Moja ya amri kumi ni kuabudu siku ya sabato, Siku takatifu iliyotengwa na Mungu kuturuhusu KUPUMZIKA kwa kuziweka kando shughuli zetu na tunashukuru kwa kujumuika pamoja kwenye shughuli za kuabudu ikiwa ni ishara ya shukran kisha tunarudi makwetu kupumzika, Kila siku ni siku ya Mungu lakini sio kila siku ni sabato kwasababu si kila siku ya kuacha shughuli zako kupumzika.
Mfumo wa kutambua siku upo tangu zamani lakini hakukuwa na majina ya kisasa ya siku kama jumamosi na jumapili ndio maana huwezi yakuta hayo majina kwenye biblia, Musa alipopewa amri kumi ikiwemo ya siku ya sabato alishaelekezwa siku rasmi ya kuanza kuiabudu Sabato ambayo kwa mfumo wa sasa imeangukia Ijumaa dakika chache kabla jua halijazama mpaka jumamosi lisaa baada ya jua kuzama, kisha baada ya hapo zinahesabiwa upya siku sita na ikifika ya saba inakuwa Sabato.
Hata Yesu aliikuta siku ya Sabato, aliiabudu, aliisifia na kuitetea (Marko 2), miaka nenda rudi hado sasa ukienda Israel wanaendeleza huu utaratibu, siku ya jumamosi maduka hufungwa na shughuli nyinginezo husimama.
Yesu ni Pumziko letu kiroho hata tunapofanya kazi nzito tukiwa hoi taaban lakini siku ya sabato tunaweka kando shughuli hizo tunapumzisha na miili