wa kutambua siku upo tangu zamani lakini hakukuwa na majina ya kisasa ya siku kama jumamosi na jumapili ndio maana huwezi yakuta hayo majina kwenye biblia, Musa alipopewa amri kumi ikiwemo ya siku ya sabato alishaelekezwa siku rasmi ya kuanza kuiabudu Sabato ambayo kwa mfumo wa sasa imeangukia Ijumaa dakika chache kabla jua halijazama mpaka jumamosi lisaa baada ya jua kuzama, kisha baada ya hapo zinahesabiwa upya siku sita na ikifika ya saba inakuwa Sabato.

Hata Yesu aliikuta siku ya Sabato, aliiabudu, aliisifia na kuitetea (Marko 2), miaka nenda rudi hado sasa ukienda Israel wanaendeleza huu utaratibu, siku ya jumamosi maduka hufungwa na shughuli nyinginezo husimama.

Yesu ni Pumziko letu kiroho hata tunapofanya kazi nzito tukiwa hoi taaban lakini siku ya sabato tunaweka kando shughuli hizo tunapumzisha na miili
Je, maana ya sabato ni Jumamosi (yaani wakati Mungu anaumba dunia alitumia kalenda tunayotumia leo - the Gregorian calender iliyoanzishwa 1582 - na ambayo inatumika hadi leo)?
 
Maana ya sabato sio Jumamosi.. Sabatho ni kitenzi chenye maana sawa na Pumziko ..

Lugha nzuri ni kusema Jumamosi ya Sabatho...
 
Ukristo imeanza na Yesu kabla ya Yesu haukuwepo
Si kweli.. Yesu hajaanzisha ukristo. Paul ndo alianzisha kuwaita watu Wakristo yaani Wafuasi wa Kristo.
 
Attachments

  • Screenshot_20240714-111658~2.png
    Screenshot_20240714-111658~2.png
    25.2 KB · Views: 1
Moja ya amri kumi ni kuabudu siku ya sabato, Siku takatifu iliyotengwa na Mungu kuturuhusu KUPUMZIKA kwa kuziweka kando shughuli zetu na tunashukuru kwa kujumuika pamoja kwenye shughuli za kuabudu ikiwa ni ishara ya shukran kisha tunarudi makwetu kupumzika, Kila siku ni siku ya Mungu lakini sio kila siku ni sabato kwasababu si kila siku ya kuacha shughuli zako KUPUMZIKA.

Mfumo wa kutambua siku upo tangu zamani lakini hakukuwa na majina ya kisasa ya siku kama jumamosi na jumapili ndio maana huwezi yakuta hayo majina kwenye biblia, Musa alipopewa amri kumi ikiwemo ya siku ya sabato alishaelekezwa siku rasmi ya kuanza kuiabudu Sabato ambayo kwa mfumo wa sasa imeangukia Ijumaa dakika chache kabla jua halijazama mpaka jumamosi lisaa baada ya jua kuzama, kisha baada ya hapo zinahesabiwa upya siku sita na ikifika ya saba inakuwa Sabato.

Hata Yesu aliikuta siku ya Sabato, aliiabudu, aliisifia na kuitetea (Marko 2), miaka nenda rudi hado sasa ukienda Israel wanaendeleza huu utaratibu, siku ya jumamosi maduka hufungwa na shughuli nyinginezo husimama.

Yesu ni Pumziko letu kiroho hata tunapofanya kazi nzito tukiwa hoi taaban lakini siku ya sabato tunaweka kando shughuli hizo tunapumzisha na miili

sabato ya kweli iko rohoni;Huwezi kwenda mbinguni just kwa kupumzika na kustarehe tuu peke yake.Haya ni mambo ya sheria za Musa.Ndiyo maana sheria ilisema mtu akifumaniwa apigwe mawe mpaka kufa.Fanya kazi siku sita siku ya saba pumzika.Ile kwamba unapumzika kwa ajili ya ibada nadhani kwa mawazo yangu inatosha.Ikiwa jumapili jumamos inatosha.Kikubwa uwe mtu mwenye hofu ya Mungu ya kweli ndani yako na siyo kuugiza
 
Back
Top Bottom