Ni kwanini amri ya kuiabudu siku ya sabato tangu enzi za Musa hadi sasa ni jumamosi lakini makanisa mengine huabudu jumapili?

Najua ila why jumamosi??
Sidhani kama wayahudi walikua wanaziita jumatatu/jumanne mpaka jumapili walikua na lugha yao!
Sasa nataka kujua aliekuja kuvumbua kwamba sabato ni jumamosi isiwe ijumaa au juma3 ni nani? Maana sabato maana yake siku ya saba ya awali ambayo Mungu alipumzika baada ya kukamilisha uumbaji . Hakuna mahala ilitajwa ni jumamosi ama lazima iwe jumamosi!
Siku ni nuru na giza vikipita, Mungu aliumba dunia kw siku 6 ya 7 alipumzika, hivyo baada ya siku 7 unaanza upya kuhesabu, maneno ya jumamosi na jumapili yalikuja baadae/

Musa alipopewa amri kumi alishaelekezwa siku ipi itakuwa ya saba ya kuanza rasmi kuiabudu Sabato ambayo kwa sasa ni Ijumaa dakika chache kabla jua halijazama mpaka jumamosi lisaa baada ya jua kuzama
 
Nimesoma Bible mwanzo mpaka ufunuo, hakuna neno jumamosi wala jumapili.
Mungu aliamuru kuwa siku ya saba iwe siku ya sabato, maana yake watu wa Israel wanaweza kuamua kuwa jumamosi ndiyo siku yao ya saba na itakuwa sabato.
Watu wa America wanaweza kuamua alhamisi iwe siku yao ya saba na hivyo ikawa sabato.
 
Mambo ya kujua dunia ina siku tayari yalikuwemo kwenye maagano ya kale, nuru na giza ndio siku moja, siku ya 7 Mungu akapumzika ni kwamba baada ya hapo huanza upya kuzihesabu.

Na sio kwamba ni jumamosi bali kwa muda mwingi inaangukia jumamosi,

Sabato inaanza jua linapokaribia kuzama siku ya ijumaa mpaka jumamosi lisaa baada ya jua kuzama.

Mungu anajua mwenyewe kwanini aliamua iwe hivi na ndio utaratibu uliofatwa na kina Musa na Yesu.
Weka aya ya Biblia inayoeleza kuwa sabato inaanza IJUMAA jioni mpaka JUMAMOSI.
 
Wasabato walimuua Yesu ili wasali KWA uhuru jumamosi yao Yesu akiwa kaburini
Kama Yesu alifufuka jumapili na ndio siku ya Bwana wa Sabato
Ndio siku ambayo Bwana alikuwa na furaha ya kuukomboa ulimwengu
 
Nimesoma Bible mwanzo mpaka ufunuo, hakuna neno jumamosi wala jumapili.
Mungu aliamuru kuwa siku ya saba iwe siku ya sabato, maana yake watu wa Israel wanaweza kuamua kuwa jumamosi ndiyo siku yao ya saba na itakuwa sabato.
Watu wa America wanaweza kuamua alhamisi iwe siku yao ya saba na hivyo ikawa sabato.
Siku ni nuru na giza vikipita, Mungu aliumba dunia kw siku 6 ya 7 alipumzika, hivyo baada ya siku 7 unaanza upya kuhesabu, maneno ya jumamosi na jumapili yalikuja baadae/

Musa alipopewa amri kumi alishaelekezwa siku ipi itakuwa ya saba ya kuanza rasmi kuiabudu Sabato ambayo kwa sasa ni Ijumaa dakika chache kabla jua halijazama mpaka jumamosi lisaa baada ya jua kuzama
 
Moja ya amri kumi ni kuabudu siku ya sabato, Siku takatifu iliyotengwa na Mungu kuturuhusu KUPUMZIKA nasi tunamshukuru kwa kujumuika kwenye shughuli za kumshukuru na kumuabudu kisha tunarudi makwetu kupumzika, Kila siku ni siku ya Mungu lakini sio kila siku ni sabato kwasababu si kila siku ya kupumzika, kazi nazo muhimu.

Ni tangu enzi za Nabii Musa alieshuka na amri 10 aliabudu sabato siku ya Jumamosi, Hata Yesu aliikuta siku hio na kuiabudu na hadi sasa ukienda Israel siku ya jumamosi maduka hufungwa.

Inashangaza kuona baadhi ya wakristo wanaabudu jumapili wakati sio siku ya sabato
Ulijuaje kama Sabato ni siku ya Jumamosi na wala siyo Ijumaa aua Jumapili; leta ushahidi.
 
Hiyo Amri ya Sabato ni siku ambayo Wana wa Israeli waliamriwa katika Torati kupumzika shughuli zote za mikono,(Kutoka20:8-10)
Ile Siku haiko tena,ile ilikuwa Kivuli cha Ile Sabato ya Kweli iliyokuwa inakuja,
(Wakolosai2:16-18)
(Waebrania4:4-9)
Katika Agano Jipya sasa kila iitwapo LEO ni Sabato,Yesu Kristo ndiye Sabato (Pumziko) yetu! Alikuja kutupumzisha na kutuweka huru mbali na Utumwa wa dhambi,na anasema
(Mathayo11:28-29)
(Yohana8:34)
Kwa kuwa Yesu Kristo ni Yeye yule yule Jana,LEO hata Milele,tumpelekee mizigo ya dhambi (tumwamini ili atupumzishe na kutuweka huru)
Kwa maana hiyo hatushiki Siku au Miezi au Mwaka,hayo ni Mafundisho Manyonge,tunamshika Yesu ambaye ndiye BWANA wa Sabato,(Wagalatia4:8-11)
Siku zote ni za Kumwabudu,Kumsifu na Kumtukuza Mungu,(Matendo2:46-47)
 
Siku ni nuru na giza vikipita, Mungu aliumba dunia kw siku 6 ya 7 alipumzika, hivyo baada ya siku 7 unaanza upya kuhesabu, maneno ya jumamosi na jumapili yalikuja baadae/

Musa alipopewa amri kumi alishaelekezwa siku ipi itakuwa ya saba ya kuanza rasmi kuiabudu Sabato ambayo kwa sasa ni Ijumaa dakika chache kabla jua halijazama mpaka jumamosi lisaa baada ya jua kuzama
Kwahiyo mimi nikiamua kufanya kazi kuanzia jumatano halafu alhamisi nikapumzika na kumuabudu Mungu kwa kufuata sheria zote za sabato je nitahesabiwa haki,au nitahesabiwa dhambi kwasababu sijasali jumamosi kama wayahudi?
 
Ulijuaje kama Sabato ni siku ya Jumamosi na wala siyo Ijumaa aua Jumapili; leta ushahidi.
Siku ni nuru na giza vikipita, Mungu aliumba dunia kwa siku 6 ya 7 alipumzika, hivyo baada ya siku 7 inaanza upya siku ya kwanza, Musa alipopewa amri kumi alishaelekezwa siku ya kuanza rasmi kuiabudu Sabato ambayo kwa mfumo wa majina ya kisasa ya siku huanza Ijumaa dakika chache kabla jua halijazama mpaka jumamosi lisaa baada ya jua kuzama, ndio maana huwezi kukuta neno jumamosi wala ijumaa kwenye biblia.
 
Sio kila kitu kimerekodiwa kuhusu kila kitu Musa alipoenda patakatifu, Ni maelekezo aliyopewa kwamba siku flani ndio itaanza kuwa sabato rasmi kwajili ya amri ya kuabudu siku hio, na haya maneno ya siku kama jumamosi na jumapili yalikuja baadae sana ndio maana huwezi yakuta kwenye maandiko
 
Wasabato walimuua Yesu ili wasali KWA uhuru jumamosi yao Yesu akiwa kaburini
Kama Yesu alifufuka jumapili na ndio siku ya Bwana wa Sabato
Ndio siku ambayo Bwana alikuwa na furaha ya kuukomboa ulimwengu
that is muslim way umetumia lie lie lie only stupidy anaweza kuamini upuuzi wako... umefundishwa msikitini au kwa waganga wa kienyeji? ukiongopa unaitwa Devil even Jesus alimuita Peter Shetani kajifunze maandiko yanasemaje na siyo ku fabricate upuuzi hadharani.. ili iweje watu wacheke au kudaganya uma?
 
Hiyo Amri ya Sabato ni siku ambayo Wana wa Israeli waliamriwa katika Torati kupumzika shughuli zote za mikono,(Kutoka20:8-10)
Siku ya sabato ni amri na amri 10 ni kwajili ya wote sio waisrael tu.
Ile Siku haiko tena,ile ilikuwa Kivuli cha Ile Sabato ya Kweli iliyokuwa inakuja,
(Wakolosai2:16-18)
(Waebrania4:4-9)
Wakolosai2:16-18 zinazungumziwa sikukuu za sabato zilizofanyika kila mwaka kama ilivyo kwa ezekieli 45:17, wala sio sabato ya kila wiki iliyowekwa kwenye amri.

Waebrania 4:4-9: soma na mistari inayofuate 10 na 11 "kwa maana, mtu anayeingia katika pumziko la Mungu, pia hupum zika kutoka katika kazi zake kama vile Mungu alivyopumzika baada ya kazi zake. 11 Basi tujitahidi kuingia kwenye pumziko hilo (sabato) asije mtu akaanguka kwa kutokuamini kama hao."

Katika Agano Jipya sasa kila iitwapo LEO ni Sabato,Yesu Kristo ndiye Sabato (Pumziko) yetu! Alikuja kutupumzisha na kutuweka huru mbali na Utumwa wa dhambi,na anasema
(Mathayo11:28-29)
(Yohana8:34)
Kumwamini Yesu ni Pumziko letu hata tunapofanya kazi nzito lakini Sabato inahitaji pumziko la mwili pia, Utaacha shughuli zako upumzike na kuabudu.

Pia hata Yesu aliitambua Sabato kuwa siku maalum takatifu naye akiiabudu, kuisifia na aliitetea pale aliposhambuliwa na mafarisayo. (Marko 2)
 
Kila mtu ashinde match zake hapa duniani , biblia zenyewe zipo aina nyingi

USSR
Zinatakiwa kuwa nyingi zaidi kulingana na kasi ya dunia inavyoenda, wingi wake ni maboresho wala hakuna madhara, ni kama yalivyo majina, unadhani tutaendelea kuwa na majina ya kizamani.
 
Moja ya amri kumi ni kuabudu siku ya sabato, Siku takatifu iliyotengwa na Mungu kuturuhusu KUPUMZIKA nasi tunamshukuru kwa kujumuika kwenye shughuli za kumshukuru na kumuabudu kisha tunarudi makwetu kupumzika, Kila siku ni siku ya Mungu lakini sio kila siku ni sabato kwasababu si kila siku ya kupumzika, kazi nazo muhimu.

Siku ni nuru na giza vikipita, Mungu aliumba dunia kwa siku 6 ya 7 alipumzika, hivyo baada ya siku 7 inaanza upya siku ya kwanza, Musa alipopewa amri kumi alishaelekezwa siku ya kuanza rasmi kuiabudu Sabato ambayo kwa mfumo wa majina ya kisasa ya siku huanza Ijumaa dakika chache kabla jua halijazama mpaka jumamosi lisaa baada ya jua kuzama, ndio maana huwezi kukuta neno jumamosi wala ijumaa kwenye biblia.

Utaratibu huu umekuwa ukifuatwa tangu enzi za Musa, Yesu aliikuta aliabudu kwa utaratibu huo huo na hadi sasa ukienda Israel siku ya jumamosi maduka hufungwa.

Inashangaza kuona baadhi ya wakristo wanaabudu jumapili wakati sio siku ya sabato
Sijawahi kuelewa ni kwa nini watu hupenda kwenda kinyume na maagizo ya Mungu tena yanayotekelezeka kirahisi
 
Cha msingi ni kumuabudu Mungu wa kweli.

Dhehebu, siku ya kuabudu (Jmosi, Jpili n.k) sio tiketi ya kwenda mbinguni.

Aidha, siku ya sabato ni ipi hasa?. Siku ya kwanza katika juma ni ipi?, siku ya saba ni ipi?, yaani ni jumaa ngapi?.
 
Moja ya amri kumi ni kuabudu siku ya sabato, Siku takatifu iliyotengwa na Mungu kuturuhusu KUPUMZIKA nasi tunamshukuru kwa kujumuika kwenye shughuli za kumshukuru na kumuabudu kisha tunarudi makwetu kupumzika, Kila siku ni siku ya Mungu lakini sio kila siku ni sabato kwasababu si kila siku ya kupumzika, kazi nazo muhimu.

Siku ni nuru na giza vikipita, Mungu aliumba dunia kwa siku 6 ya 7 alipumzika, hivyo baada ya siku 7 inaanza upya siku ya kwanza, Musa alipopewa amri kumi alishaelekezwa siku ya kuanza rasmi kuiabudu Sabato ambayo kwa mfumo wa majina ya kisasa ya siku huanza Ijumaa dakika chache kabla jua halijazama mpaka jumamosi lisaa baada ya jua kuzama, ndio maana huwezi kukuta neno jumamosi wala ijumaa kwenye biblia.

Hata Yesu aliikuta, aliiabudu, aliisifia na kuitetea (Marko 2), miaka nenda rudi mpaka sasa ukienda Israel siku ya jumamosi wanaabudu Sabato maduka hufungwa na shughuli nyinginezo husimama.

Yesu anaweza kuwa Pumziko letu kiroho hata tunapofanya kazi nzito lakini siku ya sabato tunahitaji pia pumziko la mwili, akili, n.k.
Inaabudiwa siku au mtu anaabudu kwenye siku hiyo? Pia Yesu alisema kuanzia sasa waabuduo halisi wataabudu kwenye roho na kweli. Siku haikuwekwa kama kigezo cha kuabudu halisi.
 
Siku ni nuru na giza vikipita, Mungu aliumba dunia kwa siku 6 ya 7 alipumzika
Yaani kabisaaa,kwa akili zako timamu unaamini MUNGU kwa uweza wake mkuu alionao,usiopimika wala kuchunguza kwa akili ya kibinadamu,alifanya kazi siku 6,ya saba akawa amechoka hoiiii.
Tuachane na akili zetu finyu kabisa.Tatizo Binadamu tunamfananisha MUNGU na miili yetu dhaifu ya nyama.
Kwa ukuu alionao MUNGU,hajawahi choka,hachoki na hatakuja kuchoka.That's why the Universe is still expanding at the speed even greater than the speed of light.
MUNGU wetu ni mkuu,fanya kazi zako,ila usisahau kumtengea at least siku moja ya kumuabudu na kumtukuza,haijalishi itakuwa lini.
 
Ndiye

Musa aliepewa amri 10 kutuletea, akiwa huko patakatifu, alielekezwa sabato iwe jumamosi na ikawa hivyo
Aliyekuwepo kushuhudia anapewa hizo amri ni nani? Hizo unazoziita amri ni taratibu zilikuwepo almost kwenye jamii zote labda kwa utofauti kidogo kulingana na mila na desturi.
 
Siku ni nuru na giza vikipita, Mungu aliumba dunia kw siku 6 ya 7 alipumzika, hivyo baada ya siku 7 unaanza upya kuhesabu, maneno ya jumamosi na jumapili yalikuja baadae/

Musa alipopewa amri kumi alishaelekezwa siku ipi itakuwa ya saba ya kuanza rasmi kuiabudu Sabato ambayo kwa sasa ni Ijumaa dakika chache kabla jua halijazama mpaka jumamosi lisaa baada ya jua kuzama
"Kwasasa ni ijumaa" alisema Musa?
Kwahiyo Musa alisema siku ya saba ni Jumamosi
 
Back
Top Bottom